Nimeuziwa gari la urithi bila kuelewa, najinasuaje huu msala

Nimeuziwa gari la urithi bila kuelewa, najinasuaje huu msala

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Niende moja kwa moja kwenye mada, mwezi wa 6, 2022 kuna jamaa aliniuzia gari Mkoa wa Mwanza (Crown 2010). Tukaandikishiana vizuri kabisa nikatoa hela nikapewa kadi, nikakamilisha taratibu kama bima nk sikuweza badilisha umiliki sababu ya kukosa nakala halisi za jina la mwenye kadi.

Basi katika kuvimba nalo mjini nashangaa juzi napigiwa simu na bi maza anayedai yeye ndo msimamizi wa mirathi nimeuziwa gari lake bila ridhaa yake na anakusaidia kunipeleka polisi kama mwizi wa gari.

Yule mama ana mkataba halisi wa mauziano ya gari yeye akiwa kama shahidi wa mume wake tena muuzaji akiwa ni yule ambaye jina lake lipo kwenye kadi.

Wakubwa nafanyaje kwenye hili? Nimevurugwa kabisa yule dogo aliyeniuzia simpati tena, maza mtu kasema ananipa mwezi mmoja niwe nimeshaamua.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, mwezi wa 6 2022 kuna jamaa aliniuzia gari Mkoa wa Mwanza (Crown 2010). Tukaandikishiana vizuri kabisa nikatoa hela nikapewa kadi, nikakamilisha taratibu kama bima nk sikuweza badirisha umiliki
Pole sana mzee, hapo ushauri wangu jihami mapema kwa kuripoti polisi, wapelekee maelezo yako..jitahid kila unapowasiliana na huyo maza uwe unamrekodi kama ushahidi, Kajitakase kaka.. kesi ya wizi wa gari sio ndogo
 
Kwa thamani ya hio gari watamgaia zaidi ya 1OM ni bora awahi kuchukua hela kuliko kuja kunyang'anywa kabisa gari.
Hapo akienda sehemu za kueleweka hawawezi kumpa hela maadam kadi haisomi jina lake. Labda aende kwa hawa watu wa mtaani ambako nako msala badae utakuwa mkubwa sababu itaonekana kama umewafanyia makusudi mwishoe mwanze kutafutana kwa nia ya kulipa kisasi.

Any way kama kuna njia ya kisheria ashauriwe vizuri huyu jamaa hasa pale kwenye ushahidi wa huyu mama ambae sasa amegeuka.
 
Utaibaje gari na kadi yake.! Wao ndo waelewane huko kwenye vikao vyao, siifahamu sheria lakini naamini inaweza kukubeba.

Hata yeye anaweza kuwa tapeli pia kwa kumtuma mtoto auze kisha waidai tena.

Waone wataalamu wa sheria nafikiri mfano wa issue yako sio mpya
 
Kalikopee mkopo kwwa wale jamaa wa mwezi mmoja, weka bondi ndinga upoze machungu.
Kwa kadi ambayo haina jina langu?
Aliekuuzia anasemaje?
Hana cha kusema yeye anadai maza wake alimpa lote lote ndo maana hata kadi alikuwa nayo so anashangaa maza imekuwaje anakua hivi, ila saa hizi huyo dogo hapatikani kabisa.
 
Hiyo pata potea! Busara nikumtafuta huyo maza ukae nae chini nayeye ni binadamu anajua maumivu ya pesa labda umpooze mmalizane ila zikitumika hasira yeye akasirike na wewe ukasirike mtafika mbali bila faida zozote au uamue kulipotezea tu kama sadaka ya kujimaliza pale kawe

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimejaribu kufanya hivi ila bi maza anachotaka ni gari lake na anadai atatuweka ndani mimi na mpuuzi mwenzangu(mwanae) nimepewa hadi December niwe nimerudisha gari la watu halafu nihangaike kutafuta hela zangu....kiukweli hapo sijui inakuwaje
 
Haya maelezo ulifanikiw kuyarekodi

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
Sikuona umuhimu maana mkataba wa maudhiano upo tena tulipitia ofisi ya mwenyekti wa mtaani kwao dogo, sikuwa na shaka maana ni mkazi wa huo mtaa na gari amekua akilitumia yeye tangu 2017 mzee wao alipofariki, baada ya kufariki nyumba na gari vya Mwanza alibaki navyo dogo mama yao akaenda Kuishi ARUSHA (Haya ni maelezo ya ufupi kutoka kwa majiriani wa mtaa baada ya kupeleleza kidogo)
 
Back
Top Bottom