Nimetengeneza milioni 30 faida ya kilimo ndani ya miaka 3

Nimetengeneza milioni 30 faida ya kilimo ndani ya miaka 3

ukiwa hujawahi shika hela flani kuna hela ukitajiwa unaziona nyingi sana sana

30m ndani ya miezi 6 = na 5m kwa mwezi ambayo ni sawa na 166 > 170k kwa siku

170k ni hela (faida) ambayo inapatikana kwa kuuza bidhaa 1 tu ya electronic Just 1 piece (eg: tv)

calculate kwa siku mtu anauza tv si chini ya 3,achana na electronics zingine na biashara zingine zenye faida tofauti.

hujaweka vibiashara uchwara vingine mtu anafanya,hilo ni duka 1 tu..unaongelea 30m unaona ni hela nyingi sana?

hiyo ni hela imetolewa tu mfano kulingana na level ya mtoa mada ila tukisema tuweke uhalisia wa Mtu mwenye akili na mtaji anatakiwa aingize kiasi gani kwa mwezi/miezi 6 watu wataguna mpka makoo yawaume.
We dogo endelea kutapeli mademu
 
Hata hivyo sijaleta uzi kuwa inspire nyie matajiri wakubwa, uzi wangu unawalenga vijana ambao hawana mitaji wanaoweza kujiajiri kupitia kilimo.
Safi Sana, nakupongeza kwa comnent na pia upambanaji wa kutafta ela, anayeona milioni 30 ni ndogo apite kushoto. Kimfaacho mtu, chake
 
Hapana hata kwa sekunde/dakika/saa/siku/wiki/mwezi/mwaka

Tulio wengi tunaishi kwa kuhesabu kuanzia mwezi,ni wachache hasa

tulio wafanyabiashara mapato yetu tunayahesabu kwa siku,ni vile tu unaamua

uwekeje hesabu zako ili upate jibu la kiasi ulichopata katika kazi husika ya kujiongezea kipato.

Mkuu unavyoishi wew sio kila mtu anaishi hivo
We uko sahihi na life yako na wao wako okay
Suala la kiasi kwa mwezi ni kila mtu ananjia zake Za kupata hatueZi kua sawa
Ungempa pongezi na sio kuanza kuponda hustling akat huezi hata mpa kazi akiacha kilimo
 
Wewe umejuaje nimetumia nguvu na akili nyingi?
Mkuu hakuna ubaya wala kosa kwa wewe kutumia nguvu na akili nyingi...huna sababu ya kujieleza kwa huyo kijana!

Endelea kuchapa kazi...mafanikio huja kwa nguvu na jasho jingi, hawa vijana wanadanganyana ndiyo maana wengi wapo kwenye ujinga wao wanaita sijui forex na wengine kubet.

850k kwa mwezi ni pesa nyingi sana. Ukitaka kujua hivyo...mpigie simu jamaa yako yoyote unayemjua mwambie una shida ya laki 8 uone visingizio atakavyokupa...[emoji2]..piga kazi mkuu!
 
Mkuu hisia zangu ni kuwa wanaopinga wengi watakuwa watumishi sio wafanya biashara. Mtumishi anasahau kuwa hio laki nane na ushehee au milioni+ anaisotea mwaka mzima, ili kupata milion 30 anakuwa amefanya kazi non stop miez 30. Wakati huyu mkulima analima kwenye misimu tu, mda mwingine anapumzika na kuwa huru.
Nguvu na akili nyingi inatumika jwa watumisha saba tu ila wengi wanadgani wanalia kivulini.
Watumishi kwa suala la muda tu ukilinganisha na kipato wanapata kidogo sana.
Mwenzeyu huyu ina maana stage ya pili anaenda kutengeneza milion 60.
If he will grow exponentially after five year abaweza kuwa na milioni 300 wakati mtumidhi au muajitiwa la bda jaongezewa ailimia tano ya kipato chake ie 35 millions kwa ile ile miezi.
Kwenye utumishi hakuna ku grow exponentially labda upate cheo.
 
Unaweza kuwa mkulima na bado ukaajiriwa.
Mkulima ni Mkulima na muajiriwa ni muajiriwa. Usichanganye hivi vitu? Utawapoteza wenzako.
Labda kama unaongelea kuajiriwa serikali hasa huko Halmashauri.
Serikalini ndiyo ukipata ajira unakuwa kama umewahi namba, ukisha sign mkataba unaweza enda kitaa au popote pale kuendelea na mishe zako nyingine wakati ukisubiri muda wa kustaafu bile kufanya kazi au kustaafu baada ya kuhudhuria vikao na training, semina ziara kwa miaka yote uliyokuwa kazini
 
Bila kufanya kazi hiyo serikali ya wapi?
 
Nimeanza kulima serious toka mwaka 2019, nikilima mahindi na viazi vitamu ndani ya misimu mitatu yaani toka 2022 mpaka sasa nimeweza kutengeneza faida ya 30M kupitia kilimo cha mahindi, viazi vitamu, na maharage.
Kwa hakika kilimo ni biashara tamu.

Nawashauri vijana wenzangu mchangamkie fursa.
Kwa kijana anayeshinda kijiweni asiyeelewa anaanzia wapi , 30 M si pesa ya kubeza, nikupe hongera ndugu....

Tunachokiomba ni mchanganuo wa gharama kwa ujumla, ili kijana anyetamani kuingia kwa kilimo ajue anaanzia wapi, vema ungetuleza ulianza na mtaji wa pesa ngapi, uchaguzi wa mbegu, maandalizi ya shamba, utunzaji wa mazao hadi masoko....

Hongera kwako...
 
Matajiri wa jf ni matajiri tu wakiwa wamejificha nyuma ya key board!! wanabeza faida ya m10 kwa mwaka!! lakini utakuta wengi wanashinda wakibet kwenye mitandao!!
 
Back
Top Bottom