Nimeuziwa gari la urithi bila kuelewa, najinasuaje huu msala

Nimejaribu kufanya hivi ila bi maza anachotaka ni gari lake na anadai atatuweka ndani mimi na mpuuzi mwenzangu(mwanae) nimepewa hadi December niwe nimerudisha gari la watu halafu nihangaike kutafuta hela zangu....kiukweli hapo sijui inakuwaje
Eh! Kama ndivyo ni mtihani! Ila mfuatilie kama ni mkristo fahamu ana ishi wapi au ana sali wapi kakae chini na kiongozi wake wa imani anaweza kulainisha hiyo roho ya huyo maza, vyivyo hivyo kama ni muislam nadhani itakua njia rahisi na nzuri kuliko kuja kukamatwa na kidhibiti atakupotezea muda na pesa zaidi ya ulizotumia na muda ambao ungeendelea na ishu zingine utakua ndani ukingojea wakuja kukudhamini, hao viongozi wa imani watakua rahisi kidogo na watakua na ushauri mzuri zaidi kabla hamjaenda mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kutakatisha huo ununuzi. Kimaingi hakuuza gari ila alikutapeli. Chakufanya ili kutakatisha wewe mwite huyo jamaa, aliyekuuzia, pia na warithi wote mjadili pamoja na kufikia mardhiano. Mnaandika Kwa wanasheria, thereafter,. Lengo ni kuonyesha kuwa umenunua Kwa warithi wote. Baada ya hapo utabadili jina blue card kuja kwenye jina lako. Utakuwa umetakatisha ununuzi. On the contrary gari siyo lako Hilo muda wowote watakuja kuchukua wenye nalo.
 
Kalikopee mkopo kwa wale jamaa wa mwezi mmoja, weka bondi ndinga upoze machungu.
Hakuna mkopeshaji mjinga atakayekubali kupokea gari ambalo jina la kadi na jina la mkopaji ni vitu viwili tofauti.
 
Sio kesi sana, wengi wanakuwa wanajiaminu wakikaa na gari.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, mwezi wa 6, 2022 kuna jamaa aliniuzia gari Mkoa wa Mwanza (Crown 2010). Tukaandikishiana vizuri kabisa nikatoa hela nikapewa kadi, nikakamilisha taratibu kama bima nk sikuweza badilisha umiliki sababu ya kukosa nakala halisi za jina la mwenye kadi.

Basi katika kuvimba nalo mjini nashangaa juzi napigiwa simu na bi maza anayedai yeye ndo msimamizi wa mirathi nimeuziwa gari lake bila ridhaa yake na anakusaidia kunipeleka polisi kama mwizi wa gari.

Yule mama ana mkataba halisi wa mauziano ya gari yeye akiwa kama shahidi wa mume wake tena muuzaji akiwa ni yule ambaye jina lake lipo kwenye kadi.

Wakubwa nafanyaje kwenye hili? Nimevurugwa kabisa yule dogo aliyeniuzia simpati tena, maza mtu kasema ananipa mwezi mmoja niwe nimeshaamua.
KAMA.UPO.MWANZA NITAFUTE... kesi inazimika ndani ya siku 7 na huyo mama atakukabidhi document mwenyewe
 
Kwa kadi ambayo haina jina langu?

Hana cha kusema yeye anadai maza wake alimpa lote lote ndo maana hata kadi alikuwa nayo so anashangaa maza imekuwaje anakua hivi, ila saa hizi huyo dogo hapatikani kabisa.
Mpange kuwa hujabadili jina. .. Inawezekana.

Kikubwa mazungumzo yoote ya maza na mwanae uwe unarekodi kama ushahidi.

Huenda mama alimpa kweli gari mwanae, ila hajafurahishwa na kuuzwa kwake, ukizingatia kadi ina jina lake kaamua kuleta ngolowanje.
 
Kwa kadi ambayo haina jina langu?

Hana cha kusema yeye anadai maza wake alimpa lote lote ndo maana hata kadi alikuwa nayo so anashangaa maza imekuwaje anakua hivi, ila saa hizi huyo dogo hapatikani kabisa.
Ni kamchezo kao we sio wa kwanza kuuziwa hiyo gari insvyoonekana
 
Hakuna namna naweza shinda kama tukienda mahakamani? Nina mpango afungue tu kesi afu tukutane mahakamani ila wasiwasi wangu ni uhakika wa kushinda kesi.
Unashinda asubuhi tena tutawafungulia na kesi ya uhujumu uchumi na wizi
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, mwezi wa 6, 2022 kuna jamaa aliniuzia gari Mkoa wa Mwanza (Crown 2010). Tukaandikishiana vizuri kabisa nikatoa hela nikapewa kadi, nikakamilisha taratibu kama bima nk sikuweza badilisha umiliki sababu ya kukosa nakala halisi za jina la mwenye kadi.

Basi katika kuvimba nalo mjini nashangaa juzi napigiwa simu na bi maza anayedai yeye ndo msimamizi wa mirathi nimeuziwa gari lake bila ridhaa yake na anakusaidia kunipeleka polisi kama mwizi wa gari.

Yule mama ana mkataba halisi wa mauziano ya gari yeye akiwa kama shahidi wa mume wake tena muuzaji akiwa ni yule ambaye jina lake lipo kwenye kadi.

Wakubwa nafanyaje kwenye hili? Nimevurugwa kabisa yule dogo aliyeniuzia simpati tena, maza mtu kasema ananipa mwezi mmoja niwe nimeshaamua.
Mm mwenyew nimewai uziwa la marehemu aise wale vijan sijui waliliiba vip na had kad na makbesha zote za kutoa bandarini Wakanipa

Mim nikabaki na gari nikasema siku moja nikipta Muda nitaenda kubadli siku moja tra wakalidaka wakapeleka yad Yao Happ singida mm nikijuwa Nina nakala halisi ebwana eeh kumbe gari iliibiwa Zanzibar na kuletwa huku kinyemela na Kisha kuzwaa jmn sintamsahau jamaa aliye niuzia anaitwa nusweee na mwenye gari Ni rajabu wa malindi hukoo Zanzibar

Jmn daah kidgo niarishe mbele ya jopo la uchunguzi ila nilikuja kushinda kesi hyo na kupewa gari langu leo hi imeuwa injini sina hamu nalo
 
UMETAPELIWA.
MTAFUTE ALIYEKUUZIA UMSHTAKI POLISI KWA JESI YA WIZI WA KUAMINIWA.
Lakini na wewe ni mzembe, unauziwaje gari yenye jina la mtu mwingine na hujapewa vielelezo vya original owner ambaye jina lipo kwenye kadi?

UMETAPELIWA, rudisha gari ya watu kisha mtafute tapeli wako
 
Mbona kawaida sio mara ya kwanza nanunua gari kwa mtindo huu
 
Mm mwenyew nimewai uziwa la marehemu aise wale vijan sijui waliliiba vip na had kad na makbesha zote za kutoa bandarini Wakanipa

Mim nikabaki na gari nikasema siku moja nikipta Muda nitaenda kubadli siku moja tra wakalidaka wakapeleka yad Yao Happ singida mm nikijuwa Nina nakala halisi ebwana eeh kumbe gari iliibiwa Zanzibar na kuletwa huku kinyemela na Kisha kuzwaa jmn sintamsahau jamaa aliye niuzia anaitwa nusweee na mwenye gari Ni rajabu wa malindi hukoo Zanzibar

Jmn daah kidgo niarishe mbele ya jopo la uchunguzi ila nilikuja kushinda kesi hyo na kupewa gari langu leo hi imeuwa injini sina hamu nalo
Pole sana kwa hiyo ulimuachia MUNGU au mlimalizana kinyumbani?
 
Back
Top Bottom