Leo nimefika kituo cha polizi X nikakutana na OCCID ambaye ni jamaa yangu anaitwa J alichoniambia ni hivi " kama itathibitishwa huyo mama kweli ameidhinishwa na mahakama kama msimamizi wa mirathi basi aliyenitapeli sio mwenye mali(Ni mwizi ambaye kaiba gari mama yake na kuliuza) ,Ni kama kununua Fridge au TV iliyoibwa, kama huyo mama atafungua kesi lazima nikamatwe alafu gari walizuie (seize) kisha nifikishwe mahakaman kama mwizi wa gari( hiyo ya kwamba nimemenunua itakua ni utetezi wangu ila mahakaman ntafikishwa kama mwizi, mahakama itataka kuthibitisha kuwa mm sio mwizi kwa kutoa vielelezo kama kadi ya gari (kadi ikiwa haina jina langu itabidi nitafute shahidi mwenye kadi original anitetee kuwa aliniuzia mimi ama nipeleke kielelezo cha kununua toka kwa mwenye gari kitu ambacho sina) kwa lugha nyepesi siwezi kuishawishi mahakama kuwa gari ni langu hvyo naweza tia hatiani kwa wizi na kutokana na kesi ilivyo naweza lipa fidia na kurudisha gari , kufungwa sio sana utetezi unaweza nibeba sababu ya mtoto wa complainant. Mimi na Dogo wote tuna kesi ya kuiba gari la watu".
"Pia kama ntafungua kutapeliwa inatakiwa nionyeshe aliyenitapeli ni mwenye gari, Awe huyo mama sasa ama sivyo gari litazuiwa na atapewa muhusika afu mm ntapewa RB ya kumtafuta Tapeli" pia hata ikiwa ni wizi wa Kuaminika bado aliyenipigia simu sio aliyeingia makubaliano na mmi"
Haya ni maelezo ya bwana afande manyota