Nimeumia sana kuona Mushimba Mugalu akibezwa na baadhi ya mashabiki

Nimeumia sana kuona Mushimba Mugalu akibezwa na baadhi ya mashabiki

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Nimeumia sana kuona mchezaji (Mshambuliaji)wangu ndani ya kikosi changu cha Msimbazi KOPE MUSHIMBA MUGALU akibezwa na baadhi ya mashabiki wasiojielewa.

Nani hajui mziki wa huyu jamaa?
Nani hajui mchango wake kimataifa?
Kwanini hamtaki kumpa hadhi yake huyu mkongomani?

Bila shaka hiyo ni kampeni ya wanayanga maana wanamuogopa sana (wakikumbuka vile visigino) wanadhani kwa kufanya hivyo ataondoka. Bado yupo sana na andaeni dawa za maumivu sasa hivi yupo fit hana injury wala nini dadadekiii.

Simba wenzangu tuungane kutetea wachezaji wetu hasa MUGALU NA KAGERE wanaoonekana kubezwa (kuogopwa)na wapinzani wetu.

SIMBA NGUVU MOJA.
 
Mpira ni mchezo wa wazi hauchezwi chumbani hivyo kila mtazamaji anajua nani mzuri nani mbovu.
Bwana Mushimba ni mchezaji mzuri lakini uchezaji wake hauna tija kwa Simba.
Amesajiliwa kwa lengo la kufunga na si vinginevyo. (Hafungi magoli muhimu mara nyingi ya kuamua mechi, hivyo hatufai).

Amechangia sehemu kubwa ya Simba kushindwa kufikia malengo yake hususani kimataifa kwa kukosa umakini wa kufunga nafasi za wazi kwenye mechi mhimu.

Sanjali ha hilo, ana undugu wa damu na wodi hivyo uhakika wa kuchezaji walau mechi 20 kata ya 30 kwa msimu haupo.

Pia huyu bwana hata akikosa goli hana uchungu yeye ni kunyonya Big G kiulaini mechi iendelee.

Wanaomkataa Chris tafadhali tusiwabeze tuwaunge mkono wameona mbali na wako sahihi.
 
kwani shabiki wamebeza bila sababu? angefanya busara kuondoka mwenyewe kujaribu bahati mahali pengine. strikers wote wametufelisha sana msimu uliopita. ninaficha chuki zangu dhidi yao lakini wanastahili kubezwa
 
Ww ndo unawalipa mshahara?Unaweza kumlipa mtu mihela kibao ukiwa huoni umhimu wake?Unajua mpira (Ufundi)kuliko jopo la makocha wa Simba?Kaa kwa kutulia Mugalu ni bonge la striker
 
Ww ndo unawalipa mshahara?Unaweza kumlipa mtu mihela kibao ukiwa huoni umhimu wake?Unajua mpira (Ufundi)kuliko jopo la makocha wa Simba?Kaa kwa kutulia Mugalu ni bonge la striker
Striker wa familia yenu labda, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mugalu na Kagere waendelee kuwepo kwenye timu coz ni wachezaji wazuri saa na wana potential kubwa ndani ya kikosi

Mm nafikiri simba kwasasa usajili umetosha,kwa wachezaji tuliongeza wanatosha sana na hakuna haja ya kusajili tena

Kaondoka Bwalya,Morrison na Wawa na mbadala wao amekuwa ni Akpan,Okrah na Phiri

Sifikirii kama kuna haja ya kuwa na centre defender 3 wa kimataifa ni bora tuwe na washambuliaji 3 wa kimataifa
 
Mmbadala wa wawa ndo Akpan mkuu?
 
Back
Top Bottom