Nimetengeneza milioni 30 faida ya kilimo ndani ya miaka 3

Nimetengeneza milioni 30 faida ya kilimo ndani ya miaka 3

Kubwa inategemeana unafanya reference ipi.
Una uwezo wa kuwawezesha watanzania wangapi Kama unajua hela nyingi Ni ipi Basi angalau watanzania laki moja wapate hata 15M ndani ya miaka iyo mitatu? Ama just your ego iko kazini. Wewe umemchukulia negatively mleta maada Kama akaleta majigambo fulani na ilhali sio ivyo kabisa . Sema negative mind Ina seek negative and weakness tu Vice versa haiwezi kudadavua. Yaani kwanza wewe kwenda hata kwa watt yatima ukawanunulia chakula Cha laki moja huwezi ama usomeshe Basi mmoja angalau Hadi chuo kikuu huwezi Ila unaiona iyo pesa Ni ndogo. Hapo ulipo huwezi ukaombwa alfu moja ukatoa bila ya kutaka kuiulizia Ni ya Nini.
So lower your ego be humble otherwise nature will humble you
Umemwambia Kwa usahihi.
 
Acha kutoa siri za jeshi. Sisi tulio field tunakuelewa. Wao wamezoea light motivation speakers. Ndani ya humu JF wote ni wajuaji na wako vizuri financially. Niko chimbo nitalima ufuta na karanga mwaka huu nitarudi kama siyo hapa hata Pm tupeane ma ujanja.
Yaan kama upo kichwani kwangu, hii ni project yangu kabisa an lakin ndo naanza sina uzoefu
 
Kwanza kabisa 30M sio hela nyingi za kukufanya uje utupe testimony ukitegemea utatu inspire. Secondly, ume invest how much kuja kupata hio 30M kwa miaka mitatu..? Tudadavulie mahesabu yalivyo mpaka faida ya 30M ipatikane. Thirdly, jaribu kutizama agribusiness pia, ina hela kuliko kulimo. Uki invest vizuri kwenye agribusiness za horticulture, 30M ni hela ya miezi miwili hadi mitatu unaipata.
Duuh
 
Binafsi yangu nampongeza sana huyu Mkulima aliyerudi kutupa ushuhuda wake, na kama amepata faida yoyote( acha hiyo 30m) kwenye kilimo apewe maua yake. Hapa tumechanganya mjadala kati ya madalali wa mjini na wakulima tulioko shambani, hatuwezi kuwa sawa. Mimi kama mkulima, nakupa maua yangu. Endelea kulima. Na hawa wa misheni town waendelee na misheni zao.
 
ukiwa hujawahi shika hela flani kuna hela ukitajiwa unaziona nyingi sana sana

30m ndani ya miezi 6 = na 5m kwa mwezi ambayo ni sawa na 166 > 170k kwa siku

170k ni hela (faida) ambayo inapatikana kwa kuuza bidhaa 1 tu ya electronic Just 1 piece (eg: tv)

calculate kwa siku mtu anauza tv si chini ya 3,achana na electronics zingine na biashara zingine zenye faida tofauti.

hujaweka vibiashara uchwara vingine mtu anafanya,hilo ni duka 1 tu..unaongelea 30m unaona ni hela nyingi sana?

hiyo ni hela imetolewa tu mfano kulingana na level ya mtoa mada ila tukisema tuweke uhalisia wa Mtu mwenye akili na mtaji anatakiwa aingize kiasi gani kwa mwezi/miezi 6 watu wataguna mpka makoo yawaume.
Unajua mtaji wa electronics ? Au unaleta hadithi za Sungura na Fisi

Mtaji wa 1 M kwenye kilimo ni mkubwa , ila ukiupeleka kwenye electronics ni ukichaa
 
Milioni 30 ni pesa ndogo kwa nyie matajiri lakini kwa vijana wanaotafuta maisha ni pesa nyingi sana.
Humu Jf bwana kila mtu ni Tajiri akiwa anaandika kwenye keyboard ila kwenye maisha halisi ni masikini wa kutupwa, wewe angalia kila comment unadai 30M ni ndogo ila miongoni mwao kuna watu hawana hata 10M benki.

Nikupongeze kwa jitihada zako kijana mwenzangu, 30M inaonekana ndogo leo ila ukidumu kwenye hicho unachokifanya pengine miaka kumi mbele tutakuwa tunazungumzia BILLIONS.

Utajiri hauji harakaharaka.
 
hamna aliebeza 850,000 ni pesa ndogo,ni hela nyingi sana sana

lakini kwa nguvu na muda na akili ulizotumia 850,000 ni pesa ndogo sana

ulipaswa kwa muda uliotumia akili ulizotumia upate zaidi ya 850,000 kwa mwezi.

kwanini? una sifa ya uvumilivu kama Jibu ni ndio kuna pesa sehemu nyingi sana ambazo

ukiwa na uvumilivu wa miezi kadhaa tu,huwezi kukosa hiyo hela sasa upge miaka mi 3

ungekua unaongelea pesa nyingi sana,hiyo 30m ilipaswa walau uipate ndani ya miezi 6

kwa akili ulizo nazo,muda uliotumia nk lakini matokeo yake umeipata kwa kuchelewa sana.
Tatizo ni ujuaji mwingi mkiwa hapa kwenye anonymity.

850,000Tsh ila yupo katika mkondo mzuri (uzalishaji) wa kupata zaidi kuliko zile biashara za kivivu (uchuuzi) ambazo huwa unaziimba humu.

Ukitumia akili ni lazima ukubali kuwa kuna wakulima ambao wanaingiza pesa ndefu sana (Billions of money), hiyo ni kukuonyesha kuwa hata huyu kuna vitu fulani ambavyo akizingatia atafika huko, kama kijana ulitakiwa umpe ushauri ni nini afanye ili afike huko kupitia hichohicho anachofanya, sio kukashifu.


Mwisho wa siku kila mtu ana njia yake ya kujiingizia kipato.
 
We jamaa ni kiande sana
ukiwa hujawahi shika hela flani kuna hela ukitajiwa unaziona nyingi sana sana

30m ndani ya miezi 6 = na 5m kwa mwezi ambayo ni sawa na 166 > 170k kwa siku

170k ni hela (faida) ambayo inapatikana kwa kuuza bidhaa 1 tu ya electronic Just 1 piece (eg: tv)

calculate kwa siku mtu anauza tv si chini ya 3,achana na electronics zingine na biashara zingine zenye faida tofauti.

hujaweka vibiashara uchwara vingine mtu anafanya,hilo ni duka 1 tu..unaongelea 30m unaona ni hela nyingi sana?

hiyo ni hela imetolewa tu mfano kulingana na level ya mtoa mada ila tukisema tuweke uhalisia wa Mtu mwenye akili na mtaji anatakiwa aingize kiasi gani kwa mwezi/miezi 6 watu wataguna mpka makoo yawaume.
 
Back
Top Bottom