Uko sahihi mkuu, Kitaalamu wanashauri kama unataka kufanya huu uwekezaji ni Condition mbili tu:
1. Kuwekeza ili kupata faida, hapa inatakiwa kuweka mpunga mrefu kweli kweli, Inashauriwa ukitaka ufanye uwekezaji wa aina hii bhasi hakikisha walau una vyanzo vya kipato vya uhakika vinavyokulipa vizuri na ambavyo unavyovisimamia vizuri walau vi2,3 na zaidi ...
2. Kutumia hii mifuko kama kibubu na njia ya kustawisha nidhamu yako ya pesa, hapa hata kama bado unajitafuta badala ya kucheza michezo ya mwezi, weka huko, unajifunza kutunza fedha zako mwenyewe. Unabana matumizi yasiyo lazima mf. Soda, Keki, Biskuti, Kubeti, Beer, Unatupia huko, ukipata kafaida asilimia kidogo unatupia huko..
Baada ya miezi 6 hivi utajionea maajabu ya pesa uliyojiwekea, unaweza ukaitoa ukaanzisha mradi, uzuri hii mifuko pesa haikatwi zaidi inapanda, pia huwezi kuitoa mpaka muda uliopanga ufike..
Lakini si lazima uweke pesa huko, Ziko savings account nyingi tu za bank tofauti tofauti, Ni wewe tu uamuzi wako, unapendelea nini .