Nikukumbushe tuu kitu. Yakobo wsa kwenye biblia anaetajwa kuwa baba wa taifa teule na aliyepokea mibaraka yoooote ile alikuwa ni mwizi, tapeli na laghai mkubwa kwa kushirikiana na hila za mama ake mzazi. Huyu bwana alimtapeli Ibrahim baba wa imani na Mungu mchana kweupee kwa uongo ambao yeye na mama yake waliupanga kwa Muda mresu sanaaa.
Alijifanya Essau ambaye ndiye aliyestahili kupata mibaraka kwa sababu ndio alikuwa mzaliwa wa kwanza, Kwahila za kushirikiana na mama yake waliiba kondoo wa wa Essau, wakamchinja, wakamchuna ngozi, wakatengeneza vazi la kuvaa mikononi ili kupitia kama mikono ya shati mikono mirefu ili yale manyoya ya kondoo wa essau wamzuge Ibrahimu kwamba huyu ni Essau, kwa kuwa Ibra alikuwa haoni na anajua Essau ana nywele walilifanya hili kusudi tena kwa akili kuuubwa ili kumwingiza king mzee baba. Na kweli akaingia cha kike japo alihoji mbona sauti ni kama yakobo lakini mikono ni kama essau. Mama mtu akamlazimisha mzee atoe baraka. Kwa kuwa mzee baba alimpenda sana mkewe akaamini utapeli huo
Mungu alivo waajabu sasa pamoja na utapeli huo wote ambao mimi nakadiri utakuwa ulipangwa kwa muda mrefu na kwa kutumia teknolojia kubwa lakini Mungu alimbariki yakobo, akamzidishia ukuu na utajiri mara maelfu kwa elfu na mpaka leo Mungu hajamwondolea mibaraka ile aliyomkirimu.
My take: Wakati wote unahitaji Roho wa Mungu kukuongoza nini cha kufanya au kutofanya na sio mihemko ya kibinadamu