Nimetengeneza mfumo wa usimamizi wa makanisa

Nimetengeneza mfumo wa usimamizi wa makanisa

herman3

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
556
Reaction score
736
Habarini ndugu wa jukwaa hili la Tech, nimeleta mfumo wa usimamizi wa taasisi za kidini hususani makanisa.
Kwa kipindi kirefu taasisi nyingi za kidini hasa makanisa hayajawa na mifumo rasmi ya usimamizi wa taarifa zake. Hivyo nikaamua kuunda mfumo ambao utawezesha hilo ambapo kwa sasa mfumo huu unakuwezesha kufanya yafuatayo:

1. Kusimamia taarifa za washirika/waumini

2. Kusimamia taarifa za mapato (income)

3. Kusimamia taarifa za matumizi (Expenses)

4. Kutengeneza taarifa ya mapato na matumizi (Income & Expenditures report) ya kipindi chochote kwa dakika 1 tuu

5. Kuweza kuwasilisha taarifa yoyote kwa washirika kirahizi zaidi kupitia mfumo wa Bulk SMS (utaweza kutuma SMS kwa watu 1,000 ndani ya dakika 1)

6. Kuweza kuandaa annual work plan kirahisi na kupokea reminder kwa kila activity inapofika

7. Vikundi ndani ya kanisa (mfano vikundi vya vijana, wamama, wababa, watoto n.k), vitaweza kusimamia taarifa zao (taarifa za wanakikundi, taarifa za mapato na matumizi ya kikundi, taarifa za biashara ya kikundi kama ipo, Kuandaa annual work plan na kupata reminders SMS nk)

8. Kupitia CMIS utaweza kuhifadhi taarifa za kila mahudhurio ya washirika kwenye kila ibada

9. Utafutaji wa taarifa ni rahisi zaidi kuliko taarifa zilizo hifadhiwa kwenye vitabu au MS Excel

10. Taarifa zote zinazotunzwa kwenye CMIS haziwezi kupotea kwa kuwa zinahifadhiwa mtandaoni hivyo utazipata tena hata baada ya computer yako kupata tatizo
11. Uhifadhi wa document zote za taasisi.

Karibuni kuujaribu mfumo huu unaopatikana kwa address hii churchMIS - Church Management Information System

UPDATES

Kuna wengi ambao mmekuwa mkihitaji account ya majaribio, sasa ili kuepusha usumbufu wa kusajili account na kufuta nimetengeneza account za majaribio ambazo kila mmoja anaweza kuzitumia

account ya Finance
churchID 1096
Phone 255742600079
Passwors 1122

Account ya administrator
churchID 1096
Phone 255759891571
password 1122
 
Hapo kwenye kipengele Cha sadaka ungeweka na password ya mchungaji pekee aweze ona wasione wote

Maana sadaka ndio lengo la kuanzisha kwa makanisa meng ya manabii na makuhani
Iko hivyo, kuna roles 4
1. System admin
2. Finance
3. Pastor
4. Other Leader

kila mmoja yupo limited kwa taarifa ambazo anaruhusiwa kuona
 
kama una mahitaji maalumu zaidi ya kile ambcho kipo kwenye mfumo kwa sasa unaweza nijulisha tutafanya customization kwaajili yako
 
Vipi kuhusu app ya mauzo/manunuzi/matumizi kwa wajiriamali au maduka madogo
 
Back
Top Bottom