Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Kaka huwezi kuacha mke na mtoto kwasababu ya baba yake, kwani anaekupa utamu ni mke au baba yake? Mpuuze huyo mzee maisha yako na mwanae yaendelee huku yeye akizidi kuzeeka akisubiri mahari
 
Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
Hutaki mtoto wako aolewe utamuoa wewe sasa, usione wivu ya mwanao ikiliwa kwasababu wewe umekula ya mtoto wa mtu pia
 
Pole sana, mi naona umsikilize mkeo tu, kwakuwa hana tatizo. Japo familia ya anakotoka mtu ina umuhimu sana katika ndoa, ila elewa ndoa kuna muda haziji kirahisi kunakuwaga na changamoto za hapa na pale.

Ila jiandae na jambo la mzee wake 🤣
 
Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
Siwezi kufurahi lkn angalau mwanaume kaenda kujionesha wengine huwa wanakula kona moja kwa moja. Wapunguze mahari mtoto wao aolewe jamaa akizira hasara kwa binti yao.
 
Bro Kuwa makini sana na waha Hawa jamaa nahisi shetani aliwabariki uchawi Kuna ndugu yangu walimgeuza Kuwa kichaa mpaka mda huu nao ongea na alikua mzima kabisa mtu mwenye Elimu yake
Kwaiy chukua mamuzi magum kunusuru maisha yako kuishi na Binti wa mtu bila wazaz wake kukubali hapo changamoto sana, ongea nao uone namna ya kukupunguzia tofaut na hapo piga chini tu
 
Nikuombe sana, mkeo usimwache. Hana hatia. Ishi nae, ila yeye ndo awaambie wazazi wake kuwa wewe huna hiyo 4m na kwamba utamwacha.

Lakini jitahidi utume japo 1m ukijaliwa uwezo.
 
Hapa ndo tunaona umuhimu wa kufahamiana familia tunapotokea kwanza. Braza ulishabugi tangia mwanzo. Njia za wazee wa zamani si za kupuuzwa. Unamuweka mwanamke ndani, mnalalana mpaka basi. Afu baadae ndo kwenda katika familia husika. Its very risky.

Hujui mwanaume/mwanamke unaetaka kuwa nae maisha yako yote ametokea katika familia gani. Kuna wanaume wanatokea katika very hard families ambazo wewe kama mwanamke hutaweza kuhimili. Vice versa pia. Sasa mnapokulana na kusogezana out of taratibu za kiAfrica ni rahisi sana baadae kuja kutokea mengine. Mila za zamani zisidharauliwe. Kuna pipo zitasema kama mila za zamani zinafuatwa zifuatwe jumla. Mambo ya bikra and stuff like that. Lakini ujue tu kama ni unataka bikra uwe tayari kutoa ng'ombe nyingi..maana ndo mila za zamani.

Anyways, braza pole kwa huu mkasa. Ngoma ishakua ngumu hii. What I know, kuna hakimu mkuu asiyepokea hongo wala rushwa. Anaweza kulitatua hili jambo chap. Go back to the cross. Ask God to make a way. Hii ni kama unampenda huyu mwanamke na unataka kufanya nae maisha. But if hauko tayari then endelea tu na mipango mingine. Yale magumu sana ndipo Mungu anajidhihirishaga ili kuonesha ukuu wake. Thats what I know. Ndo maisha lakini.
 
Yani we jamaa umekaa na mtoto wa watu, umemzalisha, umemtuma kwao ili uje kukamilisha taratibu za kuoa, wewe umemchukua ndugu yako mmoja eti mnaenda kujadili mahari, it doesn't make any sense, ni dharau na mazoea hayo. Kwani huko kwenu taratibu za kuoa zikoje? Au ndo ukishampiga mtoto wa mtu mimba ndo unatoka na rafiki yako kwenda kwa babamkwe kuuliza ni shangapi?
 
Mama hana shida. Hivyo ushauri wako usijumuishe wazazi wote.

Mama yupo pamoja na bintie.

Shida ipo kwa baba.

Sent from my SO-01J using JamiiForums mobile app
 
Kaka Mkubwa umeonesha hekima kubwa sana kwanza kujizua na kunyamaza hata wakati ambao ungestahili kuonesha reaction yako, na ukumbuke hata wazazi ni wanadamu wanakosea, so kwa hekima na busara hizo hizo unaweza kuishi na mke wako na kuchukuliana na ndugu zako hao, usimwadhibu mwanamke wako kwa makosa ya baba yake, maisha yenu yatakua maisha yenu basi. so ushauri wangu endeleeni na maisha yenu wazazi watagundua makosa yao na watajirudi na hata wasipojirudi wasamehe maisha yako yaendelee kwa amani.
 
Hutaki mtoto wako aolewe utamuoa wewe sasa, usione wivu ya mwanao ikiliwa kwasababu wewe umekula ya mtoto wa mtu pia
Kila jamii inatamaduni zake, kama tamaduni zenu zina ruhusu Mtoto wakike azae nje ya ndoa au akipata mchumba waishi tu kiuni itakuwa sahihi, lakini kwa tamaduni zetu ukitaka kuoa lazima ufunge ndoa kisheria ya Dini , mira au Kiserikali, siyo mnakutana chuo au Dar mnaishi chumba kimoja mnazaa watoto hata familia ya mwanamke haikujui kwa utaratibu huu haikubaliki kimira wala kidini, unakuwa umeidharau familia ya upande wa mwanamke.
 
Peleka hiyo milioni 4 anayotaka baba mkwe.
Pesa inatafutwa lakini amani ya moyo haina bei.
Fikiria ukimuacha huyo mwanamke na kupata mke mwingine je huko utakapoenda kuoa unajua mahari watakuambia ni kiasi gani?

Nakubali milioni 4 ni pesa nyingi lakini pambana kaza kende upeleke pesa ya watu ndipo utakapokuwa na amani na mema mengi yatakuwa juu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…