Nimewasikiliza wabunge wa CHADEMA waliohojiwa na PCCB, yawezekana Lijualikali ni mwongo wa "Kutupwa"

Nimewasikiliza wabunge wa CHADEMA waliohojiwa na PCCB, yawezekana Lijualikali ni mwongo wa "Kutupwa"

Nimwwasikiliza wabunge wote wa Chadema waliohojiwa na vyombo vya habari baada ya kutoka kwenye mahojiano na maofisa wa Takukuru.

Kwanza nilimsikiliza Lijualikali aliyedai wabunge wa Chadema wamepanga njama za kuidanganya Takukuru.
Nikakaa mkao wa kuwasikiliza wabunge wengine ili nibaini hizo njama.

Nilichogundua baada ya kuwasikiliza ni kweli wabunge wamekiri kukatwa fedha zao kwa ajili ya ujenzi wa chama na hiyo ni kwa mujibu wa katiba ya Chadema

Pili, makato hayo hukatwa na ofisi ya bunge chini ya Baraka za mh Spika na kuwasilishwa kwa Katibu mkuu wa Chadema.

Tatu, matumizi ya chama husimamiwa na Katibu mkuu na fedha za chama hutunzwa na mhasibu mkuu wakati matumizi ya chama huamuliwa na kupitishwa na kamati kuu ya chama.
Suzan Lyimo kwa mfano alishangaa wao kuulizwa maswali yaliyopaswa kuelekezwa kwa mhasibu kwani wao kama wabunge katiba inawataka kuchangia ujenzi wa chama siyo kupanga matumizi.
Suzan Kiwanga amedai makato yao hubsrikiwa na mh Spika.

Naye mbunge Pareso anasema kanuni ya makato huelezwa kuanzia day one unapojaza fomu ya maombi ya ubunge hivyo ni uamuzi wako kama hutaki usigombee.

Katika mazingira haya ni wazi makato ya wabunge wa Chadema yako kikatiba na matumizi yake huidhinishwa na kamati kuu ya chama.
Labda ndio maana CAG aliwapa hati inayoridhisha

Nimalizie kwa kusema fedha yoyote ya taasisi huweza kubadilishiwa matumizi na hiyo siyo dhambi ndio maana hata fedha za bajeti zikifika serikalini zinaweza kubafilishiwa matumizi kwa nia njema tu ya kuleta maendeleo kwa haraka.

Nawatakia Dominica yenye baraka

Maendeleo hayana vyama!
Nilisha sema huyu mbwana mdogo anaenda pigwa anguko kubwa kisiasa ,
Mkuu wangu .Faifa linakosa watu hasa vijana wanao shindwa kusimamia ukweli,why ?kuama Chama sio tatizo ila simamia ukweli ,sasa hasubili kama hatapotea kisiasa
 
Unafikiri wakati ukifika TAKUKURU hawatampeleka Mbowe mahakamani? Hapa mtuhumiwa ni Mwenyekiti na siyo chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko anaenda kuwavua nguo bora waishie kwenye uchunguzi wapige kimya! Kitu kiko kwenye katiba ambayo hata msajili wa vyama alishaiidhinisha! Juzi nikalisikia lile taahira la Kongwa eti linamwambia waziri afuate hela ya kodi kwa CHADEMA, ama kweli viwavi jeshi vinaathiri hadi ubongo!
 
Hapana kuna tuhuma ni nyingi. Moja ni mwenyekiti kulazimisha kulipwa deni hewa zaidi ya bil 6 kwa miaka mitano.
Pili kuna fedha ambazo wabunge walikatwa kwa ajili ya uchaguzi.Na ziliwekwa kwenye fixed. Uchaguzi umekaribia hazijulikani zimepotea vipi.
Mosi dawa ya deni ni kulipa kama Mbowe anadai ni haki yake kulipwa.

Pili, mbunge akishakatwa ile fedha ni ya chama na kinaweza kutumia kwa kadri kinavyoona inafaa.

Wafanyakazi wanakatwa Nssf lakini matumizi ya kujenga daraja ka kigamboni yalifanywa na Bodi ya Nssf, huo ni mfano tu!
 
Mfano wa Nssf na pesa ya chama kwa akaunti maalumu ya uchaguzi haviendani
Pili deni lenyewe chama kilikopeshwa kwa mdomo kimabavu. Hii ni kwa mujibu wa Waitara. Ni deni hewa tu alilojitengenezea mwenyekiti. Hapa kuna mtu laziima aibike japokuwa alifanya maigizo.
 
Nyinyi watetezi wa chadema mnajitetea sana kwenye tope la tuhuma nzito.

Chama cha demokrasia na maendeleo kinachowatoza kodi viongozi wote kwa mgongo wa katiba ya chama, ambayo ni mbovu.

Suala la lijuakali sio michango.
Wala sio uhalali wa michango.
Huu ni upotoshaji.

Juakali anapinga matumizi ya fedha zinazokatwa kutoka kwa wabunge.

TAKUKURU haiwahoji wabunge kuhusu matumizi ya fedha. Bali inawahoji ili kujiridhisha kama kweli walichangishwa fedha hizo na hapo sasa.

MUZIKI halisi utaanzia kwenye ukaguzi wa matumizi ya halali fedha hizo,kama chama kinachopewa ruzuku ya serikali na ambayo ni fedha ya walipakodi wa nchi hii.
Hapo ndio jinai inapoweza kupatikana, jinai haiwezi kupatikana midomoni bali kwenye Documents za halali za orodha ya matumizi ya CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO,
CHADEMA.na hili ndio haswa linalomfanya mwamba apige Faru john.
Mpaka kuanguka chakali.

Msijipe moyo mapema, mwenye album hii ni Mh mbowe mwenyewe sio nyinyi PUPPETS.
Upuuzi mtupu!

TAKUKURU hawana weledi kwenye masuala ya fedha kumzidi CAG. Kunapokuwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, ofisi ya CAG ndiyo chombo sahihi cha kuchunguza.

Matumizi mabaya ya fedha hayachunguzwi na TAKUKURU. TAKUKURU ni chombo cha kuchunguza rushwa. Kwa hiyo fedha iliyokuwa inachangwa na wabunge wa CHADEMA ilikuwa inatumika kutoa rushwa kwa nani?

TAKUKURU wangekuwa na akili, weledi na uadilifu wa kazi yao, walistahili kuichunguza CCM kuhusu tuhuma za kununua na kuwahonga wabunge wa vyama vya upinzani ili waunge mkono juhudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mbo
Sijui huelewi Nini? Kwa akili yako unaona kubadilisha matumizi siyo kula hela? Unaona ni sawa fedha za kusaidia wagombea kwenye kampeni zikabadilishwa matumizi na zikatumika na mwenyekiti kunywea pombe na kuhudumia nyumba zake ndogo huko siyo kula hela? Ataeleza Sasa alizitumiaje 8.9 billion.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mbona mnashindwa kujibu hoja ,hivi mfano ukichangia harusi kamati si ndo huwa wanaona sehem yenye mapungufu na kulekebisha ,sasa mtu eti anahoji makato ya Chama Leo kisa kahama Chama
na wakati alijua makato yapo kikatiba ,mliohama japo ni haki yenu kikatiba but jifunze kutoka kwa RWAKATARE.Mbeleko hipo siku ukatika ipo siku mtajuta
 
Mfano wa Nssf na pesa ya chama kwa akaunti maalumu ya uchaguzi haviendani
Pili deni lenyewe chama kilikopeshwa kwa mdomo kimabavu. Hii ni kwa mujibu wa Waitara. Ni deni hewa tu alilojitengenezea mwenyekiti. Hapa kuna mtu laziima aibike japokuwa alifanya maigizo.
Kama ingekuwa ni account maalumu ya wabunge basi hiyo michango angekabidhiwa David Silinde na siyo Dr Mashinji

Mkataba unaweza kuingiwa kwa njia ya mdomo au maandishi haitajiki mwanasheria kulijua hili!
 
Kulikuwa hakuna mkataba,bali aliibua deni hewa baada ya uchaguzi.Kuwa aliuza maghorofa yake kwa ajili ya chama.
Hiyo ni account maalumu ya chama kwa ajili ya uchaguzi. Ndio maana ikawa fixed. Chama ni mali ya umma sio ya wabunge,kumbuka.
 
Na ruzuku ndio mali ya umma siyo michango.

Hili hata Wakili Msando analielewa vizuri!
 
Wabunge wa Chadema ni wajumbe wa kamati kuu hivyo kama kuna matumizi mabaya ni wao waliruhusu.

Lakini CAG alishatoa hati safi......hakuna kesi hapo!
CAG aliyepita aliwahi kutoa hati safi katika ubarozi wa tz lakini wakarudi aikaonekana kuna matumizi mabaya huko wakamuita barozi na kumua ubarozi
 
Juakali hakulalamika juu ya makato ya fedha kwani hilo swala lipo ndani ya katiba bali alicholalamika ni kubadirishwa matumizi ya hayo makato ikiwemo mwenyekiti kujikopesha na mpaka sasa chama hakina fedha ni vyema tusiwe na haraka kwani zote ni tuhuma tusubiri takukuru wamalize uchunguzi mbivu na mbichi zitajulikana
Weka wazi wewe unamuamini nani?? Lijuakali na kundi lake akiwemo Spika unafiki wao uko wazi malengo yao yako wazi. Walilenga kumchafua na kumdhalilisha Mh Mbowe na siyo eti wana uchungu na fedha za Chadema.

Katiba ya chama iko wazi sera za chama ziko wazi. Kwanini wanaolalamika iwe sasa?? Kama siyo Chadema asingejulikana leo.

Na wote wanaobeza Chadema wajiulize kama siyo uimara na umakini wa Chadema Mh Makufuli angepitishwa na ccm kuwa mgombea wake 2015?? Waaoshindwa kulitambua hilo basi hawana tofauti na Lijuakali.
 
Hapa tunamzungumzia CPA Charles Kichere siyo yule mwalimu!

Na ndio maana lijualikali alisema CAG hawezi kujua katiba ya chadema, hivyo Takukuru wao wanaenda kuona miongozo kama ilifuatwa, pia wabunge wengi na baadhi ya wajumbe wa hizo kamati wanasema hakuna vikao vilivyopitisha hiyo pesa na ndo maana wakiuliza wanaitwa wasaliti, kwa hiyo tusubiri majibu ya Takukuru mengine hapa tutajadili uongo
 
Weka wazi wewe unamuamini nani?? Lijuakali na kundi lake akiwemo Spika unafiki wao uko wazi malengo yao yako wazi. Walilenga kumchafua na kumdhalilisha Mh Mbowe na siyo eti wana uchungu na fedha za Chadema.

Katiba ya chama iko wazi sera za chama ziko wazi. Kwanini wanaolalamika iwe sasa?? Kama siyo Chadema asingejulikana leo.

Na wote wanaobeza Chadema wajiulize kama siyo uimara na umakini wa Chadema Mh Makufuli angepitishwa na ccm kuwa mgombea wake 2015?? Waaoshindwa kulitambua hilo basi hawana tofauti na Lijuakali.
Nimekuelewa bwashee!
 
Mwenyekiti alijikopesha kwani hiyo michango anakusanya yeye?

Lijualikali apambane na CC ya Chadema!
Ningekuwa na nafasi ya kushauri ndani ya ccm ningependekeza wakupe hata Ukatibu mkuu au uenezi maana unauwezo mkubwa kuliko Dr Bashiru au Polepole. Halafu baadae unampata mwenyekiti kama Membe hivi hakika mngefika mbali na kuheshimika
 
Back
Top Bottom