Nimeua nyoka mkubwa Mikumi

Nimeua nyoka mkubwa Mikumi

Nikitokea Morogoro kuelekea Iringa alfajiri ya leo mwanzoni mwa hifadhi ya mikumini nikakutana na joka kubwa limetulia barabarani, niliyekuwa naye akashauri tusiligonge akaanza kunipa Visa vya koboko aka black mamba kuwa unaweza kumkosa akajificha kwenye uvungu wa gari ukishuka anakugonga.

Nikaona sio kesi, nikashuka nikachukua jeki, nikamtandika mgongoni nadhani nilivunja kabisa uti wa mgongo akawa anarandaranda tu pale nikatafuta kipande cha fimbo nene nikamtandika kichwa shughuli ikaisha nikamtupa pembeni safari ikaendelea.

Nyoka yoyote anayekatisha mbele yangu huwa nampelekea moto bila kujali yuko eneo gani, nyoka ni nyoka tu hata kama ni wa royo tuwa.
"Nyoka yoyote anayekatisha mbele yangu huwa nampelekea moto bila kujali yuko eneo gani, nyoka ni nyoka tu hata kama ni wa royo tuwa"

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
.
images%20(29).jpg
 
Sasa umemuwa wa Nini?

Infact wala sio sifa. Huyo nyoka umemfuata hifadhini, ndio kwake hapo ni wewe ndio hukutakiwa kuwa hapo sio yeye. Umemuonea Bure na Wala hujafanya ushupavu wowote!
Mkuu nakubaliana na wewe kuwa huyu jamaa amemuonea sana huyo nyoka maana yupo kwake ingelikuwa yupo milima ya Namanyoro ingekuwa sawa.

Huko Mlalo - Lushoto, vijiji vya Mng'aro, Mzinde, Kwamkole n.k Tembo si chini ya 10 wanakula mazao ya wakulima na kuharibu miundombinu yso hakuna hata ofisa yeyote wa Serikali anayejali.

Wakulima wavuna mahindi na mazao mengine kabla ya kulomaa. Hakuna tathimini inayofanyika kwa walio haribiwa mazao yao. Mabwana na mabibi shamba hawaonekani. INASIKITISHA.
 
Back
Top Bottom