Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Nimetoka ukweni Kigoma, ila kama hii ndiyo aina ya wazee acha wabaki na watoto wao!

Sio kila kitu Ni Cha kufuata kisa ni Cha zamani Kuna sababu gani ya kuozesha mwanao Kama unamuuza ,kwani lazima baba uwe mafia?tuache vingine vipite na wakati kikubwa tuwaombee watoto waishi kwa amani milioni 4 mahari ya mtu mmoja sio fair
Kumbe hujui hata maana ya mahari bure kabisa mahari ni shukrani kwa wazazi kwa kumtunza mwanamke ambaye ni mke wako
 
Nachojua umeambiwa utoe million 4 mahari ukaandaa uzi wa malalamiko nawakati hio ni case ya kawaida kwenye maisha hakuna jambo rahisi
Upuuzi mtupu, kama ulishindwa kukomaa ukiwa na nguvu basi komaa tu na uzee wenye stress, lakini sio stress zako unazimalizia kwa vijana wanaokuja kuoa kwako
 
Kumbe hujui hata maana ya mahari bure kabisa mahari ni shukrani kwa wazazi kwa kumtunza mwanamke ambaye ni mke wako
Wewe ndo hujui kitu sasa, hizo shukrani za kutunza zilikuwa mahususi wakati ambao mabinyi walikuwa wabakutwa wangali bikra, sasa unakuta mzee amefeli kwenye kulinda bikra za watoto wake halafu anataka kulazimisha mambo ya enzi za ubikra, inakaaje hiii???
 
Pole sana, makosa yapo pande mbili, kwako na kwa familia ya Binti. Makosa yalishafanyika kwako kuishi na binti wa watu bila kufuata utaratibu, hilo lilishapita. Mzee wa Binti ameshindwa kuling'amua Hilo, amesimamia kwenye misimamo ambayo itamfanya akose vyote. Inaonyesha Mzee Hana mtu anayeweza kumshauri, kama yupo basi hapo kwenye kikao hakuwepo.

Ushauri wangu, usije ukamwacha huyo mke wako kwa sababu ya mzazi wake mmoja. Inaonyesha wazi mama wa mke wako amechukia hicho kitendo, unaweza kujenga ukaribu naye akakusaidia baadhi ya mambo namna ya kuliweka jambo lako vizuri.

Tafuta kiasi cha mahari kile ulicho na uwezo nacho, wape wazazi wake. Endelea kuishi na mke wako na fuata taratibu za Sheria upate cheti cha ndoa.
 
Wewe ndo hujui kitu sasa, hizo shukrani za kutunza zilikuwa mahususi wakati ambao mabinyi walikuwa wabakutwa wangali bikra, sasa unakuta mzee amefeli kwenye kulinda bikra za watoto wake halafu anataka kulazimisha mambo ya enzi za ubikra, inakaaje hiii???
Mwache mwanamke wa watu kama unamuogopa baba mkwe au kama una ona million 4 ni nyingi sio unakuja kulalami lalamika mambo magumu ni kwa ajili ya wanaume na sio wavulana
 
Upuuzi mtupu, kama ulishindwa kukomaa ukiwa na nguvu basi komaa tu na uzee wenye stress, lakini sio stress zako unazimalizia kwa vijana wanaokuja kuoa kwako
Mambo magumu ni kwa ajili ya wanaume na sio wavulana
Seriou unataka usikie maneno kama unaonewa, mara baba mkwe kakosea, mara achana nae maisha ni mapambano

Mwanaume ambaye sio mwoga wa maisha hilo ni jambo kama mwanamke hana shida, mama yake hana shida ni baba yake tu imetokea kutokuelewana alafu unaamua kuzira kuishi na mwanamke ambaye hana shida yeyote
Sasa ukiwa baba wa familia unaweza ipigania familia yako siku ukikutana na changamoto utaizira familia yako au kuisusa

Mwanaume akimbii changamoto anazikabili kwa ujasiri
 
Mwache mwanamke wa watu kama unamuogopa baba mkwe au kama una ona million 4 ni nyingi sio unakuja kulalami lalamika mambo magumu ni kwa ajili ya wanaume na sio wavulana
Huo uanaume wa kuumizana na kufurahisha wakwe ni wa kipumbavu!

Uanaume wa kutafuta pesa kwa ajili ya familia yangu (mke na watoto wangu) ni sawa kabisa!
 
Situation ya mzee ingekuwa mbaya kama mtoto wake angekuwa alitelekezwa, lakini nimekuwa na yeye bega kwa bega, tangu ujauzito mpaka leo!

Tumechelewa kwenda kujitambulisha na kulipa mahari, (hilo nakubali ni kosa) lakini je, ni kosa linalofanya aamue kunikomoa n'a kunidhalilisha ?

Naamini baada ya watu kuoana undugu na mashirikiano huendelea, husaidiana katika huzuni na furaha, sasa ukinihuzunisha na kunisimanga kwa sababu una "hasira" kwa vitu ambavyo havina maana kabisa nitakuchukuliaje? Utegemee kuwa tutashirikiana kweli?

Lakini kilichonishangaza zaidi ni kwamba mama mtoto wangu ananiambia, dada yake alitoroshwa na jamaa wa huko huko kwao, na aliishi na mumewe kwa muda mrefuu mpaka akazlishwa watoto 2 then alipoenda "kujisalimisha" alipangiwa mahari ya sh.laki sita tu, na jamaa alilipa laki 4 na wanaishi huko Nyakanazi!

Dada yao mwingine, aliolewa na mtu wa karibu na Kijijini kwao, (huyo alikataa kwenda shule kwa ajili ya jamaa, yaani aliishia form 3) jamaa aliishia kulipishwa faini ya mbuzi 2 na mahari ya laki 6 pia!

Mama mtoto anajiuliza pia kwamba kwanini sisi anatuwekea uzibe na kuonyesha chuki ya wazi kiasi cha kutudhalilisha? Ananiambia hayupo tayari kuachana na mimi hata kama baba akimkataa (na hili naliona kabisa namna anavyokuwa upande wangu) lakini akili inaniambia, inawezekanaje kutengeneza undugu wa aina hii?

Nafika mahali naanza kuhisi pengine mzee ana chuki na watu wasio wa kabila lake tu?
Kwa upande wangu bado naona nafasi ya kurekebisha unayo!!

Binti anasema nini kuhusu wewe akiwa kwao?? Labda anakunadi wewe ni tajiri.

Tafuta wazee wa huko uwaelezee scenario wakusaidie kuongea nae.
 
Mambo magumu ni kwa ajili ya wanaume na sio wavulana
Seriou unataka usikie maneno kama unaonewa, mara baba mkwe kakosea, mara achana nae maisha ni mapambano

Mwanaume ambaye sio mwoga wa maisha hilo ni jambo kama mwanamke hana shida, mama yake hana shida ni baba yake tu imetokea kutokuelewana alafu unaamua kuzira kuishi na mwanamke ambaye hana shida yeyote
Sasa ukiwa baba wa familia unaweza ipigania familia yako siku ukikutana na changamoto utaizira familia yako au kuisusa

Mwanaume akimbii changamoto anazikabili kwa ujasiri
Nimemshangaa sana jamaa kutaka kumkimbia mwanamke ambae anaonekana ni jasiri na mwenye kutumia akili na sio hisia kama jamaa.
 
Huo uanaume wa kuumizana na kufurahisha wakwe ni wa kipumbavu!

Uanaume wa kutafuta pesa kwa ajili ya familia yangu (mke na watoto wangu) ni sawa kabisa!
Swala sio kuumizana ndo maana unatakiwa ndoa ni kwa ajili ya watu ambao wako tayari kupambana

Nikusaidie watu wengi hayo mamahari yenye fugure kubwa wanalipaga tu sehemu wengi hawalipi yote kwenye maisha jifunze kutumia akili na sio hisia wewe ni wa kiume na acha tabia ya kuzirazira kila unapokutana na changamoto
 
Nimemshangaa sana jamaa kutaka kumkimbia mwanamke ambae anaonekana ni jasiri na mwenye kutumia akili na sio hisia kama jamaa.
Tukubali tunakizazi cha wanaume waoga sana ambao kila wakikutana na changamoto kidogo wanakimbilia kuzira au kususa
Somo la ujasiri ikiwezekana inabid ifundishwe huko mashuleni mtu anataka kufanya jambo pasipokuwa na changamoto yeyote ile ikitokea tu anasusa aiseeee
Yaan naisha sio marahisi hivyo
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Kigoma tangu 2020, tulikutana chuo, na penzi likakolea haswaa!

Kipindi cha Covid penzi lilinoga zaidi kwani "Working from home" ilifanya muda wote tuwe pamoja, ilikuwa mwendo wa kwenda sokoni kununua mazaga zaga pamoja, tinaweka ndani then kila baada ya mlo ni mnyanduano tu, hatimaye binti

Kweli tembea uone, all the way from Dar to Kigoma, naenda kukutana na aibu tu, anyways.
Hamna jambo lisilo na suluhu. Itafte uoe huyo mwanamke. Naamini ni bora sana kwako kuliko kuja kuanza moja hawa wala shisha. Utakuja kujutia kumwacha huk mbele,itunze hii msg.
 
Tukubali tunakizazi cha wanaume waoga sana ambao kila wakikutana na changamoto kidogo wanakimbilia kuzira au kususa
Somo la ujasiri ikiwezekana inabid ifundishwe huko mashuleni mtu anataka kufanya jambo pasipokuwa na changamoto yeyote ile ikitokea tu anasusa aiseeee
Nipambane na changamoto za kuandaa maisha ya watoto wangu, then bado nipambane na changamoto za wazee wenye shari shari kama huyu, hapana!

Kwangu nadhani kuanzisha familia ni jambo la kheri, halipaswi kufanywa kama kutafuta kazi, kwamba unafanya interview na michujo ! Haifaiiii
 
Yaani nifunge safari kutoka Dar niende nikafanye uhuni Kigoma, inaingia akilini kweli?

N'a kama huo ndo mtazamo wao, hakika wananikosea sana, sio lazima nioe kigoma, nilienda kwa nia njema kabisa ila kama wametafsiri kuwa ni uhuni, basi nitawaacha wapate mstaarabu kwa tafsiri yao!
Mkuu kataa kabisa unyonge wa kipumbavu. Na usijaribu kabisa kutoa million 4 kuhamisha mtu kuja kwako. Bora uwekeze milioni tatu halafu hiyo moja utafute pisi nyingine uoe. Kama huyo mzee anaendeleza itikadi za kipumbavu basi mwambie amuoe yeye huyo binti yake. Kutishiwa kurogwa sio rahisi, ni ngumu sababu wataloga baba wa mjukuu wao. Do you think what next mtoto anakua halafu aambiwe baba alirogwa na babu? Kama huyo mzee hatabadilika basi atamnyima haki mtoto wake wa kike ambae kiuhalisia anakupenda sana tu.
 
Nipambane na changamoto za kuandaa maisha ya watoto wangu, then bado nipambane na changamoto za wazee wenye shari shari kama huyu, hapana!

Kwangu nadhani kuanzisha familia ni jambo la kheri, halipaswi kufanywa kama kutafuta kazi, kwamba unafanya interview na michujo ! Haifaiiii
Kama changamoto ya mtu mmoja inakushinda ndo za maisha na purukushani za watoto utaziweza kweli
 
Iliwahi nikuta scenario kama hiyo hiyo mwaka 2018 ,japo nashukuru Mungu nipo na binti yao mpaka leo

Mzee ujinga aliacha siku hizi aliniheshimu
 
Kama changamoto ya mtu mmoja inakushinda ndo za maisha na purukushani za watoto utaziweza kweli
Hii sio changamoto ni upumbavu tu, yaani kama mtu anaweza kuona mimi n'a ndugu yangu kusafiri zaidi ya kilomita 1200 kutafuta undugu wenye nia njema kabisa kuwa ni upuuzi na kuamua kucheza na akili yangu kwa makusudi, halafu nijibembelezeshe kwa kuitazama kama changamoto, kwa kweli HAPANA!

Nampenda binti yao, nilifanya wajibu wangu kwa kadri ya uwezo wangu,mzee ameidharau dhamira yangu, basi nitamuacha mtoto wake, sio kwa sababu simpendi, ila kwa sababu sitaki kutengeneza familia yenye misingi ya ugomvi na udhalilishaji!
 
Back
Top Bottom