Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha COVID penzi lilinoga zaidi kwani "working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa Kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalokuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswaaa mpaka dk ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume!
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea n'a maisha ya sogea tuishi!
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka!
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya, (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa Mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpnz wangu!
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nomeambatana na brother angu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi Kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "hivi dogo hukuona wanawake mikoa yooote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu.(tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za kiha ili mambo yasiwe magumu)
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi! (Hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe) nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh.laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa Kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba n'a mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu!mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani!
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k,
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema " Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, SITAKI MJADALA!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sanaaa, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri" tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani sh.500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote Nina hasira vibaya mnooo, ila najitahidi kuificha japo mpnz wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia!
Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu" tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpnz wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari, akagoma akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki Kijijini tena, nikamwambia hapana, unapswa kubaki mpaka tumalizane n'a mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu,machozi yanamtoka tuuu
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "kama mnaobdoka wote nendeni tu" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu) akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa Kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kiahingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira, akamuita mtoto wake, akamwambia "mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, n'a mimi mama naomba atusamehe tu)
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mnoo, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini, tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpnz wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba SITOKAA NIRUDI KIGOMA, WALA SITOKAA NIPELEKE HIYO MAHARI WALIYOSEMA, nasubiri mwanangu akue kue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena!
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyway!