Kwanza lazima nikiri wazi kuwa Mugalu ni bonge la mashabuliaji na hilo amelidhihirisha kwenye msimu wake wa kwanza aliposajiliwa Simba. Kilichotokea msimu wa pili akiwa Simba hata sijui ni nini nafikiri yeye Mugalu mwenyewe ndio anajua. Mugalu ni mshambuliaji ambaye anajua kukaa sehemu sahihi wakati sahihi, ana kontroo nzuri sana mguuni, anaweza kwenda juu na mabeki hata wawili akarudi chini akabaki na mpira sekunde kadhaa mpaka wenzake wakafika, pasi zake zinafika vizuri na hata "assist" anatoa japo ni mara chache. Kwa ujumla kila kitu anakifanya kwa usahihi kama mshambuliaji kwa asilimia zote. Lakini sasa linapokuja swala la yeye kutimiza wajibu wake kama mshambuliaji wa kati yaaani kutumbukiza mpira wavuni haoni goli!! Na akikosa hata goli la wazi yeye haonyeshi kujutia hata kidogo wakati mwingine unakuta timu yake imeshafungwa inahitaji goli la kusawazisha kwa udi na uvumba lakini jamaa hajali kabisa.
Tatizo kubwa la wapenda mpira wengi nchi hii sio wafuatiliaji wa mpira kiundani kwenye ligi hata za majirani zetu tu hapa karibu. Mugalu alikuwa majeruhi muda mrefu msimu mmoja kabla hajasajiliwa Simba. Viongozi wa Simba sijui waliingiaje mkenge wakampa mkataba wa muda mrefu badala ya kumpa wa muda mfupi ili waendelee kumwangalia kama kapona vizuri. Kwa muda wa miaka hii miwili Mugalu aliyocheza kwenye ligi yetu nafikiri zaidi ya asilimia 25 ya muda huo ameutumia kutibu majeraha na si kucheza uwanjani. Sidhani kama amewahi kucheza mechi 15 mfululizo bila hata kuwa na "injury".
Kwa timu kama Simba ambayo inashiriki mashindano mbali mbali ndani na nje ya nchi hawapaswi kundelea kucheza kamari kwa kuendelea kukumbatia mchezaji kama Mugalu ambaye ni majeruhi wa mara kwa mara. Na vile vile linapofika suala la kutimiza wajibu wake kuamua mechi muhimu kwa kufunga magoli muhimu yeye anakosa magoli tena mengine ya wazi kabisa. Na mbaya zaidi huyo Mugalu ni mchezaji wa kimataifa ambaye analipwa mshahara mkubwa sana. Wakati mwingine ni bora hata kusajili mchezaji wa ndani kuziba nafasi yake ili kupunguza mzigo na gharama kwa timu.
Ni mtizamo tu.