Bundakwetu
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 551
- 1,014
Habari zenu wakuu, leo nimerudi kutoka mishe mishe zangu za ufundi, ile nafika nyumbani baada ya watoto wangu kunipokea na kusalimiana nao mwanangu akaniambia baba Mwalim Joyce amesema ukifika umpigie anashida na wewe nikamjibu sawa.
Ikumbukwe mimi ninaishi na mabinti zangu wawili baada ya kushindwana na mama yao na mimi kuamua kumuachia mji na kuanza upya, sasa niliona baada ya kufanikiwa kuwahamisha shule toka kule Mwanza hadi hapa Morogoro na hawa ni watoto wa kike na niwadogo bado mkubwa ana miaka 11 na mdogo miaka 8 basi hapa shuleni wanaposoma kwa sasa nikaona ni bora niwakabidhishe kwa mwalim ambae anafundisha shule hiyo wanaposomea watoto wangu, na huwa anakuja hapa nyumbani kwa ajili ya kuwafundisha masomo ya ziada (Tution) na nilishamsimulia mkasa wangu na mke tuliyeachana na akanipa pole nyingi sana,
Nirudi kwenye mada sasa baada ya kumpigia kuwa nimeambiwa na watoto kuwa nikifika nimpigie nikafanya hivyo na Madam kaja kwakweli amefunguka mwanzo mwisho kuwa ananipenda na yupo tayar kuanzisha mahusiano na ikibidi tuoane kabisa, yeye ni mwenyeji wa Lindi na ni muajiriwa wa serikali Mwalimu na hajazaa na hana mume wala mchumba, kiukweli sijampa jibu nimemwambia ngoja nitafakar kwakuwa sina hamu tena ya kuoa kwa sasa, na amesisitiza kuwa hawa watoto wangu wanahitaji malezi ya mama ambae ni yeye kiukweli nipo njia panda sijampa jibu la ndio au hapana, ila kiujumla yeye na watoto wangu wako vizur sana sijajua nimkubalie au vipi na Madam ananiambia ananitegemea nitampa jibu zuri nipo njia panda sijajua nimjibu nini Madam.