Nimetongozwa na kavulana kauza bucha la nyama

Nimetongozwa na kavulana kauza bucha la nyama

Kirumba sokoni au Nela? hebu njoo tuonane sisi watu wazima kwanza,achana na watoto NAKWEDE,

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
hahahahahah, mi noti ya wapi? nimenunua nyama ya Tshs.24,000/= tu
Yaani kilo tatu steak
Ndo mana ulimdatisha Dogo wew,, kazoea kukata nyama robo robo... 3kg mbona akaona kashafika.. ila usimkatishe tamaa.
 
Kirumba sokoni au Nela? hebu njoo tuonane sisi watu wazima kwanza,achana na watoto

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Kirumba sokoni bucha namba 28 kwa Mwarabu hapo
 
Enyi watoto wadogo, wakiume, wavulana nani amewaloga?

Mmekuwaje mbona hamna hofu ya kuogopa wakinamama wakubwa waliowazidi umri mara 20000?

Mnapata wapi ujasiri huo?

story iko vile:
Jana nilipita kwenye bucha la nyama ambako huwa ninapenda kununulia hapo kwa kuwa wana nyama ya kutoka wilaya ya Ukerewe. Kwa ufupi nyama inayotokana na ng'ombe wa Ukerewe ni nzuri kwa kuwa ng'ombe wa Ukerewe wanalishwa tu maeneo jirani na nyumbani, hawajachoka na pia nyama ya Ukerewe ina ladha nzuri na ni laini. (sio tangazo za biashara mjue)

Baada ya kununua nyama, wakati nafungua mkoba kutoa hela, hako kavula kakawa kananiangalia sana, na mie nikakazia macho. Kakawa kanaonesha ishara ya kuomba namba za simu (yaani kakawa kanaweka mkono wake kwenye sikio kama vile kanapokea simu). Nilikaelewa nikakausha tu. Nikamlipa mwarabu hela yake.

Nilivyotoka hapo kuelekea kwenye usafiri, ghafla nikaona dogo yuko nyuma yangu. Mazungumzo yakaanza:

Dogo: Mama shikamoo.

Mie: Marahaba.

Dodo: huku akiwa anatoa tabasamu kama la panya, samahani mama naweza kupata namba yako ya simu.

Mie: Kwa ajili ya matumizi yepi?

Dogo: Ili niwe nakupigia kukupa taarifa za nyama inapoingia toka Ukerewe.

Mie: Mbona ratiba naijua tu, kwani ni lini niliikuja hapo nikakosa nyama?

Dogo: hahahaha, basi tuyaache hayo ya nyama, nataka tu nipate namba zako tuwe tunachat, kwa ufupi nimependa uwe mtu wangu!

Mie: Mxeeeewuu (nikaondoka zangu nikakaacha kamesimama hapo)
Dogo anataka Kusoma Katiba hivi hivi.
 
Hahahaha!! Pole sana.
Dogo baada ya kuona pochi imetuna akahisi kiu ghafla, ungemtupia mwekundu tu akanywe maji aache usumbufu.
 
Back
Top Bottom