Nimeua nyoka mkubwa Mikumi

Nimeua nyoka mkubwa Mikumi

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Nikitokea Morogoro kuelekea Iringa alfajiri ya leo mwanzoni mwa hifadhi ya mikumini nikakutana na joka kubwa limetulia barabarani, niliyekuwa naye akashauri tusiligonge akaanza kunipa Visa vya koboko aka black mamba kuwa unaweza kumkosa akajificha kwenye uvungu wa gari ukishuka anakugonga.

Nikaona sio kesi, nikashuka nikachukua jeki, nikamtandika mgongoni nadhani nilivunja kabisa uti wa mgongo akawa anarandaranda tu pale nikatafuta kipande cha fimbo nene nikamtandika kichwa shughuli ikaisha nikamtupa pembeni safari ikaendelea.

Nyoka yoyote anayekatisha mbele yangu huwa nampelekea moto bila kujali yuko eneo gani, nyoka ni nyoka tu hata kama ni wa royo tuwa.
 
Mnajisumbua kwa Bei elekezi ni fix tupu
Kwani kwenye kile kibao kilichowekwa kule mbugani hawajaweka bei atakayolipa mtu kwa kumuua nyoka?

Nilipita pale niliona listi ya wanyama wengi na tembo.

Ikiwa ni US dollar 15,000 ambayo ni sawa ni Tsh milioni 35 na ishirini na tano elfu.
 
Back
Top Bottom