Tatizo uelewa mdogo halafu hujui kama hujui maskini ya Mungu. Bandari yako imepata muwekezaji mpya na hana tofauti na kina TICTS.
DP World sio mwekezaji wa kwanza kuja Tanzania, kwanini anapingwa kwa nguvu zote hizi?. Ni ukosefu wa uzalendo wa watanzania kama ilivyo sifa yetu kuu.
Hiyo treni ya SGR imejengwa kwa trilioni 14, pesa nyingi mno. Inarudije hiyo pesa iliyotumika?. Hayati JPM kufikiria tu kujenga hiyo reli tayari kwetu ni changamoto nzuri sana.
Hakuna anayepora mali ya mtanzania, ni mtanzania mwenye kuwa na upeo wa kubadilisha maisha yake ya kesho, sio kuishi kwa kukariri kule kule kwa jana na juzi.
Ngoja nikuvumilie kigogo, pengine bado unazo akili za kujua ninachokueleza kuhusu ujuha wako..
Mimi nikiwa na uelewa mdogo, wewe utakuwa ni mahututi kabisa; utakuwa huelewi kitu chochote, hapo nikupe mlinganisho tu, kama unao uwezo wa kulinganisha.
Sasa angalia, sijui nikukumbushe mara ngaai? Kama DP World ni mwekezaji ambaye siyo tofauti na TICTS, sasa unamtaka wa nini mwekezaji wa namna hiyo? Umekaa na huyo TICTS hapa zaidi ya miaka 20, akivuna, wewe hukujifunza chochote katika miaka yote hiyo 20, na sasa unaleta mwingine, na yeye avune, tena unampa mkataba usiojulikana utakoma lini? Hapa bado utaniambia unayo akili timamu kweli mtu kama wewe?
Hilo ni jambo la kujivunia, kuleta TICTS mwingine wakati huu, na bila hata ya kuwa na lengo la kuhakikisha unajijengea uwezo wako wa ndani uweze kujiendeshea mambo yako mwenyewe? Wewe kazi yako ni kutegemea tu hao watu wa kukodi waje wakupanguse kamasi na kukufanyia upuuzi mwingi mwingine? Haya ndiyo mambo ya kujivunia kama nchi
Nchi kuwa tegemezi kwa kila kitu, hata kujengewa mashimo ya vyoo?
Nikisema ufikiri wako na hao unaowatetea una kasoro, bado huwezi kuelewa.
DP World sio mwekezaji wa kwanza kuja Tanzania, kwanini anapingwa kwa nguvu zote hizi?. Ni ukosefu wa uzalendo wa watanzania kama ilivyo sifa yetu kuu.
Akili yako kuwa finyu ndiko kunakokufanya uone kuwa ni DP World anapingwa kama mwekezaji. Sijui hili unalitoa wapi?
Uwezo wako wa akili hauwezi kukufanya uelewe kuwa siyo "uwekezaji" unaopingwa, bali ni mkataba mbovu ndio unaopingwa? Wewe hapo huoni tofauti kabisa?
Anayekosa "uzalendo" ni watu kama wewe na hao viongozi wasiokuwa na upeo na kujua maslahi ya nchi yapo wapi.
Hiyo treni ya SGR imejengwa kwa trilioni 14, pesa nyingi mno. Inarudije hiyo pesa iliyotumika?. Hayati JPM kufikiria tu kujenga hiyo reli tayari kwetu ni changamoto nzuri sana.
Unachanganya mambo, kwa sababuhuelewi unachokisema hapa. Unatumia tu jina la Magufuli kujaribu kuhalalisha upuuzi huu unaofanywa na Samia. Reli haikujengwa ili ndiyo iwe sababu ya kuingia mikataba mibovu ya kubinafsisha bandari zetu. Hapa unajaribu kutumia hoja mbovu tu kutetea ujinga unaofanywa na hii mikataba ya DP World, huna lolote la maana. In fact ni mwendelezo ule ule wa kutetea jambo usilokuwa na ufahamu nalo.
Hakuna anayepora mali ya mtanzania, ni mtanzania mwenye kuwa na upeo wa kubadilisha maisha yake ya kesho, sio kuishi kwa kukariri kule kule kwa jana na juzi.
"...mTanzania kubadilisha maisha yake...", huku aliowaweka kwenye madaraka wasimamie shughuli zote za kubadilisha maisha yake wakiwa ndio wahujumu wa juhudi hizo? Unalo tatizo kubwa sana kichwani mwako kutoweza kujua haya.
Kwa hiyo, ni wazi kabisa sasa kutokana na haya unayoandika humu ni wazi kwamba huna upeo kabisa juu ya juhudi za waTanzania kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Sina shaka tena kuhusu uelewa wako mbovu wa yote unayotetea humu kwa maandishi yako.