Nimetumia hela vibaya, ndugu zangu wanateseka. Moyo unaniuma

Nimetumia hela vibaya, ndugu zangu wanateseka. Moyo unaniuma

unawaza na kuwazua ghafla unashtuka kumbe usingizi ulikupitia, baada ya nusu saa inapigwa hodi wadeni wako.

hali ngumu ndio chanzo cha roho mbaya, watu wana hasira tayari hata kabla hujaleta shobo[emoji23]
 
hapana.
Nilikuwa nimejiwekea kwenye kibubu.
Nilizikusanya kama miezi miwili hivi.
Sasa kuna jumapili moja nilipigika mbaaya
Nikasema isiwe tabu kibubu changu kipo wapi,msumeno upo wapi.
Nikakikata.
Nilipata Laki 820.
Bwanaa wee.
Mpaka jioni yake nimebakiwa na Laki 6.
Kesho Yake jioni Nina Laki 4.
Ndani ya Siku nne kwishaaaa.
Duuuh noma kweli
 
Naandika haya atleast kupunguza majonzi nilionayo moyoni.

Mimi ni kijana kutoka familia masikini sana, nimebahatika kupata kazi, nitazungumzia mshahara wa october.
Baada ya kupokea 280,000 kama mshahara wangu, nililipa elfu 60 deni lililokopa katikati ya mwezi, kisha nikamtumia mama elfu 10, nikamtumia mdogo wangu hela ya shule elfu 15 na rafiki yangu anaeoa machango wa 15 elfu. Roughly nilibakiwa na kama 180,000. (laki na themanini).

Sasa sijui imekuaje (naomba nisiseme ilivyotumia) ndani ya usiku mmoja nikatumia shiling 90 elfu kwa starehe tu za ajabu. Imeniuma sana kutokana na hali ya maisha ya nyumbani, ndugu zangu wengine hata kula ni shida. Sasa nimebakiwa na 90 elfu ambayo inabidi inifikishe mwisho wa mwezi wa kumi na moja.

Ni hayo tu ndugu zangu, siwezi kumwambia mtu huku
Inaitwa ulimbukeni wa pesa, kazi unayo utapata mshahara mwingine, usirudie kosa.
 
having brother's Lookin after my mom ...helps a lot 😂😂😂 my salary i can finish it on One night alafu kesho napiga simu kaka fanya mafekecheee nakufaaa mie sina hta mia 😂😂😂
 
Sasa wewe unalinganisha Elimu ya mtu na pesa anazopata? U're not serious maisha yanabadilika within a second, njoo inbox nikutumie documents za bank
 
Invest isee usitegemee hako ka mshahara tena ukiweza kakope benki ufanyie mambo mengine yakukupa japo 20k kwa siku
 
Si bora ww elfu 90 tu!!!mimi weekend iliyopita jmosi mpaka jtatu nimepiga mahesabu nimetumia laki 3 kwenye mambo ya kipumbavu hasa pombe na kuacha nimeshindwa acha.
Hatutofautiani ndugu,Mimi nilibet October 19 nikamla mhindi Laki mbili na elfu 53 then tarehe 30 October nikala Tena Laki tatu na 39 Hakuna la maana nililofanya zaidi ya kukusanya marafki kuila pesa sijanuna hata shati. POMBE hazina maana kabsa. Nilikuwa na deni sehemu la elfu 26 sikuweza hata kuliliwa,na nilifanya Siri hata wife asijue kuwa nimeshinda bet
 
Kweli maisha magumu jamani tuache utani msione kama hiyo salary ya jamaa ni ndogo

Mi mwenyewe Jana usiku nimeacha kiporo changu mezani, leo asubuhi nimeamka kukicheki nakuta hakipo kumbe kala jeremiah
hahaha kala mashaka mkuu
 
Pole ila kimising anza kufikiria njia ya kuongeza kipato chako. Uwe na budget halisi kutokana na mapato yako. Kuteleza sio kuanguka songa mbele huwezi kubadilisha ya jana ila tumia leo kubadilisha kesho
 
Back
Top Bottom