Mkuu,
Kutukana au kutumia lugha ya matusi inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani ni kosa la jinai kufuatana na Penal Code Act, Cap. 16 ya Sheria za Tanzania.
Kifungu cha 89 kinasema ifuatavyo:
Section 89.
(1) Any person who
(a) uses obscene, abusive or insulting language to any other person in such a manner as is likely to cause a breach of the peace; or
(b) brawls or, in any other manner, creates a disturbance in such a manner as is likely to cause a breach of the peace,
is guilty of an offence and liable to imprisonment for six months.
Nenda polisi na ujumbe huo na watawasiliana na kampuni ya simu husika na kupata ushahidi stahiki. Kama uko DSM nenda Central Police Station wamefungua kituo maalum kwa makosa ya namna hiyo.
Pole sana kwa kero hiyo.