PreGE2025 Nimeumia sana chama kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ za uongozi mpya!

PreGE2025 Nimeumia sana chama kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ za uongozi mpya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
WE SHALL WIN!

Na Yericko Nyerere
Mkuu 'Erythro', umeiona hii?
Mkuu Yerricko unaweza kweli kusema Chanzo cha hawa G55 kuondoka ni uchaguzi au madaraka?

Ina maana Yericko bado yumo kwenye mapambano, ni yapi hayo?
Huku wakati huo huo anasema CHADEMA "imeparaganyika". Sasa anatazamia ku-WIN nini/wapi/lini?

Enzi zile nilikuwa nikikwambia CHADEMA na CCM hawakuwa na tofauti yoyote. Usifikiri nilikuwa nayasema yale maneno kirahisi rahisi tu!
Utakuwaje na watu wenye fikra kama hizi ndani ya chama; halafu useme unacho chama unachotegemea wananchi watakipenda kiwaongoze?
 
Kama umeumia sana si uchomoe tuu kinacho kuuma shida iko wapi kwani wafuate wenzako huko
 
Chama kipo imara kijana than ever. CDM kwa sasa ipo kitaifa zaidi maana imebeba ajenda ya wananchi.
Hakuna mwananchi yeyote ambaye atakwambia uchaguzi Tanzania huwa huru na haki, eti hao jamaa leo wanadai wanautaka wa Otober wakati uchaguzi Serikali za mitaa wakiwa viongozi WALIPIGWA nje ndani chama kikaambulia SIFURi kama si unafiki ni nini.

Hao waende, tena waondoke na wake zao kabisa kabisa hatutaki kesi sisi kwamba wamepewa ujauwazito.
 
Nia yako ovu Iko katikati ya maneno ya HEADING yako.mpumbavu mkubwa wewe😡
 
Kuna mtu akikihama chama unasikitika sasa huyo salum mwalimu ana impact gani
 
Naona mnazidi kuchanganyikiwa! Yaani team Mbowe mngetoka wote mngekuwa mmekisaidia Sana chama kujenga safi yake mpya isiyo na madalali. Amini yote yanayofanyika sasa ni mpango wa Mungu kuijenga cdm mpya. Hivi we mhehe kwa akili yako Lissu anaweza kufanya kazi na Mtu Kama Mrema au Mwalimu?
 
Sisi tumetoka CCM tukaja Chadema baada ya kuona hatima mpya ya uongozi, hawa wanaoondoka ndio miongoni mwa wale waliokiuza chama Kwa EL..na tukaondoka...nyie ni wachache kuliko mamilion ya wananchi wanaoiona Tanzania mpya ndani ya Chadema Mpya.
 
Sema hapa lisu kafeli kweli kwa mtazamo wangu
Uongozi wakati mwingine unahitaji kushuka
Alipaswa kuwarudisha hata wale wabunge wa viti maalum
#weneedeachother
 
Nimeumia sana, imenichukua masaa kadhaa kusema chochote baada ya uamuzi huu mgumu wa waliokuwa viongozi wakuu wa Chama changu Chadema Naibu Katibu Mkuu Bara Mh Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh Salumu Mwalimu na Waliokuwa wajumbe wa Sekretaieti yote ya Chama kujivua uanachama wa Chadema.

Nimeumia kwasababu tatizo hili uongozi mpya umeshindwa kulitibu tangu uchaguzi ulipomalizika, Tulishauri uongozi mpya uwaunganishe wanachama waliogawanyika baada ya Uchaguzi, Lakini walioshinda wakakomaza mafuvu na kutupuuza, wakatuita tuna madonda ya uchaguzi hayajapona kisha tukaitwa wasaliti na mwisho tukaitwa maccm. Haya ndio yametufikisha hapa.

Katika siasa lolote linatokea, huu ndio utofauti wa siasa na harakati, Mwanasiasa anafikiria kushika madaraka ili afanye mageuzi ya sheria na mifumo mbali mbalimbali ya kijamii. Wakati huo Mwanaharakati anafikiria kuhimiza mageuzi ya sheria na mifumo mbalimbali ya kijamii, Yaani mwanaharakati hafikirii kuitoa ccm madarakani bali kuishinikiza ccm ifanye mageuzi ya sheria na mifumo ya kijamii tu, Kwamba ccm ikitekeleza madai hayo, basi mwanasiasa huyo anaweza kuhamia tu katika madai mengine mfano haki ya wanafunzi wa kike kupewa taulo za kike, Haki ya wanaume kupata unyumba kwa wake zao, nk. Hii ndio tofauti kuu.

Ninawapongeza viongozi hawa kwa uamuzi wao ili wakatimize ndoto zao katika majukwaa mengine kwakuwa jukwa lako walilolijenga kwa maisha yao likawa jukwaa pendwa kwa umma limeharibiwa na wanaona linaenda shimoni. Vyama vya siasa ni vyama vya hiyari, ukiona hapa wenzio hawakutaki basi unatafuta jukwaa lingine.

Niwatakie mapambano mema huko waendako, Mimi nitapambana ndani ya Chadema ili kujaribu kukirejesha chama kwenye misngi yake na kuhakikisha chama kinafuata katiba na miongozo yake, Na kurejesha umoja na mshikamano uliojengwa kwa miaka mingi.

Nimeumia sana chama changu kuvunjika na kuparaganyika siku 70+ tu za uongozi mpya!😭😭😭😭

WE SHALL WIN!

Na Yericko Nyerere

View attachment 3327116
Sisi tupo na mwamba lissu nenda mwana kwenda.
 
Hivi Chama kinaparaganyika nini kisa wanachama kujitoa kwenye chama? Kwani chama ni gereza? Hiyo demokrasia mnayohubiri ni ipi;? Japo ni wazi Hawa walizoea kuwa na vyeo.Salumu mwalimu na kigaila walipaswa kabisa kuvuliwa uongozi Toka kipindi kile Cha mbowe, wake zao wakiingia kinyemela bungeni kupitia COVID 19
 
Chadema ilijengwa kwa damu na jasho la watu, chadema kwa sasa hakuna chama cha upinzan kinachoweza kuitoa katika nafasi yake. Kwa kifupi hakuna mbadala wa chadema.

Hii ni kwa sababu ya uanzishwaji wake na namna kilivyoanzishwa pamoja na harakati na operation mbalimbali zilizofanyika miaka takribani 15 iliyopita.

Chana hicho hakiwez kupotea kwa sababu ya akina kigaila na wenzake wameondoka.

Hivi unaijua nguvu aliyokuwa nayo Dr. Slaa?? Au Zitto Kabwe, au akina Prof Kitila na wenzake?? Hawa wote waliondoka lakini chadema bado imeendelea kuhofiwa na watawala, jiulize hicho ni chama cha aina gani??

Hawa walioondoka bado hawaamin kama mbowe ameondoka kwenye kiti chake. Hawajakubali kama chama kinaweza kuongozwa na mtu mwingine tofauti na Mbowe.

Ushauri wangu kwa chadema. Waboreshe kitengo cha research, wafanye recruitment ya wasomi ndani ya chama walio na uwezo mkubwa wa kufanya analysis na kuja na sera mbadala.
Bado najiuliza kina MREMA waliamini demokrasia ni kushinda tu? Waliamini mbowe atakuwa mwenyekiti daima.
 
Eti unafikiria kushika madaraka na kufanya mageuzi, sijui nani kakudanganya CCM inaweza kukuachia madaraka kirahisi.

Serikali ya CCM inapaswa kulazimishwa kubadili mifumo na sera ili iwafae Watanzania wote.
Haahaa Leo nimemsikiliza zitto nimeshangaa Sana, eti anagombea ubunge anasema tutapambana tukiwa kwenye uchaguzi, anaulizwa mbona 2020 hamkupambana anabaki kujiumauma tu.Wananchi Gani wataenda kupiga kura upinzani ilhali wanajua kura zao hazitahesabiwa?
 
Wahame tu,wachumia matumbo.
Ndo utagundua kwamba baada ya kukosa ulaji wanaanza kujiengua taratibu,nawachukia watu wanaotanguliza maslahi yao
Leo kigaila na MREMA wanaponda no reform no election mkakati waliobuni wenyewe kisa mbowe kashindwa uchaguzi🤣🤣🤣
 
Sema hapa lisu kafeli kweli kwa mtazamo wangu
Uongozi wakati mwingine unahitaji kushuka
Alipaswa kuwarudisha hata wale wabunge wa viti maalum
#weneedeachother
Haahaa kushuka nje ya taratibu hapana, chama ni vikao mkuu, lissu Hana KOSA, KOSA lake kusimamia maamuzi ya chama, nimejaribu kumsikiliza MREMA na kigaila siwaelewi hasa wanapoanza kuulizz no reform no election🤣🤣 wakati wao walikuwa kwenye secretariet iliyoandaa agenda
 
Back
Top Bottom