LGE2024 Nimevunjika moyo na uchaguzi huu wa leo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hawa watu wanacheza sana na akili zetu. Of course, wanajua bado tumelala, lakini siku watakayojichanganya wakamkuta tumeamka watakiona kilichomtoa nyoka pangoni.
 
Hawa watu wanacheza sana na akili zetu. Of course, wanajua bado tumelala, lakini siku watakayojichanganya wakamkuta tumeamka watakiona kilichomtoa nyoka pangoni.
Ni kweli mzalendo ,hivi kupiga kura mwisho ni saa ngapi mkuu na matokeo yatatangazwa saa ngapi ?
 
Kwahiyo maslahi mapana ya taifa ni pamoja na kuiba kura ?kupiga watu risasi na kuweka mapingamizi ya kinguruwe?
Kama kweli CCM imejipanga kama unavyodai mnaogopa nn hadi kura zipigwe nje ya vituo na ujinga mwingine
Gentleman,
risasi hadi huko America zimerindima sana na hukuna alievuna huruma kwenye hilo jambo la kawaida kabisa maeneo mbalimbali duniani..

dhana ya kuibiwa kura ni kisingizio kisicho na maana yoyote, cha miaka nenda miaka rudi.
Ni mtu mwenye akili za kinyumbu pekee ndio kazi yake ni kuibiwa tu, tena anaibiwa kitu asichokua nacho. Huu ni unyumbu wa kuwango kibaya zaidi.

CCM imejipanga na ndio maana mwaka huu na mwaka ujao mtaisoma namba gentleman,

na mtaishia kumbwelambwela hivi hivi huku CCM ikiendelea kutawala na kuwapelekea wananch maendeleo..🐒
 
Unasumbuliwa na ujinga wa kihalaiki. Kama marekani waliuana Tanzania pia kuuana ni sahihi? Sasa hiyo amani mnayohubiri ni ipi?
Marekani wanaruhusu USHOGA kwa hiyo na sisi turuhusu kwasababu ni jambo dogo?
Marekani silaha zinauzwa supermarkets na sisi kama Tanzania tuanze kuuza silaha kwa kila mtu?
 
Wewe uliamini kuna uchaguzi?

Huo ulikuwa ni upotezaji wa rasilimali muda na fedha kwenda kushiriki ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura .

CCM kama ilivyo jina lake itatoka tu kwa mapinduzi na sio sanduku la kura.

Cc Tindo
Kama kuna mtu anaamini ccm itatoka madarakani kwa box la kura anajidanganya. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio njia pekee.
 
Mtaani kwetu raia wamegoma kupiga kura wanapita kuwatangazia watu wakapige kura. CCM na TAMISEMI yao ni hovyo sana utalazimisha vipi watu wameshakuchoka ? Kaa pembeni jifunzeni kutoka kwa wenzako.
Mimi nipo na masela hapa geto tangu asubuhi., saiv tumepiga ugali mkubwa na kitimoto, maini na kachumbali tunapiga mitungi mdogo mdogo kuangalia game ya simba then tupange tunaingia kiwanja gani kumalizia siku. Hakuna hata mmoja mwenye habari na uchaguzi
 
Uchafu uendelee kuzidi/ kurundikana ili muda wa kuuondoa utimie kwa wepesi.
 
block takataka hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…