Nimevunja uchumba sababu ya Majina ya Watoto na gharama za harusi

Nimevunja uchumba sababu ya Majina ya Watoto na gharama za harusi

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Nimendika baada ya kuona post kama hii ila ina utofauti kidogo.
Kwa upande wangu hii ilinitokea Mwakajana ambapo kuna dem nilimuweka target nikasema huyu anaweza kuwa mke kwa mvuo wake, maana binafsi ninajali sana hisia zangu na ninajua mizigo inayo niwehusha. Basi huyu alikua anakaba engo nyingi.

Shida ilianzia kwenye kujadili mambo ya harusi. Dem akataka ifanyike bonge la harusi ya gharama ya kufa mtu. Kuanzia kadi za kifahari mpaka fungate akawa anapendekeza Hoteli ambazo hata getini sijawahi waza kufika. Kidume nikawa naitikia tu huku naandika kwenye page flai kichwani.

Siku moja nikatoa msimamo wangu juu ya aina ya harusi ninayoitaka, nikamwambia kwake nahitaji ndoa sio harusi. Mimi nilitaka ifungwe ndoa kisha mambo yaishie hapo au kuwe na tafrija ya kawaida kumkaribisha mwali katika familia na maisha mengine yaendelee. Lakini dem aling'aka na kuzua ubishi mkubwa na kutoa amri badala ya kushawishi na kuweka maoni yake kwa hekima. Niliaendelea kuandika kwa page yangu kichwani.

Siku zikasonga huku nikiangalia kama atalegeza msimamo wake, siku moja tukawa tunajadili majina ya watoto. nikamwambia mimi wanangu wataitwa majina ya kiafrika au Majina ya ukoo wetu na ndio taraibu zetu hasa kwa mtoto wa kwanza na hata hao wengine unawapa majina ya asili kisha baade unaweza kuaongeza hilo la kizungu kama kujifuraisha maana hata mimi sina jina la kizungu wala kiarabu. Hapa sasa dem alivurumisha maneno mazito na kusema jina la mama yangu ni lakishamba. Anataka watoto waitwe akina Oprah, Precious, Candy, Chrisbrown na mengine kama hayo.
Kwakweli kuanzia hapo nikaanza kukanyaga breki ili nimuache aendelee na safari.

Mpaka leo Mwakampya tayari uchumba ni rasmi umesha kufa.
Happy new year.
 
Humu ni JF au unataka wasio julikana waninyonyoe?

Kwa taarifa yako, humu mnamojificha ndimo mnaonyesha tabia halisi kuanzia jina utalotumia! Kama ni mjivuni tunakuona, kama mzungu tushakuona kuanzia jina, huyo binti umempa lawama za bure tu.

Huwezi kujificha kwenye jina la Justine then useme wewe ni mswahili pure 😂😂😂😂
 
Duh, muwowaji hapa hakuna.....! Utaacha Wengi iwapo hata vi 'issue' vidogo vidogo ivi vinakutoa jasho unashindwa kuvitatua.
 
Huoni raha kuitwa baba chirs brown [emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16] utawaona akina Drake... future...Yan uchoke weww

kelphin kepph
 
Eeeh Mungu tusaidie na haya mafurushi. Kwani akili ulisahau kuwapa hawa wa sasa hivi au?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Ukiwa tayari kuoa jaribu tena kutafuta mchumba, kwa sasa fanya mambo mengine.
 
Back
Top Bottom