Nimetukaniwa Mzazi wangu kwa SMS, Naombeni Muongozo!

Nimetukaniwa Mzazi wangu kwa SMS, Naombeni Muongozo!

Na kule Bungeni wapo wenye mitusi na mipasho na wanafurahia saana hiyo tabia.Hebu tuwatambue kwa hizo sifa:Kombo wa ZNZ,Asha Bakari huyu mama anastahili kuingia kwenye world record ya mitusi.
 
jamaa hajataka kufunguka...nadhani angetuambia waliko anzia hadi akaanza kuporomoshewa matusi angepata ushauri mzuri sana....anyway kama vipi amshughurikie kichawi tu!

Ni kweli, huwezi ku-solve tatizo bila kujua chanzo.
 
Mkuu,

Kutukana au kutumia lugha ya matusi inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani ni kosa la jinai kufuatana na Penal Code Act, Cap. 16 ya Sheria za Tanzania.

Kifungu cha 89 kinasema ifuatavyo:

Section 89.
(1) Any person who–
(a) uses obscene, abusive or insulting language to any other person in such a manner as is likely to cause a breach of the peace; or
(b) brawls or, in any other manner, creates a disturbance in such a manner as is likely to cause a breach of the peace,
is guilty of an offence and liable to imprisonment for six months.

Nenda polisi na ujumbe huo na watawasiliana na kampuni ya simu husika na kupata ushahidi stahiki. Kama uko DSM nenda Central Police Station wamefungua kituo maalum kwa makosa ya namna hiyo.

Pole sana kwa kero hiyo.
 
Kuna siku mtu atanyimwa unyumba na mme wake au mkewe atakuja kushitaki hapa jukwaani
 
Chanzo nini mkuu...ameanza kutukana kama mwehu tu...pole ignore tu
 
Back
Top Bottom