PreGE2025 Nimeumia sana chama kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ za uongozi mpya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Na wewe ungeondoka uwafwate wenzako,unasubiri nini,
 
Mzee Makanja ametoa sababu tatu kubwa kwa nini wameondoka ni kuwa hawana maslahi binafsi humo yamekatwa. hamna namna chama chini ya Mbowe kilishapoteza mwekekeo. sasa hivi wananchi wameanza kurudisha imani.
 
We mjinga pamoja na wenzio mliokua mnajiita team mbowe ndo wavurugaji wakubwa wa chama..!!

Mna tamaa na madaraka kwendeni, bado wewe wakutimue ukacheze na mizimu yako.!!
 
Wakati nyie mnahama, sisi tunapanga kuingia huko ili kuongeza nguvu tuitie presha ccm kwa maslahi mapana ya Tanzania
 
Chama kimeparanganyika au njaa kali waliotaka nusu mkate wamekutana na hewa nzito hakuna ventilation wametoka nduki?
Asante kwa bandiko lako, ama kweli kweli ni hewa nzito, hakuna ventilation , lazima watoke kama kasongo Warthog huko shimoni. Umenichekesha sana.
 
Zitto ni msaliti na vijana wake habibu change, juliana shonza na mtela mwampamba, tunaomba mwenyekiti mbowe amvue uanachama kwa kushirikiana na TAL
 
Eti unafikiria kushika madaraka na kufanya mageuzi, sijui nani kakudanganya CCM inaweza kukuachia madaraka kirahisi.

Serikali ya CCM inapaswa kulazimishwa kubadili mifumo na sera ili iwafae Watanzania wote.
 
Kumbe familia ya Nyerere ilikuwa sahihi kukupiga marufuku@Yericko Nyerere kutumia jina la Mzee wao kama ubini wako. Kwa huu uzwazwa ulioonyesha, Madaraka Nyerere alikuwa sahihi.
 
Na mtuambie aliyehujumu chama kuwapeleka COVID 19 bungeni ni nani? Na zaidi kwanini wahame watu wa upande ule tena waliokuwa viongozi waandamizi? Wapumbavu wakubwa nyie!
 
Binafsi nilikuwa nawadharau sana CDM, kila mwaka wanashiriki uchaguzi wakishindwa wanakuja na ngonjera za "uchaguzi haukua huru na haki". sasa nilikuwa najiulizaga unakwendaje kwenye uchaguzi unaojua kabisa hautakuwa huru na haki.
 
Wala usiumie, hakipo na hakitakuwepo daima chama Cha siasa Duniani ambacho wanachama hawatatoka na wala hawataingia wapya. Kwa mtazamo wangu Hawa waliotoka ni Hila zao na kushindwa kukubali kwamba kambi yao ilishindwa na sasa mwenyekiti ni TAL. Acha waondoke bana. What is 55 in millions of followers. Hata wewe nakuona tu una Hila na unafurahi kuona wameondoka. Hapa ni kata mti panda mti. No reforms no election. Ni mjinga tu ndiye anaweza kuingiza chama kwenye uchafuzi wa October. Mwamba atatoka na mapambano yataendelea.
 
Hakuna mtu anayeweza kunidanganya kwa lisu huyu ndo mwambaaa wa bongoo mwambaaa wa dar mwambaaa wa lusaka.
 
Wananchi waliowengi na wapenda mabadiliko wanayoimani kubwa sana na Tundu Lissu, hivyo chadema kwa sasa ipo mikono salama.
Wait and see
 
Kuondoka kwa sekretariati ya Mbowe ndiyo transformation yenyewe ndani ya Chadema hakuna namna hata Samia alipoingia CCM kama mwenyekiti akina Polepole Bashiru nk waliondoka hii ni kawaida katika kujenga utamaduni mpya na imani kwa wananchi wamejinyanyapaa wenyewe kwa maovu waliyo fanya wakiwa sekretariati msikilize mzee Makanja.
 
Mwenyekiti na Katibu wa tawi lako wanakuchelewesha sana wewe na tapeli Mbowe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…