Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Haa ha ha ha, hi ndio tunaitaga, "MGANGA HAOMBAGI TEMBELE"
 
haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Upo humu jf kama member halafu unatapiliwa kirahisi hivyo?? kwanini hukuuliza kuepukana na hilo kuuliza sio ujinga ni kupata maarifa fulani fulani, , pili kuna uzi uliozungumzia sana namna ya kupata kiwanja halali pasipo kutapeliwa njia za kutumia kukwepa mitego
 
Kwa hiyo mkataba wa mauziano, ofisi ya mtaa na mashahidi hawatambuliki kabisa, anayetambulika atakuwa nani sasa?
Mkuu kwenye sheria ya ardhi, hao hawatambuliki kabisa kwenye kuuziana , labda kama ni ardhi ya kijiji.
Anayetambulika ni hakimu, na mawakili tu, ndio wanaoweza kusimamia mauziano hayo na yakawa na nguvu ya kisheria.zile hati za serikali za mtaa ni makaratasi tu, ambayo kisheria hayana nguvu kabisa.Ukiwa nalo hilo halafu akaja mtu akauziwa hicho kiwanja chako tena na akawa na hati ya mauziano yaliyosimamiwa na wakili, huwezi kushinda hiyo kesi kwa kuonyesha hizo karatasi.
 
Point muhimu Bexb, zungumzia viwanja vya vyenye migogoro ya kifamilia.
Nime'edit kidogo, pitia tena. Ila mkuu hata kama kiwanja umekipenda vipi, endapo tu ukasikia kuwa kuna mgogoro wa kifamilia USINUNUE narudia tena USINUNUE kwani wewe mnunuzi utakua kwenye upande mgumu zaidi
 
Watu wanatapeliwa huku wakiwa na hati original toka wizarani, sembuse hivyo vipeperushi vya ofisi ya mtendaji!!kwa taarifa yako kisheria kwenye mauziano ya ardhi hakuna sehemu iwe, mwenyekiti, ama mtendaji anatambulika kuwa atayasimamia.
Huwa nashangaa sana, yaani unakuta eti jamaa msomi kabisa yupo busy eti tumeuziana na shahidi ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa😂😂😂😂😂 kinachoniuma zaidi hao wenyeviti wanakula 10% ya mauzo ghafi dah! Huwa natamani kuwatia hata makofi wanunuzi wa namna hiyo.
 
Nime'edit kidogo, pitia tena. Ila mkuu hata kama kiwanja umekipenda vipi, endapo tu ukasikia kuwa kuna mgogoro wa kifamilia USINUNUE narudia tena USINUNUE kwani wewe mnunuzi utakua kwenye upande mgumu zaidi

Wakati mwingine hujui kama kuna mgogoro wa kifamilia. Ukiongeza hicho kipengele kitawasaidia wengi.n
 
Asante sana mkuu kwa kuendelea kuwafumbua macho. Utakuta kiwanja kinauzwa 50M, mwenyekiti anapewa eti 5M ya kusimamia mauzo halafu ukishauri akamwone wakili anasema wakili gharama wakati wangeweza hata kumomba kumlipa hata 3M na kuepusha hasara inayoweza kutokea mbeleni
 
Pole sana mkuu,serikali ya mtaa si waliweka sign?wanasemaje??

Aliekuuzia yupo?
 
Ni rahisi sana mkuu hili suala ukimshirikisha wakili atakuongoza vizuri Sanaa na utapunguza chances za kuingia kwenye hasara. Mfano umeambiwa hii nyumba ni ya familia na mimi ndiye kiongozi wa familia, simple tu unamwambia mimi nawataka wanafamilia wote wawepo. Wakati huo unapita hata kwa majirani wawili watatu kuuliza kuhusu idadi ya wanafamilia, uzuri sisi watanzania tutakunyima mchongo wa hela lakini sio umbea😂😂😂😂😂
Wakati mwingine hujui kama kuna mgogoro wa kifamilia. Ukiongeza hicho kipengele kitawasaidia wengi.n
 
haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Unatapeliwaje 45m mkuu? Kwani hukujiridhisha kabla ya kuitoa?
 
Muhimu kwa faida ya wengi, kujua jinsi ya kuchukua tahadhari mbalimbali.
 
Mkuu vipi kama ...nimeuziwa kiwanja cha familia na mwanamke ambaye mume wake ameishafariki na waliosaini ni watoto 2 kati ya wanne na mama yao (huyo mwanamke),mwenyekiti na katibu wao pia....hapo kuna hitilafu....???
 
Nakazia...

Hata Serikali za Mitaa siku hizi nao ni wale wale tu...
Wanachojali ni ile asilimia yao.. likikupata janga huko unapambana mwenyewe..
 
Nakazia...

Hata Serikali za Mitaa siku hizi nao ni wale wale tu...
Wanachojali ni ile asilimia yao.. likikupata janga huko unapambana mwenyewe..
Mkuu sio kwamba serikali ya mtaa hawakusaidii ila HAWANA MAMLAKA WALA UWEZO WOWOTE WA KUKUSAIDIA KWA LOLOTE KISHERIA. Labda iwe hiyo ni ardhi ya kijiji, ila kama ni ardhi binafsi aisee hao ni sawa na hakuna. Wakili ama hakimu ndio maafisa pekee wanaoruhusiwa kusimamia mikataba ya mauziano ya ardhi.
 
Mkuu vipi kama ...nimeuziwa kiwanja cha familia na mwanamke ambaye mume wake ameishafariki na waliosaini ni watoto 2 kati ya wanne na mama yao (huyo mwanamke),mwenyekiti na katibu wao pia....hapo kuna hitilafu....???
Mkuu kila situation huwa inaamuliwa kwa namna yake. Katika sheria ya mikataba Tanzania kuna kitu kinaitwa 'voidable contract ' hii ni aina ya mkataba ambao ni halali hadi pale mmoja wa pande za mkataba atakapogundua tatizo na kutoendelea na mkataba, ila akiamua kuendelea nao kunakua hakuna tatizo kisheria.

Sasa kwa wewe sijui kama msimamizi wa mirathi ya marehemu baba mwenye nyumba ni nani na kama kiwanja kilikua cha urithi, na kama kila upande wa urithi umepata mgao wake. Nadhani tukipata maelezo ya kutosha tunaweza kuwa na chochote cha kutoa maoni.
 
Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Kama ni siyo maeneo yaliyopimwa basi hukufikiri kabla ya kutenda. 45ml nunua surveyed area.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…