Nianze kwa kusema Albert Einstein alikua kichwa sana, Maua yake 🌷🌷
Albert Einstein aligundua hii kanuni ya 72 [72 Rule], Hii kanuni inakusaidia kujua iwapo utatumia Muda gani kwa uwekezaji wako kuji double Mara2 kama utatumia njia ya riba mkusanyiko [Compound Interest] .
Kwa lugha nyingine riba mkusanyiko yaani unaiwekeza hela yako bila kutoa, Mwaka ukiisha unaweka tena pesa yote na faida uliyoipata pia, hivyo hivyo miaka na miaka.
Unachukua 72 unagawanya kwa kiwango cha riba unayoitegemea kwa mwaka, Mfano ukiwekeza Milioni 10 vodacom kwa riba ya 13.02% kwa mwaka 👇
View attachment 3159766
Sasa ukataka kujua itakuchukua muda gani ili uwe umepata Milioni10 nyingine, Unachukua 72 gawanya kwa riba unayoipata kwa Mwaka.
72%13.02= 5.6
Kwahiyo ukiiacha hiyo pesa iendelee kujizalisha bila kuitoa itakuchukua Miaka5 na miezi6 kupata Milioni 10 nyingine, Tutumie calculator Tuhakiki;
View attachment 3159772
Hiyo No.6 ni nusu mwaka, Unajionea hayo Maajabu, Tuwekee mfano mwingine unaoendana na UTT.
Tuseme umewekeza Milioni3 UTT kama mdau hapo, japo hajatuambia riba ya sasa ila Tufanye 14% kwa mwaka.
Kwahiyo achukue 72 ➗14=5.1, Unaona hapo, Itamchukua miaka 5 na na mwezi mmoja kupata Milioni 3 nyingine, Na hapo inaweza ikapanda kidogo au kushuka kidogo kulingana na Mtikisiko wa Uchumi.