Nimewasikiliza wabunge wa CHADEMA waliohojiwa na PCCB, yawezekana Lijualikali ni mwongo wa "Kutupwa"

Na ndio maana lijualikali alisema CAG hawezi kujua katiba ya chadema, hivyo Takukuru wao wanaenda kuona miongozo kama ilifuatwa, pia wabunge wengi na baadhi ya wajumbe wa hizo kamati wanasema hakuna vikao vilivyopitisha hiyo pesa na ndo maana wakiuliza wanaitwa wasaliti, kwa hiyo tusubiri majibu ya Takukuru mengine hapa tutajadili uongo
CAG asipojua katiba za vyama atavikaguaje?!

Kwa taarifa yako ukaguzi wa CAG hauishii kwenye fedha pekee, nenda kawaulize MSD watakusimulia vizuri!
 
Ni ujinga uliopitiliza na upuuzi kuhoji watu kitu ambacho kiko kisheria na walikubaliana wenyewe! Hii mijitu inayowahoji inatumia vibaya rasilimali zetu, tuna issue ngapi za rushwa hazijawa solved unakaa unapoteza muda na Chadema wambao walijiwekea utaratibu wao na wakakubaliana kwa kanuni zao? Mambo ya hovyo, sasa ukiwaita unadhani watasema hawakatwi au? Si wangeenda kuangalia form za kupata ubunge wali kubaliana nini! Akili za ajabu sana!
 
Nimwwasikiliza wabunge wote wa Chadema waliohojiwa na vyombo vya habari baada ya kutoka kwenye mahojiano na maofisa wa Takukuru.

Kwanza nilimsikiliza Lijualikali aliyedai wabunge wa Chadema wamepanga njama za kuidanganya Takukuru.
Nikakaa mkao wa kuwasikiliza wabunge wengine ili nibaini hizo njama.

Nilichogundua baada ya kuwasikiliza ni kweli wabunge wamekiri kukatwa fedha zao kwa ajili ya ujenzi wa chama na hiyo ni kwa mujibu wa katiba ya Chadema

Pili, makato hayo hukatwa na ofisi ya bunge chini ya Baraka za mh Spika na kuwasilishwa kwa Katibu mkuu wa Chadema.

Tatu, matumizi ya chama husimamiwa na Katibu mkuu na fedha za chama hutunzwa na mhasibu mkuu wakati matumizi ya chama huamuliwa na kupitishwa na kamati kuu ya chama.
Suzan Lyimo kwa mfano alishangaa wao kuulizwa maswali yaliyopaswa kuelekezwa kwa mhasibu kwani wao kama wabunge katiba inawataka kuchangia ujenzi wa chama siyo kupanga matumizi.
Suzan Kiwanga amedai makato yao hubsrikiwa na mh Spika.

Naye mbunge Pareso anasema kanuni ya makato huelezwa kuanzia day one unapojaza fomu ya maombi ya ubunge hivyo ni uamuzi wako kama hutaki usigombee.

Katika mazingira haya ni wazi makato ya wabunge wa Chadema yako kikatiba na matumizi yake huidhinishwa na kamati kuu ya chama.
Labda ndio maana CAG aliwapa hati inayoridhisha

Nimalizie kwa kusema fedha yoyote ya taasisi huweza kubadilishiwa matumizi na hiyo siyo dhambi ndio maana hata fedha za bajeti zikifika serikalini zinaweza kubafilishiwa matumizi kwa nia njema tu ya kuleta maendeleo kwa haraka.

Nawatakia Dominica yenye baraka

Maendeleo hayana vyama!
Chama cha siasa kinachokata kodi wanachama wake/wabunge wake kwa lazima.
 
Leo ulipata somo gani kanisani.
Naona upo na utulivu, na unajibu kwa upole na point sana.[emoji2]
 
Nitajie wanakokata kodi kwa hiyari!
Muktadha wa hoja yangu unazungumzia kwenye chama wabunge kulazimishwa kukichangia chama kwa lazima wakati huo yale makato hayaonekani yanafanya nn, wakati nikiwa mwanachama wa Mawakili Tanganyika Zamani nikiwa Tanzania, mimi na wenzangu tulikuja na hoja ya kuchangishwa elfu50 kila wakati wa kulipa ada za TLS kwa ajili ya wakili house, ambapo hyo hela iliyokuwa inachangwa ikawa haionekani.
 
Leo ulipata somo gani kanisani.
Naona upo na utulivu, na unajibu kwa upole na point sana.[emoji2]
Hahahaaaa....... Lijualikali anataka kujipatia umaarugu wa bure wakati amekiri kabisa yeye na Lowassa waliiba kura uchaguzi mkuu 2015.

Watu wa aina hii ni hatari sana kwenye chama " kinachoongoza" nchi bwashee!
 
Muktadha wa hoja yangu unazungumzia kwenye chama wabunge kulazimishwa kukichangia chama kwa lazima wakati huo yale makato hayaonekani yanafanya nn, wakati nikiwa mwanachama wa Mawakili Tanganyika Zamani nikiwa Tanzania, mimi na wenzangu tulikuja na hoja ya kuchangishwa elfu50 kila wakati wa kulipa ada za TLS kwa ajili ya wakili house, ambapo hyo hela iliyokuwa inachangwa ikawa haionekani.
Bwashee, huu mchango wa wabunge wa Chadema uko kwenye katiba yao.

Hakuna anayekulazimisha maana vyama vya siasa viko vingi unaweza kwenda TLP kule ni bure kila kitu.
 
Hahahaaaa....... Lijualikali anataka kujipatia umaarugu wa bure wakati amekiri kabisa yeye na Lowassa waliiba kura uchaguzi mkuu 2015.

Watu wa aina hii ni hatari sana kwenye chama " kinachoongoza" nchi bwashee!
Kwa kweli kama alikua na nia ya kuhama CHADEMA angehama tu kistaarabu ama kimya kimya. Sidhani kwa mapovu aliyotoa hata huko alikopokelewa watamuamini

Lijuakali ni hopeless kabisa.
 
Muktadha wa hoja yangu unazungumzia kwenye chama wabunge kulazimishwa kukichangia chama kwa lazima wakati huo yale makato hayaonekani yanafanya nn, wakati nikiwa mwanachama wa Mawakili Tanganyika Zamani nikiwa Tanzania, mimi na wenzangu tulikuja na hoja ya kuchangishwa elfu50 kila wakati wa kulipa ada za TLS kwa ajili ya wakili house, ambapo hyo hela iliyokuwa inachangwa ikawa haionekani.
Hivi hata umesoma ulichoandika.

Hayaonekani yanafanya nini? Wewe ni mwanachama wa chadema ?

Si wengeende tu TLPau UDP
 
Back
Top Bottom