NIMEULIZWA SWALI: Ungekuwa Mchungaji au Sheikh ungefungisha hii ndoa?

NIMEULIZWA SWALI: Ungekuwa Mchungaji au Sheikh ungefungisha hii ndoa?

Ndoa inafungishwa tu nani asiyezini.
Tatizo hiyo nguo aliyovaa ni ushamba na ujinga kuvaa hivyo hadhatani
nimekupa like kwa hapo "nani asiyezini"
Hata hivyo wakiwa wanafungishwa, bidada hakuwa amevaa hivyo. alivaa vyema.
 
Nikukumbushe tuu kitu. Yakobo wsa kwenye biblia anaetajwa kuwa baba wa taifa teule na aliyepokea mibaraka yoooote ile alikuwa ni mwizi, tapeli na laghai mkubwa kwa kushirikiana na hila za mama ake mzazi. Huyu bwana alimtapeli Ibrahim baba wa imani na Mungu mchana kweupee kwa uongo ambao yeye na mama yake waliupanga kwa Muda mresu sanaaa.

Alijifanya Essau ambaye ndiye aliyestahili kupata mibaraka kwa sababu ndio alikuwa mzaliwa wa kwanza, Kwahila za kushirikiana na mama yake waliiba kondoo wa wa Essau, wakamchinja, wakamchuna ngozi, wakatengeneza vazi la kuvaa mikononi ili kupitia kama mikono ya shati mikono mirefu ili yale manyoya ya kondoo wa essau wamzuge Ibrahimu kwamba huyu ni Essau, kwa kuwa Ibra alikuwa haoni na anajua Essau ana nywele walilifanya hili kusudi tena kwa akili kuuubwa ili kumwingiza king mzee baba. Na kweli akaingia cha kike japo alihoji mbona sauti ni kama yakobo lakini mikono ni kama essau. Mama mtu akamlazimisha mzee atoe baraka. Kwa kuwa mzee baba alimpenda sana mkewe akaamini utapeli huo

Mungu alivo waajabu sasa pamoja na utapeli huo wote ambao mimi nakadiri utakuwa ulipangwa kwa muda mrefu na kwa kutumia teknolojia kubwa lakini Mungu alimbariki yakobo, akamzidishia ukuu na utajiri mara maelfu kwa elfu na mpaka leo Mungu hajamwondolea mibaraka ile aliyomkirimu.

My take: Wakati wote unahitaji Roho wa Mungu kukuongoza nini cha kufanya au kutofanya na sio mihemko ya kibinadamu
 
Tunapoteza time kudiscuss ujinga ndoa ishafungwa na hao watu ni Mr and Mrs tuendelee na mambo yetu mengine
Nakupa mfano ndg computa, late presida JPM alishafariki why mpaka leo mnamjadili?.
 
Sehemu kama hizo watu wanapenda kuuza sura,rais wa yanga naona kavamia hapo
Sehemu hizo kila mtu anataka kuonekana,nasikia hata yule mwenye lambogini #A naye alitia nayo timu kwenye tukio hilo

Ova
 
Asee kawoli reply yako nzuri sana, kweli Yakobo alifanya ulaghai na jambo la kujiuliza je, Mungu hakujua ule ulaghai mpaka akaruhusu utokee?.

Jibu silitaki hapa, maana bado kuna swali, Je ungekuwa Mchungaji au Sheikh ungefungisha NDOA huku binti na mimba kubwa kama hiyo?.
 
Kuhusu ujauzito hakuna shida
Unatengeneza jamii ya aina gani kuanzia hapo, mfumo wa maisha ya kutiana mimba kisha mnaenda kufunga NDOA unaona ni sahihi kisa hakuna mkamilifu chini jua..?
 
Angalia picha ya bibi yako hakuna tofauti na nyani sasa watoto wa siku hizi wanatamanisha sana
Acha kabisa umesema bibi angu vipi dada yako akizeeka afadhari hata na bibi yangu maana rangi ya ngozi yake itakuwa kama kababuliwa na radi kwa mikorogo anayotumia sasa.
 
Unatengeneza jamii ya aina gani kuanzia hapo, mfumo wa maisha ya kutiana mimba kisha mnaenda kufunga NDOA unaona ni sahihi kisa hakuna mkamilifu chini jua..?
Watoto ni baraka, ukiishi kwa kutazama macho ya watu, ni vigumu kufanikiwa; kwa sababu hata ukiugua hawatakununulia panado.
 
nje ya Mada

alipopandishwa Jukwaani Wakala wa Tajiri 'Mhandisi' Hersi ndio Machawa wakajifyatua akili kweli kweli kwa kuanza kubebana na vurugu za hapa na pale ili wakala afurahi
 
Nilichokigundua una chuki
1.hivyo sivyo walivyokua katika ibada ya ndoa
2.kwanini hukuweka picha ambayo walivaa tofauti na hivyo(ambayo ilivaliwa kanisani)

Uzi wako haujakaa sawa
 
Kulikuwa na haja gani ya yeye kuliweka litumbo wazi ivyo
 
Shida kubwa ya Tanzania ni kuwa watu hatujifunzi kumind mambo yetu. Tunapenda sana kufuatilia ya wenzetu yani.
 
Back
Top Bottom