Nimeunda File Server kwa Shilingi Laki 2, Njia Rahisi ya Kuhifadhi na Kuhamisha Mafaili

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
1. Nimepata hard disk 6 TB kwa shilingi 150,000 used (used ila disc health safi )

2. Nimenunua cpu used kwa elfu 50 ikiwa na hard disk ya GB 80 (Hp Optiplex SFF)

Kwanini ninunua cpu wakati ningeweza kununua waya wa usb wa hard disk ?
  • Hard disk iliyounganishwa ndani kwa cable zake maalum za SATA ina kasi zaidi kuliko kutumia USB cable.
  • Hard disk iliyounganishwa ndani kwenye motherboard ina utulivu dhidi ya mitikisiko na vumbi
  • Hard disk iliyounganishwa ndani inapata hewa na kupunguzwa joto kwa feni
  • Hard disk ya ndani haiwezi kung’olewa kwa urahisi kama diski ya nje
  • Hard disk ya ndani hupata umeme wa kutosha kutoka kwenye power supply ni tofauti na usb
  • Hard disk ukiweka ndani ya cpu inakaa muda mrefu zaidi

3. Nimenunua waya wa ethernet wa kuhamishia mafaili shilingi elfu saba ( maduka mengi wanauza nyaya za kuhamisha MB 10 kwa sekunde, nimekuwa makini kununua wa kuhamisha MB 100 kwa sekunde)

4. Mouse na keyboard ninavyo

SETUP

Kwa kuwa PC ni ya zamani, nimeweka "Tiny 10", ni toleo jepesi la Windows 10. Itanifaa kwa kazi ya kutunza na kuhamisha mafaili, kazi nyingine zikifanyika kwenye laptop na simu.

Hard Disc ya GB 80 ni kwajili ya window, Hard disk ya 6 TB ya kutunzia mafaili

Nimetengeneza Network ya kuhamisha mafaili (file sharing) baina ya Pc niliyonunua na laptop yangu kwa kutumia waya wa ethernet, waya una speed nzuri naweza kuhamisha MB 100 kwa sekunde
 
Boss kwani ungeishia kwenye hard disc na cable yake tsh 157,000 siungekua umemaliza tu me naona umeingia hasara isiyo ya lazima ya 43000.
 
Hapo umejiona msomi kweli kweli wa udsm ...hii nchi inawapumbavu wengi sana.
 
Umeme vipi? Desktop yenye hdd 80GB pengine inalamba 100W+ umeme.
 
Boss kwani ungeishia kwenye hard disc na cable yake tsh 157,000 siungekua umemaliza tu me naona umeingia hasara isiyo ya lazima ya 43000.
No, kutumia hard disk ndani ya cpu kuna faida nyingi zaidi kuliko kutumia cable
  • Hard disk iliyounganishwa ndani kwa cable zake maalum za SATA ina kasi zaidi kuliko kutumia USB cable.
  • Hard disk iliyounganishwa ndani moja kwa moja kwenye motherboard ina utulivu dhidi ya mitikisiko
  • Hard disk ya ndani haiwezi kung’olewa kwa urahisi kama diski ya nje
  • Hard disk ya ndani hupata umeme wa kutosha kutoka kwenye power supply ni tofauti na usb
  • Hard disk ukiweka ndani ya cpu inakaa muda mrefu zaidi sababu ya kupunguza mitikisiko na vumbi
 
Kiongozi umejipangaje na backup, kuna hardware failure, accidential deletion au shambulizi la virus...
Ina maana kama una files za muhimu sana utahitaji backup, kwa kila file unayotunza inahitaji kwenda drives mbili tofauti, pengine iwe kwenye server nyingine ya backup tu..
 
Hard ware failure nimeiwekea tahadhari kwa kuiweka hard disk ndani ya cpu, kuna umeme wa kutoha kutoka kwenye power supply, kuzuia mitikisiko, kupunguza vumbi, n.k. Hard disk inaweza kukaa miaka 10 ijayo bila tatizo.

accidental deletion kuna recycle bin

shambulizi la virus nalipunguza kwa kuscan mafaili kwa antivirus

Kuhusu back up, Mafaili yangu muhimu sana ambayo siwezi kuyapata kwengine yana GB 100 tu, nimeyatunza sehemu kama tatu. haya mengine naweza kuyapata upya.
 
Nilichotaka kusema ni kwamba,je mimi naweza kutumia hiyo server yako kutunza file zangu nikiwa huku huku bariadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…