Nimetumia hela vibaya, ndugu zangu wanateseka. Moyo unaniuma

Si bora ww elfu 90 tu!!!mimi weekend iliyopita jmosi mpaka jtatu nimepiga mahesabu nimetumia laki 3 kwenye mambo ya kipumbavu hasa pombe na kuacha nimeshindwa acha.
Hii kitu alcohol ilinimalizia pesa hatar.ila baada ya kupumzika three months now.najiona tajiri alafu mwepesi na jasho halivuji sana .Aya mapepo ni hatar aisee
 
pole sana kiongozi, maisha ni vita na hali uwa ngumu sana sababu unapigana na nafsi yako. usipokuwa na msimamo unaweza toka nyumbani ukarudi mshahara umeisha na haujanunua LUKU[emoji23]ndio pale unapoamini uchawi upo.

mimi kuna kipindi nilikaa na kufikiri nikaamini kabisa nilikosea kusomea fani niliyonayo. bora ningesoma ufundi labda ningejiajiri.

mshahara ni moja ya gharama ya uzalishaji, na mnene atapima mshahara wako ili yeye apate faida yake.
maisha haya tutafaidi kama mapato yetu yatabadilika kutoka ujira na kuwa faida.
 
Hii kitu alcohol ilinimalizia pesa hatar.ila baada ya kupumzika three months now.najiona tajiri alafu mwepesi na jasho halivuji sana .Aya mapepo ni hatar aisee
Hahah kuingia ni rahisi ila kutoka sasa ni shughuli.
 
Si bora ww elfu 90 tu!!!mimi weekend iliyopita jmosi mpaka jtatu nimepiga mahesabu nimetumia laki 3 kwenye mambo ya kipumbavu hasa pombe na kuacha nimeshindwa acha.
Pole sana. Jaribu kujizuia.
 
ndugu zangu kma nilivyosema ni wanfunzi na wengi ni wakike, mzee alishafariki mama anaishi kijijini kibingwa bingwa ivyo ivyo. ni mengi nikisema nileleze mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…