OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
[emoji1787] mahari 6M dadeki kama mfuko hausomi unakimbia mazima.
Unajaribu kuwatetea lakini unafahamu kabisa, kuna watu wanazalishwa na wenye watoto hawatumi pesa za malezi wala kwenda kujitambulisha!Sasa mkuu ulitakiwa familia ya mwanamke ikujue kabla ya mimba au mtoto kuzaliwa, sasa wewe unaishi na mtoto wa mtu kabla ya kumpa ujauzito mpaka anajifungua upo kimya na mpaka anaenda kwao anakaa miezi mingi kazi yako ni kupiga simu na kumtumia pesa we unavyoona ulikuwa sahihi?, je mimba ingetoka mpaka leo ungekuwa unaishi naye bila kujulikana kwao, wewe ulienda kuweni kwaajili ya mtoto bila kuwepo na mtoto safari ya Kigoma hakuna .
Kabila gani hii?afu mahali milioni 4 huyo binti hatarudi kwao??? sema sishangai bro wangu alitajiwa mahali 6M akalia lia wakapunguza mpaka 4M[emoji23][emoji1787][emoji174][emoji174] mama angu ana hasira mpaka leo na hiyo pesa mwanae katajiwa[emoji119][emoji119]
Wewe ni mjinga, mtu kukuletea zawadi ni kudanganywa 🚮 au mtaonekana mnadhiki..?Mfano wewe mtoto wako azalishwe bila ndoa itafurahia ? Na aje kuishi na mwanaume bila kumjua na aje kwako kujitambulisha na vizawadi vya kuwadanganya kama watoto au familia yenye dhiki sana.
Ningekua mm hata 100 nisingetoa. Kwanza nilivoona amekasirika ningejifanya kukubaliana nae kwa kika kitu. Na kusema anisamehe fidia nitatoa pia. Yaan kumuaminisha kua Niko tayar kwa lolote atakalo. Baadae sasa tukishakuabaliana nawaambia leo nimekuja kuelewana mahari na gharama zote maana sikujua gharama na mahali. Waniruhusu nirudi siku nyingine kuvilipa.
Baada ya hapo nisingerudi. Huyo binti ningeondoka nae kufika mbele kidogo ningemtelekeza kwa mshenga na kuondoka milele. Nisingerudi kigoma kamwe. Na huyo mtoto wangemsomesha wao na kumtunza baadae akiamua kunitafuta atanitafuta.
Kwa tabia na hiyo, nakuhakikishia watoto wako watazalishwa na hutokaa uone sura za waliowazalisha, achilia mbali kuwapiga makofi...Wewe ndie mpuuzi tena huna hata chembe ya busara. Karma is real nawewe utapata watoto wa kike naombea sana suala hili likupate siku moja. Yaani umzalishe binti yangu halafu uje kujileta baada ya mwaka? Utachezea vitasa mpaka MOI wadhani umegongwa na Treni. Be Calm umeharibu wewe na ugomvi umeauanza wewe kwa mzee.
nafikiri mtu hadi kufikia mpango wa kuoa ac yako iwe na 17m kwenda juu.Kwa watu wenye vipato vya kueleweka sio issue sana ila tia maji 6M ni nyingi sana.
Sawa.nafikiri mtu hadi kufikia mpango wa kuoa ac yako iwe na 17m kwenda juu.
Kabila gani hii?
Mpenzi wako ndio kakuchoma bro, siku nyingine uwe na akili uwo mchongo ni wa binti na wazazi wake ila kwakuwa love is blind unawaparua wazazi badala ya binti.Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!
Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti akashika mimba!
Baada ya mimba kufikisha miezi minne bibie akaniambia ni bora aende kwao kwanza kwani kubaki tukiwa wawili hatuwezijua complications za mimba, nilikubaliana nae, nikajipiga kwa kadri ya uwezo wangu nikamkatia tiketi na vizawadi kidogo vya wazee akaenda kwao!
Akiwa kwao mawasiliano yetu yalikuwa vizuri kabisa mpaka akajifungua salama salmin, na mimi niliwajibika haswa mpaka dk. ya mwisho, hatimaye tukapata mtoto wa kiume.
Bibie baada ya mtoto kufikisha miezi 6 bila mimi kwenda kujitambulisha akatoa wazo la kurudi kwangu kwani alikuwa amechoka kuishi nyumbani kwao, nikamkaribisha tukaendelea na maisha ya sogea tuishi.
Mwaka jana December, ilitokea msiba kwao akalazimika kwenda msibani, nikamfanyia maandalizi vizuri kabisa, akaondoka.
Amekaa huko tangu December, mpaka juzi nilipoamua kufuata taratibu za kwenda kwao ili tusiendelee kuishi kimya kimya (tufanye kuwa official), nikajiandaa kwa mambo kadhaa kama nilivyokuwa nimeng'atwa sikio na mpenzi wangu.
Nimeanza safari kutoka Dar kwenda Kigoma (kwao), nikiwa nimeambatana na brother wangu wa damu, aisee kwao ni mbali, maana tulitembea siku 2 njiani, tulipofika mjini, safari ya kwenda kwao ikachukua masaa mengine 8, vumbi kali hatari, tulipofika Kijijini kwao tukaambiwa Burundi ni mwendo wa kutembea nusu saa tu.
Brother akaniuliza, "Hivi dogo hukuona wanawake mikoa yote tuliyopita mpaka kuja huku?" Nikamwambia mapenzi yana nguvu bro, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningesafiri umbali namna hii kufuata mwanamke tu. Tulipofika mjini tulitafuta mzee mwenyeji, anayejua mila na desturi za Kiha ili mambo yasiwe magumu.
Basi bwana, tumefika pale tumepokelewa vizuri wakaandaa utaratibu wa mjadala, mshenga akatambulisha na kuanza mazungumzo rasmi, hapo nilikuwa na zawadi ya baba mkwe na mama mkwe, nilinunua tangu Dar kwa upendo kabisa.
Wakataja kiasi cha mahari kuwa wanataka mil. 4.5, hapo tukashtuka kweli, kabla hatujakaa sawa wakataja mkaja wa mama sh. laki saba, jumla wanataka 5.2 Milioni!
Yule mzee tuliyeenda naye akaomba twende nje kwa mazungumzo, akatuuliza kama tulipewa mwongozo na tuliyekwenda kumuoa, nikamjibu ndiyo (alisema mahari kwao haizidi Milioni moja) na mkaja wa mama huwa ina-range kuanzia 100k - 200k, na mimi niliandaa 200k kama mkaja wa mama! Mzee akasema hapa kuna tatizo, huku haijawahi kutokea mahari kubwa kiasi hiki, akasema tutasimamia kwenye hiyo 1M na mkaja wa mama 200k, tukarudi ndani!
Mzee (mshenga) akaanza kuzungumza, kuwa sisi tuna mahari 800k na mkaja wa mama 100k, lakini pia tuna zawadi kwa ajili ya baba na mama, ambazo si sehemu ya mahari, ni zawadi tu ya kijana wetu kwenu, mzee akatoa zile zawadi akaweka mezani.
Mshenga wao akashukuru na kuanza kuzungumzia mahari yetu kuwa angalau tufanye mahari mil.4 mkaja wa mama 500k.
Kabla hajamaliza akasimama baba mkwe, akionyesha kukasirika akasema "Sitaki mjadala wa kitoto hapa, mimi ndiye baba wa x, mkaja wa mama laki 5, mahari yangu nataka Milioni 4, Sitaki mjadala wala kusikia kupunguziana, kwanza unabeba zawadi kutuletea nani amekutuma utununulie, tumekuomba sisi utuletee zawadi zako?"
"Kwanza huyu kijana anadharau sana, tangu mtoto azaliwe hajawahi kufika hapa nyumbani, anaishia kumtumia mwenzake pesa tu, sisi hajawahi kututumia pesa hata mara moja, tumepata msiba hajawahi kuja kutupa pole zaidi ya kupiga visimu vyake tu, sasa mimi nimeshasema mkaja wa mama laki tano, mahari Milioni 4, sitaki mjadala!"
Aisee nilijikuta nimejaa hasira mpaka basi, mshenga wetu akatutaka twende nje, akasema "huyu mzee inaonekana ana lake jambo, tusiingie kwenye mtego wake, iweni wapole, tuondoke salama, watu wa huku ni hatari sana, tukiwa na hasira tunaweza tusirudi salama, hii si dalili nzuri."
Tukajadili tuvyojiandaa pale, mzee akasema muhimu tuanze na mkaja wa mama, tuwawekee hiyo 500k then tutawapa faini za mbuzi mbuzi, na vingine vidogo vidogo, baada ya hapo mahari tuwaambie kuwa tunaenda kuitafuta then mtaangalia wenyewe baada ya kufika nyumbani!
Tuliporudi ndani tukakuta mzee anaonyesha kuwa na hasira hasira tu, kiasi kwamba mshenga wao akawa ameduwaa tu, basi mshenga wetu akaanza kujitetea pale, akaweka mezani sh. 500k mkaja wa mama, akawaambia mbuzi watatu wa uchafuzi 300k sijui koti la mjomba, mara blanketi ya wazee na vikolo kolo vingine kwa Kadri ya taratibu zao, ile pesa tuliyoenda nayo ikawa imekata!
Muda huo wote Nina hasira vibaya mnooo, ila najitahidi kuificha japo mpnz wangu aligundua kabisa kuwa nimechukia!
Tukawaambia hiyo mil. 4 tunaenda kuitafuta, mzee akasema "mkaitafute muilete hapa, au mutanitumia kwenye simu" tukawaambia sawa.
Muda wa kutoka nikakuta mpnz wangu ameshabeba mabegi anataka tuondoke wote, nikamwambia hapana unapswa kubaki nitakuja kuwachukua nikimalizia mahari, akagoma akawa analia wakati wote akiwa amenikumbatia, anaomba radhi kwa kilichotokea ila anaomba tuondoke wote, yeye hawezi kubaki Kijijini tena, nikamwambia hapana, unapswa kubaki mpaka tumalizane n'a mzee, akagoma kata kata, akawa amepiga magoti huku amekumbatia miguu yangu,machozi yanamtoka tuuu
Mzee wake alipotoka akaona mwanaye analia akasema "kama mnaobdoka wote nendeni tu" Mara mama mkwe akaja na dogo (mtoto wangu) akamshusha nilipokuwa, nikambeba mtoto nikamwambia mama mtoto asimame, bro na mshenga wetu wakaniita pembeni, mshenga akasema tuondoke nao, tukimuacha na wakahisi kuwa Kuna dalili za sisi kutorudi, watamuua huyu mtoto.
Basi kiahingo upande, tukawakubalia kuondoka nao, mama mkwe akaleta maharage na jogoo akataka tuondoke navyo, nikakataa kuchukua, nikamwambia tutabeba wakati mwingine, akagundua bado nina hasira, akamuita mtoto wake, akamwambia "mwambie mumeo amsamehe bure baba yako, amekosea sana, n'a mimi mama naomba atusamehe tu)
Tukaondoka zetu, kichwani nikiwa nimejaa mawazo mengi mnoo, kiasi kwamba sikuweza kujua niamue nini, tumefika Dar lakini moyoni nimejikuta sina tena interest ya kutengeneza undugu na familia ya mpnz wangu, japo yeye binafsi hana shida, lakini kwa namna tulivyopokelewa na tulivyoondoka, nilijisemea moyoni kwamba SITOKAA NIRUDI KIGOMA, WALA SITOKAA NIPELEKE HIYO MAHARI WALIYOSEMA, nasubiri mwanangu akue kue kidogo nimwambie mama mtoto kwamba hakuna namna naweza kuunganisha undugu na familia yake, japo namhurumia ila ndiyo hivyo tena!
Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyway!
Mkuu kila jamii inatamaduni zake jaribu kujua hilo,mfano huyo binti uliye mzalisha angekuwa Mzanzibari leo hii ungeleta habari mbaya, yan ingekuwa umeenda Zanzibar cha kwanza ungewekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ya kutorosha na kuishi na binti wawatu kutoka chini ya uangalizi wa wazazi na kesi ya kubaka na kumpa binti ujauzito kwa Zanzibar yake kukuta hayo.Unajaribu kuwatetea lakini unafahamu kabisa, kuna watu wanazalishwa na wenye watoto hawatumi pesa za malezi wala kwenda kujitambulisha!
Sisi kwa kujua kwamba hatujui mila na desturi zao, tuliomba mzee mwenyeji atuongoze, na tulipata pre information kwa mahari zao huwa hazizidi Milioni moja, tunajiandaa hivyo, na tulienda kwa nia njema!
That is why, mshenga wetu (ambaye ni mwenyeji wa huko) alishangaa kuona aina ile ya reaction, na mahari iliyotajwa, akasema wana lao jambo, na akasisitiza tuwe wapole ili tusimpe nafasi!
As long as tumeshatoka huko salama, basi ntalazimika kuamua tu, kama kurogwa basi nirogwe tu!
Ama binti akaongee na wazazi wake, kuwa wewe HUNA HELAKwa hiyo kwa mtazamo wako sisi kutoka Dar mpaka Kigoma kwenda kuyajenga tulikuwa wapumbavu?
Ilikuwa busara kuona dhamira yetu na kuwa muungwana, ila kwa réaction aliyoonyesha atabaki n'a mtoto wake tu, siwezi kuwa n'a baba mkwe wa aina yake
huko usukumani watu wanatoa hadi ng'ombe 20+
Tafuta hela mkuu, Kigoma wala siyo mbali. Ni mwendo wa around saa mbili tu.Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!