Nimetosheka na maisha ya ujana wa ki-bachelor (natangaza nia: jimbo lipo wazi)!

Nimetosheka na maisha ya ujana wa ki-bachelor (natangaza nia: jimbo lipo wazi)!

MOSintel Inc

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2016
Posts
817
Reaction score
593
Habari za wakati huu wana-jukwaa,

Nina imani mmekuwa na siku njema na mwaka mwema tunapoelekea kuumaliza mwaka 2021. Tuna kila sababu ya kumshukuru MUNGU kwa Neema hii ya Uhai aliyoendelea kutubariki; Jina lake lihimidiwe.

Niwashukuru sana ndugu, jamaa na marafiki hapa jukwaani ambao tumekuwa tukishauriana mambo mengi katika nyanja mbalimbali. Kuna ambao walikuwa na changamoto kubwa, lakini kupitia jukwaa hili wakapata majawabu ya shida wanazopitia. MUNGU awabariki mno wale wote mliotoa msaada wenu kwa wale wenye uhitaji.

Ndugu yenu nimekuwa hapa jukwaani na mara kadhaa nimefarijika kwa testimonies za watu mbalimbali kuhusiana na mapenzi, mahusiano na urafiki, na kujifunza kupitia changamoto kadhaa zinazohusisha masuala ya ndoa. Kusema ukweli ndani ya Moyo na fahamu za medula yangu najiona nimeiva na nipo tayari nami kuingia katika ulimwengu mwingine ambao, imekuwa ni shauku, kwa kila kijana ambaye ana utayari wa kuanzisha familia.

Najua kuna mambo mengi sana ambayo sijayasikia na mengine nimeyasikia hapa kuhusu NDOA, na hata wakati mwingine kuuliza kwa undani kwa watu ambao tayari wapo katika taasisi hii NYETI iliyopelekea wengi wetu kuja hapa duniani. Nimesikia, Nimeelewa, Nikaeleweshwa zaidi na nikafanya utafiti wa kina juu ya taasisi hii ya NDOA.

Leo tarehe 08.12.2021 masaa machache kabla ya Taifa letu kutimiza miaka 60 ya Uhuru, natangaza rasmi NIA yangu ya kuanzisha FAMILIA, namaanisha natangaza rasmi mchakato wa:

1. Kumpata binti (wa kuendana naye)

2. Kuingia naye katika mahusiano

3. Kuingia naye katika uchumba

4. Kuingia naye katika NDOA(kuanzisha FAMILIA)

Eeh, MWENYEZI MUNGU, nisaidie.


Hold-on!:
Ninaposema "kumpata": namaanisha kuwa ninao MARAFIKI WA KIKE hapa jukwaani na nje ya jukwaa, lakini sijafanya utafiti wa kina kujua hasa ni nani kati ya hao ataendana na Mimi katika familia iliyopo katika maono yangu.

Kwa wale MABINTI waliokuwa wakiniuliza kila mara 'naoa lini', niwape habari njema kuwa nimefungua rasmi dirisha langu la uchambuzi na uchaguzi!...nawasisitizia kwamba: "JIMBO LIPO WAZI".[emoji4]

Ni imani yangu kuwa nimeeleweka vyema. Jambo kubwa ninalo waomba ndugu zangu; Nahitaji MAOMBI, SALA na DUA zenu kwa MWENYEZI MUNGU ili aweze kunipatia Binti mwema, msikivu, mcha-MUNGU, Msaidizi, Mpenda maendeleo, Mvumilivu na Mwaminifu. Kwa kifupi, yule wa kuendana/kufanana naye.

Natanguliza shukrani.
Mbarikiwe mno. Ahsanteni sana.

images%20(7).jpg

 
Habari za wakati huu wana-jukwaa,
Nina imani mmekuwa na siku njema na mwaka mwema tunapoelekea kuumaliza mwaka 2021. Tuna kila sababu ya kumshukuru MUNGU kwa Neema hii ya Uhai aliyoendelea kutubariki; Jina lake lihimidiwe.
Unapaswa Utafute Mchumba na Uoe sio tena Uanze Kuzini Kama ambavyo Umekuwa Ukifanya hapo kabla

Unapotaka kuoa inatakiwa uwe Humjui mwanamke huyo Kimwili sip Ushalala nae Kama mara 100 hivi ndo Unakuja Kuoa hiyo inaua ile ari ma Morari ya Ndoa Ndo maana Vijana wengi hawaoi siku hizi

Wewe Tafuta Mchumba ukiridhika nae muoe kabisa Huna sababu ya Kuanza Kumfunuafunua

Hapo kwenye kutafuta mchumba ukiweza shirikisha wakubwa zako huku Ukumuomba Mungu akupe aliye mwema ila Usinzini kwanza

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom