InvisibleTarget
JF-Expert Member
- Dec 20, 2014
- 1,138
- 2,176
huyo mama kipindi chote alikuwa wapi ?kuna dalili ya watu kula deal hapo, iweje mtu auze gari halafu kadi OG awe bado anayo au hawakumaliza deni na kama hawakumaliza deni kadi ilibidi iwe kwa Wakili, aliipateje ?....Fanya hivi, likongoroe gari lote uza spear kisha kachukue lost report ukipenda vinginevyo wakija waambie sina gari na sijawahi kununua hilo gari sababu kuna dalili za kuanza usumbufu usiokuwa na msingi utakaokupotezea muda na gharama zako...bora hasara kidogo.
Niende moja kwa moja kwenye mada, mwezi wa 6, 2022 kuna jamaa aliniuzia gari Mkoa wa Mwanza (Crown 2010). Tukaandikishiana vizuri kabisa nikatoa hela nikapewa kadi, nikakamilisha taratibu kama bima nk sikuweza badilisha umiliki sababu ya kukosa nakala halisi za jina la mwenye kadi.
Basi katika kuvimba nalo mjini nashangaa juzi napigiwa simu na bi maza anayedai yeye ndo msimamizi wa mirathi nimeuziwa gari lake bila ridhaa yake na anakusaidia kunipeleka polisi kama mwizi wa gari.
Yule mama ana mkataba halisi wa mauziano ya gari yeye akiwa kama shahidi wa mume wake tena muuzaji akiwa ni yule ambaye jina lake lipo kwenye kadi.
Wakubwa nafanyaje kwenye hili? Nimevurugwa kabisa yule dogo aliyeniuzia simpati tena, maza mtu kasema ananipa mwezi mmoja niwe nimeshaamua.