Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Habari za mida hii ndugu wananchi, kifupi mimi siyo mtaalamu wa wanyama ila ni mpenzi na mfuatiliaji wa masuala ya wanyama na makala zao kupitia TV na mitandao.

Nimetembea mikoa karibu yote Tanzania ila nimegundua kuwa dodoma ndo mkoa wenye NYOKA wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania. Pia nimekutana na watu wengine ambao pia wanadai dodoma hakufai, kisa wingi wa NYOKA.

Hii ni orodha ya nyoka ''HATARI" niliowaona kwa macho yangu katika ardhi ya Dodoma.

Koboko (black mamba)
Swila wa msituni (forest cobra)
Nyoka kijiti (twig snake)
Boomslang
Kifutu (puff adder)
Kifutu magamba (saw scalled viper)
Swila mweusi (spitting cobra)

THIBITISHENI AU BATILISHENI HILI KUHUSU DODOMA.
Umefika Nachingwea Mkuu??
 
dodoma ni ccm
 
Nasikia wale nyoka wa nachingwea waliletwa kwaajili ya kumaliza panya kwenye mashamba ya wazungu ya karanga wakaisha panya imebaki kero ya nyoka had leo
Ni kweli. Ila kuna sehemu zenye nyoka zaidi. Kuna jamaa yangu alifiwa na baba yake huko Nachingwea. Ilikuwaje? Baba aligongwa na nyoka akiwa shambani analima. Ktendo cha alikuwa nao kutoka shambani kwenda kutafuta bodaboda na wa kumpeleka hospital akawa ameshafariki. Sikujua ni nyoka gani alimgonga.
 
Ni kweli. Nilisoma Bihawana miaka ya mwanzoni mwa 2000. Kukutana na nyoka wakati tunaelekea kwenye shamba la shule ilikuwa kawaida kabisa. Kipindi cha kiangazi rangi zao zinablend na majani makavu yaloanguka.
 
Back
Top Bottom