Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Kufuatia uandishi wako...!

1.Wewe ni mtu mzima mwenye umri kati ya 35-40
2.Uliingia kwenye mahusiano na mume wa mtu
3.Ulikuwa una tafuta mume Kwa mhemuko wa kuzaa
4.Hakuna mimba ya bahati mbaya kwenye umri wako ,ulikuwa unajua unacho kufanya
5.Mwanaume alikuwa ana stress zake na hustling zake za maisha hakuwa serious
Watabiri wengi wao ni wachawi

Niko palee
 
Maskini pole
Ila shida anaweza tokea msamalia kijana wa watu akakusaidia, bahati mbaya aka fall in Love kwako akakubali na kulea Mtoto.

Ila ukijifungua tu mtoto akikua kua na Baba mzazi yule aliekukimbia siku akisema anataka kuona mtoto.

Utasahau shida hizi zote, hadi aliekusaidia na kukupenda siku zako za uhitaji.

Na mbaya zaidi uta kimbia kimbia mbio kumpelekea Mtoto na utampanulia mapaja tena.

Inasikitisha Sana.

Ila Pole Sana Kiongozi, Mungu atakulinda katika kipindi hiki, ni mapito tu na utavuka salama maana Fadhili zake ni za milele.
 
Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia kompu1ta vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.
Laiti ungetumia condom yote haya yasingekupata. Salama Condom ni Tsh 1 000 unapata 3.

Halafu hauko serious katoka mahusiano. Unatafutaje mwanaume JamiiForums? No regrets kwa yaliyokukuta
 
Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia komputa vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.
Pole sana, Mungu akusaidie sana.
 
Back
Top Bottom