Nimethibitisha jamii inayoongea Kiingereza ina uelewa mkubwa na IQ za juu kulinganisha na waongeaji wa Kiswahili

North Korea wanazungumza kiingereza?
Hili hapa sasa wazi ni tatizo la Kiswahili, wewe huenda unasikiliza the story book kuhusu Kiduku au zile movies za kutafsiriwa ambazo huwa zinawasifia Wakorea na ukaaminishwa kabisa kwamba Korea Kaskazini ya Kiduku ni taifa la maana la kutolea mfano. Fahamu sasa kwamba Tanzania inaweza kuwa bora sana kuliko Korea Kaskazini.
 
Naamini we ni 1 ya wanufaika wa mfumo
 
Russia wanazungumza kiingereza?
Warusi wengi wanajua Kingereza ila wazungumzaji ni wachache, Putin mwenyewe anakielewa Kingereza vizuri japo kuongea sio fluent. Yani Warusi wengi wanaweza kuangalia CNN, Aljazeera au BBC English wakaelewa taarifa vizuri tofauti na Watanzania wengi ambao watakuwa wanaelewa kupitia picha tu.

Halafu mataifa kama Urusi, China, Japan, Korea, India, Uturuki na Ethiopia ni mataifa muendelezo ya mamia ya karne au millenia kadhaa huku wakizungumza lugha moja ya/za kitaifa, kujaribu kuyatumia kama mifano ni ujuha uliopitiliza.
 
Wakati sie watanzania tunajivunia kua raia wa nchi, hatuna la kujivunia zaidi ya Amani na umoja wetu.
Kwanza Tanzania hakuna Amani.

Tanzania kuna Amani uchwara. Amani ya mdomoni tu na kwenye makaratasi.

Mauaji ya albino kama yule mtoto Asimwe, watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kuokotwa kwenye mifuko ya Sandarusi ni mifano tosha kwamba Amani ya Tanzania ni Amani uchwara tu.

Hata kwenye top 100 ya nchi zenye amani duniani Tanzania haifai kuwepo.

Kwa nchi zenye amani Afrika, angalau uniambie Mauritius, Namibia, Botswana at least.
 
Ukishaambiwa Sigara ni hatari kwa afya haina maana kwamba kila mtu atakayevuta sigara atakufa kwa cancer, jiongeze kama unataka kuelewa, ila kama uko kwenye ligi endelea kuuliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Mfano waingereza na waongeaji wa Kiingereza ni watu wenye utamaduni wa kuwa wazi, wakweli na wathubutu. Waswahili wana tabia ya kuwa waoga, waongo na wanafiki.
Huu ni ukweli usiopingika, waswahili tu waoga sana, waongo tunaoukubali uongo, na tuna unafiki mwingi huku tukiwa hatuna maendeleo katika nyanja zote.
 
Mimi ningekuwa na mamlaka, ningeajiri waalimu 20,000 wa hesabu na waalimu 15,000 wa saiyansi; Hiyo habari ya Kiingereza/Englisha tungekutana nayo huko mbele
Wanaofaulu Hesabu na sayansi ndio hao hao wanaongoza masomo ya Arts.
 
East africa uganda ndio wanaongea na kujua kingereza vizuri kuliko kenya unasemaje kuhusu wao.
 
Ukishaambiwa Sigara ni hatari kwa afya haina maana kwamba kila mtu atakayevuta sigara atakufa kwa cancer, jiongeze kama unataka kuelewa, ila kama uko kwenye ligi endelea kuuliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu.
Man siko na mentality za ushindani hapa.Mind you binafsi hoja yangu ilikuwa kwa mtoa mada and you showed up(meaning that you were ready for debate)

Sasa kama ulikosa hoja ya kulinda unachosema kuwa sahihi.Unahisi kwamba hapa tuko kwenye racing sio?Ulikuja mwenye sikuwa na interest ya kwenda mbali zaidi na debate kuhusu hili but uliendelea kuquote hoja zangu

Just to remind you,kama unakuwa huna namna ya kulinda hoja zako ni vema ukiona comment yangu upite kama hukuona and I'll do the same.
 
East africa uganda ndio wanaongea na kujua kingereza vizuri kuliko kenya unasemaje kuhusu wao.
Wanaweza kuwa wanajua Kingereza vizuri kuliko Kenya ila raia wanaozumgumza Kingereza Uganda ni wachache kuliko Kenya.
 
East africa uganda ndio wanaongea na kujua kingereza vizuri kuliko kenya unasemaje kuhusu wao.
Waganda wako juu kuliko sisi, angalia bunge lako lina wapinzani wangapi linganisha na walevi wetu huko Dodoma
 
Bro kama unajidharau jinsi ulivyo ipo siku utaolewa na hao unaowasifia. Kwa akili kama zako nchi isingepata uhuru
Kwa matusi ya nguoni ndio asili ya waswahili, zaidi ya hapo ni umbea na uchawi tu
 
Uko sahihi, ukimaster lugha ya kingereza unajiongezea utamaduni ni mpya wa kufikiri na kutenda
 
Nikusahihishe kidogo, Tanganyika haikuwahi kutawaliwa na Muingereza kama zilivyokuwa Uganda na Kenya
 
NIMEUNGA MKONO HOJA HII KWA KUSOMA HEADING TU KWA SABABU UMEANDIKA UKWELI MTUPU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…