Namshakende
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 867
- 2,275
Wakuu habari za wakati huu.
Naandika uzi huu nikiwa kwenye wakati mgumu wa kifikra kuhusu namna ya kusimamia fedha zangu. Kila nikijaribu kufanya saving (akiba) nashindwa. Sielewi hela naipeleka wapi, na mwisho wa siku hakuna kitu cha msingi cha maana ambacho nimefanya au nimefanikiwa kukamilisha. Mwezi unapoisha najikuta sina kitu kabisa.
Ili kukabiliana na hili, nilikaa chini na kutengeneza Expenses Tracker ya Excel ambayo imenisaidia kwa kiasi fulani. Kwenye hii tracker, kila jioni kabla ya kulala huwa najaza matumizi yote niliyofanya siku hiyo hata kama ni ya shilingi mia moja.
Pia, niliweka mfumo kwenye hiyo tracker ambapo matumizi yangu yakizidi asilimia 40 (40%) ya kipato changu, seli inabadilika na kuwa nyekundu, na chini ya hapo inakuwa kijani (kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini).
Hata hivyo, pamoja na kuweka utaratibu huu wa kuandika matumizi kila siku, bado siridhishwi na mwenendo wa matumizi yangu na ninajikuta nashindwa kuweka akiba ya maana.
Kama kijana ambaye sina mke wala mtoto na ninaishi peke yangu, nahisi nina nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kifedha lakini nashindwa kupata msimamo.
Wakuu wa JamiiForums, naombeni mbinu, elimu ya fedha (saving literacy), na ushauri wenu:
NB: Picha hapo chini ni sample tu

- Ni mbinu gani za ziada za kisaikolojia au kiutendaji naweza kutumia ili kuacha matumizi yasiyo ya lazima?
- Ni mfumo gani mzuri wa kugawanya kipato (kama vile kanuni ya 50/30/20 au mingineyo) unaoweza kufanya kazi kwenye mazingira yetu?
- Nifanye nini ili hii tracker yangu ya Excel iweze kutoa matokeo chanya kwenye akiba yangu badala ya kuishia kuona tu rangi nyekundu ikigonga kila mwisho wa mwezi?
NB: Picha hapo chini ni sample tu