Nimeumia kisa mapenzi

Nimeumia kisa mapenzi

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
“Naanzaje kukataa Joshua? Nipo tayari uniowe hata kesho. Nikikumbuka jinsi tulivyokutana moyo wangu unajawa na furaha na amani sana. Nakupenda pia Joshua” Alisema Noela kisha alimkumbatia Desmond.

Sura ya Desmond ilibadili taswira kutoka kutabasamu hadi kuwa mtu aliye siriazi na jambo lililo akilini mwake.

Majukumu ya kazi yaliendelea kwa pande zote yaani kwa Desmond na kwa upande wa Noela, kumpata Desmond kulimpa furaha sana Noela akawa anachapa kazi zake.

Mchana wa siku hiyo, Desmond alienda Hospitalini kama kawaida, alipewa nafasi ya kumuona Mke wake Mandy. Alikuwa na hasira na Mwanamke huyo. Mandy alikuwa amepoteza fahamu kwa zaidi ya miezi mitano hivyo kwa kipindi chote alikuwa Hospitalini tu, Desmond alisogea akaketi kwenye kiti kimoja ambacho kilikuwa kando ya kitanda cha Mke wake, alikunja nne kisha akamwambia Mandy

“Nina uhakika unanisikia Mandy! Katika vitu sitamani kuona katika Maisha yangu basi ni uhai wako, natamani uwe umekufa na usiamke tena hapo Kitandani” Alisema Desmond akiwa amevalia suti nyeusi zilizomkaa vizuri, alikuwa kijana mwenye muonekano mzuri sana. Desmond alisimama kisha alimsogelea Mandy

“Siri unayoijuwa kuhusu Mama yako ibaki kuwa siri ya Ulimwengu mzima, sipo tayari kuyaharibu Maisha yangu kwasababu yako. Asante kwa utajiri mkubwa ulioniachia Mandy, nasikitika sababu uliyemuamini siku zote hakuwa na mapenzi na wewe, sikuwahi kukupenda Mandy….Nilizipenda pesa zako tu” Alisema Desmond kisha alivuta pumzi zake huku chozi likimlenga, licha ya uamuzi huo mgumu bado alionesha kuumia ndani ya Moyo wake

Ghafla aliona Mandy akitingisha kidole, hii ilimshtua sana Desmond, miezi yote Mandy hakuwahi kutingisha hata kope za macho yake, ilionesha wazi hata alichokizungumza Desmond alikuwa akikisikia. Akiwa anaendelea kushangaa Desmond aliona macho ya Mandy yakifunguka huku yakibubujikwa na mchozi, Mandy alikuwa ni Mwanamke mzuri mwenye weupe wa asili, chozi la Mandy lilionesha wazi kuwa lilibeba maumivu makali sana

“Mandy umeamka? Ina maana siri yangu utaisema!! Hapana Unakufa” Alisema Desmond ndani ya moyo wake huku akiwa amevurugwa sana, aliangalia huku na kule kisha alichukua mto na kumziba pumzi Mandy ili afe pale kitandani. Mandy alihangaika kwa nguvu chache aliyokuwa nayo lakini hakuweza kufanya lolote zaidi ya kuziona pumzi zake zikifika mwisho, Desmond alidhamiria kumuuwa Mandy mchana huo ili hiyo siri yake isijulikane.

Mara Desmond alisikia chupa ikivunjika, alipogeuka alimuona nesi Lucia akiwa anaokota vipande vya vyupa pale mlangoni. Haraka aliacha jaribio la kutaka kumuuwa Mke wake Mandy. Aliuweka mto pembeni, alikuwa akitokwa na jasho jingi kisha alimtazama Mandy alionekana kuzima, Desmond aligeuza macho alimuona nesi Lucia akisogea hapo

“ooh Desmond” Alisema Nesi Lucia huku akiwa anaweka vifaa juu ya meza iliyo pembe ya ukuta, alipomtazama vizuri Desmond alimuona akiwa anatokwa na jasho jingi sana, alishangaa kisha alipeleka macho yake kwenye AC, kisha alirudisha kwa Desmond. Alionekana kushangaa jasho la Desmond lilitoka wapi ikiwa chumba hicho kilikuwa hakina joto kabisa

“Kulikoni Desmond mbona unavuja jasho hivyo” Aliuliza Nesi Lucia akiwa anamtazama kwa makini Desmond

“Aaah- aaah…Jasho….unajuwa!! Lucia sijisikii vizuri naomba nipumzike nje” Alisema Desmond kisha alitoka lakini Nesi Lucia aliendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu, mwisho alipuuzia jambo hilo.

Alienda kumtazama Mandy, alionekana kupowa huku mapigo ya moyo yakienda sawa kwa maana Desmond hakufanikiwa jaribio la kuondoa uhai wa Mandy, alibadilisha dripu na kufanya mambo mengine kisha naye alitoka. Hali ya Mandy haikujulikana kwa wakati huo kuwa ataamka lini wala saa ngapi laiti kama taarifa ya kuamka kwake ingewafikia madaktari basi tumaini lingekuwa kubwa sana.

Akiwa nje ya wodi ile, Desmond aliendelea kutafakari kuhusu usalama wa Mandy, alifikiria kama Mandy alikuwa amekufa au alikuwa hajafa na kama hajafa basi siri yake iliyojificha kuhusu Mama yake Mandy ingefichuka, akiwa hapo alisikia sauti ikimuita

“Mr Desmond” Alipogeuka alimuona Mtu mmoja akiwa amemsimamia, alishtuka sana sababu hakutarajia kumuona Mtu huyo kwa wakati huo

“Mbona umeshtuka au hukutarajia kuniona?” Alihoji Mtu huyo aliyekuwa Mwanaume mwenye sauti nzito

“Hapana ila nilikuwa mawazoni ndiyo maana nimeshtuka” Alisema Desmond kisha aliketi vizuri ili Mwanaume huyo naye aketi

“Hali ya Mkeo vipi?” Aliuliza Mwanaume huyo

“Mke wangu anaendelea…Hali yake bado ipo vile vile” Alijibu Desmond

“Mkeo ni shahidi namba moja wa kifo cha Mama yake, mara ya mwisho alituma ujumbe kituo cha polisi kuwa anamjuwa Muuwaji wa Mama yake, baada ya hapo ndiyo tukio la wewe kupigwa risasi na Mke wako kupigizwa ukutani lilipotokea, Mkeo ni Mtu muhimu zaidi katika kesi ile” Alisema Mwanaume huyo ambaye sasa alitambulika kuwa ni askari

“Yaah! Ni kweli, ilikuwa ni siku ngumu sana katika Maisha yangu ni kama nilimpoteza Mke wangu tokea siku ile hadi hivi leo” Alijikakamua Desmond kisha alijibu, huyu Desmond alionekana wazi kutambua juu ya kifo cha Mama yake Mandy lakini kwanini hakutaka ukweli uwekwe wazi? Au yeye ndiye aliyemuuwa Mama yake Mandy? Kwanini Amuuwe? TUSONGE MBELE

“Kwa lolote usisite kutujulisha Mr. Desmond” Alisema Askari huyo kisha aliondoka hapo. Kumbe nesi Lucia alikuwa anamuangalia Desmond akizungumza na polisi kisha alipoondoka yeye alimfuata Desmond alipokaa

“Desmond najuwa unavyojisikia, najuwa unaumia sana lakini Mkeo atakuwa sawa tu siku moja mtarudi kuwa kama zamani” Alisema Nesi Lucia, Desmond alimtazama Lucia kisha alijisemea moyoni

“Ungejuwa ninavyotamani afe wala usingesema hayo maneno” Kabla hajamjibu chochote Lucia alipokea simu ya Noela

“Hello” Alisema Desmond baada ya kupokea simu hiyo

“Desmond nakusubiria Mgahawani” Alisema Noela kisha Desmond alijibu

“Sawa nakuja”

“Unaenda wapi?” Alihoji Lucia

“Mjini”

“Hata mimi ninaenda huko kwa ajili ya chakula, tafadhali nipe lifti” Alisema Lucia

“Haya sawa!” alisema Desmond kisha waliongozana hadi kwenye gari ya Desmond na safari ya Kuelekea Mjini ilianza.

Wakiwa barabarani Nesi Lucia macho yake yote yalikuwa kwa Desmond, alimpenda sana Mwanaume huyo lakini alishindwa kumwambia sababu alikuwa Mume wa Mtu istoshe alikuwa akimuuguza Mke wake huyo.

Desmond aligundua hilo akamuuliza Lucia

“Kwanini unaniangalia hivyo?”

“Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwa na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha Desmond alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafika eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawa huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake Noela

“Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” Aliuliza

“Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee na majukumu mengine”

“Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingia kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na pia ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipanga kuonana na Noela.
 
SEHEMU YA PILI

Waliagiza chakula kwa pamoja kisha walianza kula huku wakizungumza masuala yao ya kimapenzi, japo Desmond alikuwa akicheka ila akili yake ilikuwa kule Hospitalini alipo Mke wake, ucheshi wa hapa na pale uliendelea huku wakinyweshana na kulishana, ghafla simu ya Desmond iliita, kutokana na hofu aliyonayo alijikuta akiangusha glasi ya Juisi ikamwagikia kwenye nguo ya Noela

“Oooh samahani mpenzi naomba nipokee simu” Alisema Desmond

“Usijali Joshua, naenda chooni mara moja” Alisema Noela kisha alinyanyuka akaelekea chooni kwa ajili ya kujisafisha.

Aliingia chooni akajisafisha vizuri lakini wakati anatoka alikutana na Nesi Lucia, walikuwa ni marafiki wa zamani sana, basi walipoonana walikumbatiana kwa furaha

“Eeeh za Maiaka Noela?” aliuliza Lucia

“Nzuri, jamani Lucia umekuwa mzuri hivyo jamani” Alisema Noela kisha alimkumbatia tena Lucia

“Oooh Miaka mingi imepita Maisha yapoje?” aliuliza Lucia

“Mungu anasaidia, kuna kipindi nilisikia umekuwa Mwanasheria mzuri sana Nchini”

“Yeah!! Mimi ni Mwanasheria pia mpelelezi nina kampuni yangu Binafsi japo bado nipo serikalini, wewe je?” Alisema Noela kisha alitupa swali kwa rafiki yake huyo wa zamani

“Namshukuru Mungu mimi ni Nesi napambana na wagonjwa” Alijibu Lucia kisha walicheka kwa pamoja, walipeana namba za simu kisha Lucia aliuliza

“Kumbe unakujaga hapa kula?”

“Ndio mara nyingi sana ila leo nipo na Shemeji yako”

“Oooh! natamani kumuona jamani, hapana shaka ni mzuri kama wewe mwenyewe” Alisema Lucia

“Ha!ha!ha! hujaacha utani tu, haya twende ukamuone” Alisema Noela

“Haya twende mara moja, ni muda sana aisee kweli Maisha yanabadilika” Alisema Lucia kisha stori zao zingine ziliendelea, Desmond alikuwa bize na simu hivyo hakujuwa kama Mpenzi wake ameongoznaa na nesi anayemuhudumia Mke wake Hospitalini.

Bahati nzuri ile anageuka anawaona Lucia na Noela wakienda alipo, Desmond aliinama chini

“Ina maana Nesi Lucia na Noela wanafahamiana, oooh nimeshaharibu hapa, vipi kama Lucia akimwambia Noela kuwa nina Mke?” alijiuliza Desmond, aliponyanyua tena kichwa alimuona Noela akiwa peke yake, alishangaa sana wakati sekunde chache alikuwa ameongozana na Lucia, Noela aliketi

“Mwenzio yupo wapi?” alihoji Desmond kwa umakini sana

“Ni rafiki yangu yule kumbe ulimuona, anaitwa Lucia ni nesi, nilisoma naye kitambo” Alijibu bila wasiwasi Noela lakini hakutatua kiu ya Desmond ya kutaka kujuwa alikuwa ameenda wapi

“Yupo wapi sasa?” Alihoji Desmond

“Amepigiwa simu kuwa kuna Mgonjwa amerudisha fahamu hivyo ameelekea Hospitali” Kusikia hivyo Desmond alijuwa moja kwa moja ni Mke wake Mandy

“Amerudisha fahamu, hajataja chochote?” aliuliza Desmond kama Mtu aliyeingiwa na kichaa

“Kutaja chochote? Nani unamzungumzia”

“Aah samahani, siwezi kuendelea kuwa hapa mpenzi” Alisema Desmond kisha aliondoka hapo mbio mbio

“Hivi huyu Mwanaume anan nini siku hizi mbona amekuwa na tabia za hovyo? mara hapokei simu mara anazungumza vitu sivielewi” Alijiuliza Noela kwa sauti iliyoambatana na kilio kidogo.

Haraka haraka Desmond alifika Hospitalini ambako Mandy alikuwa amelazwa, alikuwa amechoka mwili na akili yote huku hofu yake ikiwa kwa Mandy kuwa ameamka, alipofika wodini alimkuta Mandy akiwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua, pembezoni kukiwa na daktari, wahudumu wote wa afya ndani ya Hospitali hiyo walikuwa wakimfahamu Desmond, yule Daktari alimuuliza

“Mbona upo hivyo Desmond” Aliuliza akiwa anafanya kazi yake, Desmond alitikisa kichwa chake kisha alitoka wodini humo akiwa amechoka sana, kiasi fulani alishusha pumzi zake baada ya kugundua kuwa Mandy alikuwa hajazinduka, alishika sehemu ya moyo wake kama ishara ya hali yake ya wasiwasi.

************

Jioni Noela aliporudi nyumbani kwao alijikuta akikosa raha, mvua ilikuwa ikinyesha hivyo alijifungia chumbani kwake, alianza kupitia mafaili ya kazi zilizo mbele yake. Kila alichokisoma hakikuingia kwenye akili yake, alijiona ana mzigo mzito kichwani pake.

Alijilaza kitandani akiwa hoi kwa mawazo, Desmond alimchanganya sana kwa jinsi alivyobadilika ghafla, hakujuwa jambo zito lililo kichwani pa Desmond ambaye yeye alikuwa akimfahamu kama Joshua, wakati anawaza baadhi ya mambo alijikuta akikumbuka tukio la mchana alivyokutana na rafiki yake wa zamani ambaye ni nesi Lucia. Alifikiria amtafute maana baada ya kupeana namba ule mchana hakuna aliyemtafuta mwenzake, alinyanyua simu yake akampigia, simu iliita kwa kitambo kidogo kabla ya kupokelewa.

“Hello Lucia” Alisema Noela

“Abee kipenzi! nilitingwa kidogo nikasema nikutafute baadaye” Alisema pia Lucia

“Oooh nafikiri hiyo baadaye ndiyo hii, hebu subiri vipi hali ya huyo Mgonjwa wako uliyemkimbilia?” Aliuliza Noela maana alipoachana na Lucia ule mchana alikuwa alikimbilia Hospitali

“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri sana, sijui shem wangu japo sikubahatika kuonana naye” Alisema Lucia

“Naye yuko poa Lucia, usijali utamuona siku moja” Alisema Noela

“Anaitwa Nani vile?” aliuliza Lucia, Noela alikaa kimya kwa sekunde chache kisha akamjibu

“Anaitwa Joshua”

“Ohooo ana jina la kipekee, natumaini ni mzuri kama wewe” Alisema Lucia kisha wote walicheka kisha waliagana kwa kutakiana jioni njema na mara moja simu ilikatwa.

Noela alishusha pumzi zake, angalau kidogo alijiona hana mzigo mzito kichwani.

Mara mlango wa chumba chake uligongwa, alijisomba kitandani akaenda kuufungua, alikuwa ni Mama yake aliyezoea kumuita Mlami

“Vipi Mlami?” Alihoji Noela, alimtazama Mama yake alikuwa ameshikilia kikombe cha Maziwa

“Na hii baridi nimekuletea maziwa ya moto Binti yangu, vipi ulizungumza na Joshua?” Aliuliza Mama yake Noela akiwa anampatia Noela kikombe chenye maziwa, Noela alikipokea kisha alimjibu Mama yake akamwambia

“Ndiyo Mama! Lakini Joshua siku hizi simuelewi elewi” Alisema kisha alipiga maziwa kidogo

“Humuelewi? Kwani amekuwaje!” Aliuliza Mama Noela

“Wee Mlami acha tu, nitakueleza vizuri Mama. Nikutakie jioni njema” Alisema Noela kisha alifunga mlango, hali hii ilimfanya Mama yake Noela kupata mawazo ya jambo lipi lililokuwa likimsibu Binti yake.

Siku iliyofuata mapema sana Desmond alikuwa ofisini kwake akiendelea na kazi, alionekana kuwa bize sana siku hiyo kuliko hata kawaida yake. Akiwa anaendelea na kazi alisikia simu yake ikiita, alipotupa macho kwenye kioo aliona ni askari ambaye alikuwa alichunguza tukio la kifo cha Mama Mandy ambaye alionana naye kule Hospitalini, ndiye aliyekuwa akimpigia Desmond. Aliishika simu akiwa ana tafakari huku akijiuliza askari huyo alikuwa akitaka kusema nini?

“Kwanini ananipigia leo?” Alijiuliza huku simu ikizidi kuita, aliweka sauti vizuri kisha aliipokea

“Hallo” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa umakini wa hali ya juu

“Mr. Desmond, mtuhumiwa namba moja wa kifo cha Mama Mandy ameonekana kwenye kijiji kimoja kinachoitwa Pendahili ambacho kipo kaskazini mwa Mkoa jirani, tukimpata yeye tutakuwa tumepata ufumbuzi wa kesi hii” Ilisikika sauti ya Askari huyo, Desmond alishtuka sana akauliza

“Unamaanisha Sanga?”

“Ndiyo! Mfanyakazi wenu wa ndani aliyepotea baada ya tukio lile lililopelekea Mkeo kuwa katika koma”

“Amekamatwa?”

“Bado hajakamatwa ila tayari tumetuma polisi kuelekea huko sasa hivi” Alisema Askari huyo

“Haya asante kwa taarifa” Alisema Desmond kisha alikata simu hiyo haraka sana

“Sanga anawezaje kurudi Kijijini kwao wakati tulikubaliana aende mbali?” Alijiuliza Desmond akiwa ameshikilia simu yake, akakumbuka jinsi ilivyokuwa siku ya Tukio

Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiongea na Huyo Sanga ambaye alikuwa ni mfanyakazi wao wa ndani wakati huo Mwili wa Mandy ukiwa katika ngazi ukivuja damu. Desmond alikuwa ametapakaa damu mikononi, alimwambia Sanga akiwa katika hali ya Kuchanganikiwa sana

“Polisi watakuja hapa watakukamata Sanga kwasababu kuanzia sasa wewe ndiye Muuwaji uliyemuuwa Mke wangu! Ukikamatwa utaozea jela, nakupa pesa uwende mbali sana na usirudi” Alisema Desmond kisha alipandisha juu akarudi na kiasi kikubwa cha pesa akampa Sanga

“Kumbuka hupaswi kwenda Kijijini kwenu wala kujulikana mahali ulipo” Sanga naye alikuwa amechanganikiwa alipokea pesa hizo kisha alikimbia nyumbani hapo, kisha Desmond aligeuka akamtazama Mke wake ambaye aliamini alikuwa amekufa, alichukua bastola akajipiga begani, aligumia kwa maumivu akajilaza chini kisha akapiga simu polisi, walipofika polisi Desmond aliwaambia polisi hao kuwa aliyefanya matukio hayo alikuwa ni Mfanyakazi wao wa ndani aliyeitwa Sanga.

Tokea siku hiyo Sanga aliyafutwa kila kona huku akihusishwa na tukio la kutaka kufanya jaribio la kumuuwa Mandy pamoja na Desmond, tukio hilo likahusishwa kitaalam na ufichaji wa siri ya kifo cha Mama Mandy ambacho kilitokea miezi miwili iliyopita kabla ya tukio hilo.

Desmond alimaliza kukumbuka kisha alisema

“Sanga ukikamatwa utatoa siri ya ulichokiona, sitoruhusu hilo litokee” Mara moja Desmond aliondoka ofisini hapo akachukua gari yake akaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji hicho ambacho alitokea Sanga. Aliendesha gari kwa spidi sana ili awahi kabla ya polisi kumkamata Sanga.

Upande wa pili, Noela alikuwa akimpigia simu sana Desmond bila mafanikio ya kupokelewa kwa simu hiyo hali iliyomfanya azidi kuwa na wasiwasi na mpenzi wake huyo, alimuita Zanda akampa kazi ya kumtafuta Desmond kwa njia ya mtandao ili ijulikane mahali alipo Desmond, hofu na mashaka vilianza kumuingia Noela huku akitafakari mpenzi wake huyo alikuwa akipitia jambo gani maana alikuwa haeleweki, ndani ya dakika kadhaa mtandao ulionesha alipo Desmond, alikuwa akitoka nje ya Jiji hilo.

“Aaas!! Anaenda wapi!?” Alijiuliza sana Noela kisha alichukua kibegi chake akaondoka ofisini hapo.

Safari ya Desmond kuelekea Kijijini ilizidi kusonga mbele, lengo likiwa kumzuia Sanga asiingie mikononi mwa polisi, alizidi kuunguza mpira kwa spidi kali sana.

Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika Kijijini hapo.

Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuata Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenye gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyo alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo, alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangaza huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbani anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu, hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. Macho ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond alienda hadi alipojificha Sanga

“Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapo na Sanga
 
“Naanzaje kukataa Joshua? Nipo tayari uniowe hata kesho. Nikikumbuka jinsi tulivyokutana moyo wangu unajawa na furaha na amani sana. Nakupenda pia Joshua” Alisema Noela kisha alimkumbatia Desmond.

Sura ya Desmond ilibadili taswira kutoka kutabasamu hadi kuwa mtu aliye siriazi na jambo lililo akilini mwake.

Majukumu ya kazi yaliendelea kwa pande zote yaani kwa Desmond na kwa upande wa Noela, kumpata Desmond kulimpa furaha sana Noela akawa anachapa kazi zake.

Mchana wa siku hiyo, Desmond alienda Hospitalini kama kawaida, alipewa nafasi ya kumuona Mke wake Mandy. Alikuwa na hasira na Mwanamke huyo. Mandy alikuwa amepoteza fahamu kwa zaidi ya miezi mitano hivyo kwa kipindi chote alikuwa Hospitalini tu, Desmond alisogea akaketi kwenye kiti kimoja ambacho kilikuwa kando ya kitanda cha Mke wake, alikunja nne kisha akamwambia Mandy

“Nina uhakika unanisikia Mandy! Katika vitu sitamani kuona katika Maisha yangu basi ni uhai wako, natamani uwe umekufa na usiamke tena hapo Kitandani” Alisema Desmond akiwa amevalia suti nyeusi zilizomkaa vizuri, alikuwa kijana mwenye muonekano mzuri sana. Desmond alisimama kisha alimsogelea Mandy

“Siri unayoijuwa kuhusu Mama yako ibaki kuwa siri ya Ulimwengu mzima, sipo tayari kuyaharibu Maisha yangu kwasababu yako. Asante kwa utajiri mkubwa ulioniachia Mandy, nasikitika sababu uliyemuamini siku zote hakuwa na mapenzi na wewe, sikuwahi kukupenda Mandy….Nilizipenda pesa zako tu” Alisema Desmond kisha alivuta pumzi zake huku chozi likimlenga, licha ya uamuzi huo mgumu bado alionesha kuumia ndani ya Moyo wake

Ghafla aliona Mandy akitingisha kidole, hii ilimshtua sana Desmond, miezi yote Mandy hakuwahi kutingisha hata kope za macho yake, ilionesha wazi hata alichokizungumza Desmond alikuwa akikisikia. Akiwa anaendelea kushangaa Desmond aliona macho ya Mandy yakifunguka huku yakibubujikwa na mchozi, Mandy alikuwa ni Mwanamke mzuri mwenye weupe wa asili, chozi la Mandy lilionesha wazi kuwa lilibeba maumivu makali sana

“Mandy umeamka? Ina maana siri yangu utaisema!! Hapana Unakufa” Alisema Desmond ndani ya moyo wake huku akiwa amevurugwa sana, aliangalia huku na kule kisha alichukua mto na kumziba pumzi Mandy ili afe pale kitandani. Mandy alihangaika kwa nguvu chache aliyokuwa nayo lakini hakuweza kufanya lolote zaidi ya kuziona pumzi zake zikifika mwisho, Desmond alidhamiria kumuuwa Mandy mchana huo ili hiyo siri yake isijulikane.

Mara Desmond alisikia chupa ikivunjika, alipogeuka alimuona nesi Lucia akiwa anaokota vipande vya vyupa pale mlangoni. Haraka aliacha jaribio la kutaka kumuuwa Mke wake Mandy. Aliuweka mto pembeni, alikuwa akitokwa na jasho jingi kisha alimtazama Mandy alionekana kuzima, Desmond aligeuza macho alimuona nesi Lucia akisogea hapo

“ooh Desmond” Alisema Nesi Lucia huku akiwa anaweka vifaa juu ya meza iliyo pembe ya ukuta, alipomtazama vizuri Desmond alimuona akiwa anatokwa na jasho jingi sana, alishangaa kisha alipeleka macho yake kwenye AC, kisha alirudisha kwa Desmond. Alionekana kushangaa jasho la Desmond lilitoka wapi ikiwa chumba hicho kilikuwa hakina joto kabisa

“Kulikoni Desmond mbona unavuja jasho hivyo” Aliuliza Nesi Lucia akiwa anamtazama kwa makini Desmond

“Aaah- aaah…Jasho….unajuwa!! Lucia sijisikii vizuri naomba nipumzike nje” Alisema Desmond kisha alitoka lakini Nesi Lucia aliendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu, mwisho alipuuzia jambo hilo.

Alienda kumtazama Mandy, alionekana kupowa huku mapigo ya moyo yakienda sawa kwa maana Desmond hakufanikiwa jaribio la kuondoa uhai wa Mandy, alibadilisha dripu na kufanya mambo mengine kisha naye alitoka. Hali ya Mandy haikujulikana kwa wakati huo kuwa ataamka lini wala saa ngapi laiti kama taarifa ya kuamka kwake ingewafikia madaktari basi tumaini lingekuwa kubwa sana.

Akiwa nje ya wodi ile, Desmond aliendelea kutafakari kuhusu usalama wa Mandy, alifikiria kama Mandy alikuwa amekufa au alikuwa hajafa na kama hajafa basi siri yake iliyojificha kuhusu Mama yake Mandy ingefichuka, akiwa hapo alisikia sauti ikimuita

“Mr Desmond” Alipogeuka alimuona Mtu mmoja akiwa amemsimamia, alishtuka sana sababu hakutarajia kumuona Mtu huyo kwa wakati huo

“Mbona umeshtuka au hukutarajia kuniona?” Alihoji Mtu huyo aliyekuwa Mwanaume mwenye sauti nzito

“Hapana ila nilikuwa mawazoni ndiyo maana nimeshtuka” Alisema Desmond kisha aliketi vizuri ili Mwanaume huyo naye aketi

“Hali ya Mkeo vipi?” Aliuliza Mwanaume huyo

“Mke wangu anaendelea…Hali yake bado ipo vile vile” Alijibu Desmond

“Mkeo ni shahidi namba moja wa kifo cha Mama yake, mara ya mwisho alituma ujumbe kituo cha polisi kuwa anamjuwa Muuwaji wa Mama yake, baada ya hapo ndiyo tukio la wewe kupigwa risasi na Mke wako kupigizwa ukutani lilipotokea, Mkeo ni Mtu muhimu zaidi katika kesi ile” Alisema Mwanaume huyo ambaye sasa alitambulika kuwa ni askari

“Yaah! Ni kweli, ilikuwa ni siku ngumu sana katika Maisha yangu ni kama nilimpoteza Mke wangu tokea siku ile hadi hivi leo” Alijikakamua Desmond kisha alijibu, huyu Desmond alionekana wazi kutambua juu ya kifo cha Mama yake Mandy lakini kwanini hakutaka ukweli uwekwe wazi? Au yeye ndiye aliyemuuwa Mama yake Mandy? Kwanini Amuuwe? TUSONGE MBELE

“Kwa lolote usisite kutujulisha Mr. Desmond” Alisema Askari huyo kisha aliondoka hapo. Kumbe nesi Lucia alikuwa anamuangalia Desmond akizungumza na polisi kisha alipoondoka yeye alimfuata Desmond alipokaa

“Desmond najuwa unavyojisikia, najuwa unaumia sana lakini Mkeo atakuwa sawa tu siku moja mtarudi kuwa kama zamani” Alisema Nesi Lucia, Desmond alimtazama Lucia kisha alijisemea moyoni

“Ungejuwa ninavyotamani afe wala usingesema hayo maneno” Kabla hajamjibu chochote Lucia alipokea simu ya Noela

“Hello” Alisema Desmond baada ya kupokea simu hiyo

“Desmond nakusubiria Mgahawani” Alisema Noela kisha Desmond alijibu

“Sawa nakuja”

“Unaenda wapi?” Alihoji Lucia

“Mjini”

“Hata mimi ninaenda huko kwa ajili ya chakula, tafadhali nipe lifti” Alisema Lucia

“Haya sawa!” alisema Desmond kisha waliongozana hadi kwenye gari ya Desmond na safari ya Kuelekea Mjini ilianza.

Wakiwa barabarani Nesi Lucia macho yake yote yalikuwa kwa Desmond, alimpenda sana Mwanaume huyo lakini alishindwa kumwambia sababu alikuwa Mume wa Mtu istoshe alikuwa akimuuguza Mke wake huyo.

Desmond aligundua hilo akamuuliza Lucia

“Kwanini unaniangalia hivyo?”

“Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwa na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha Desmond alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafika eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawa huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake Noela

“Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” Aliuliza

“Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee na majukumu mengine”

“Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingia kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na pia ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipanga kuonana na Noela.
Majina ya kina Desmond yameingia Dosari kuanzia leo 😜
 
Nyuzi zako zote zinahusu kikojoleo😊! Vipi? Huna kingine cha kuandika?
 
Ahahah na ww ukazane kusoma sasa ila hii ndefu kidogo kwahy naombeni mnipe muda kwa siku mmoja siwezi maliza ata ww unae soma kwa siku moja uwezi maliza
Mimi Mwandishi Stori ndefu ndo nazipenda Nasoma dakika 😜😜lete mambo
 
Yangekuwa mambo ya teknolojia usingesoma mara watu wangelalamika kuwa ni ndefu. Our brains love pleasure by all costs found on the universe
Hatuwezi kusoma vitu vigumu kila wakati tunahitaji vitu vizuri tupumzishe akili.
 
Back
Top Bottom