Nimeweka 3M UTT lakin imeongezeka 360 Nimeshtuka?? watalaam mje mnifafanulie

Nimeweka 3M UTT lakin imeongezeka 360 Nimeshtuka?? watalaam mje mnifafanulie

Ukizungumzia uwekezaji inamaanisha ni mpango wa miaka 10 na kuendelea .

Neno kuwekeza means Long term plan yaani watafaidika mpaka wanao .

Mfano kuna Bro wangu mmoja [Mentor], anafanya uwekezaji wa real estate, amejenga Hoteli mpaka inaanza kufanya kazi ametumia Milioni 430, Kwa mwaka anatarajia kupata return ya 10-15%

Tuseme mfano ingekua kaweka UTT kwabriba ya 13%, Tukitumia hesabu ya Albert Einstein chukua 72 gawanya kwa 13=5.5

Yaani itamchukua miaka 5 na Miezi mitano kurudishia mara2 ya pesa aliyowekeza, ndipo awe na 860M .

Kwahiyo uwekezaji sio kwa ajili yako tu, ni mpaka vizazi vinavyokufuatia .
Hii bado siyo kweli mkuu. Itamchukua miaka 20 ku double investment. Piga hesabu vizuri.
Hotel kwa faida 13% kwa mwaka itamchukua miaka 8 kurudisha mtaji. Na itachukua miaka mingine 8 kupata faida ya 430m. Jumla miaka 16 ku double. Assuming faida ni ile ile y a 13% kwa mwaka, gharama za uendeshaji ziko pale pale na hakuna matengenezo makubwa yamefanyika.
 
Unaomba ufafanuzi baada ya kujiunga kwenye kitu usicho kijua? Kwanini usimgeomba kabla
 
Hii bado siyo kweli mkuu. Itamchukua miaka 20 ku double investment. Piga hesabu vizuri.
Hotel kwa faida 13% kwa mwaka itamchukua miaka 8 kurudisha mtaji. Na itachukua miaka mingine 8 kupata faida ya 430m. Jumla miaka 16 ku double. Assuming faida ni ile ile y a 13% kwa mwaka, gharama za uendeshaji ziko pale pale na hakuna matengenezo makubwa yamefanyika.
Nachoka kabisa
 
wakuu mimi niko Liquid fund .Haya ndo niliyoyaona nimeweka 3M nina wiki na imeongezeka 360 ndo nn yaan mbona haiendani na % nazo calculate

NB: Nyie wa kulike kila comment tafadhari sana Mnisamehe.Nahitaji notification za hoja siyo like! Natafuta maisha jamani tusameheane
Nadhani huwa wanatoa 11%, - 15% depends kwa mwaka Nakupa mfano ukiweka 500,000 Kwa mwaka means mwisho wa mwaka Utakula 50000 Sasa chukua gawia kwa miez 12=Ina Utakuwa unakula 4166.7 Kila mwezi as dividend(kama gawio)

Sasa hiyo M3 yako nakadaria ni 300,000 dividend kwa mwaka Sasa gawia hii 300,000/12=25000 kwa mwezi hilli ndo gawio lako Sasa sjui unapata je mkuu
 
Hii bado siyo kweli mkuu. Itamchukua miaka 20 ku double investment. Piga hesabu vizuri.
Hotel kwa faida 13% kwa mwaka itamchukua miaka 8 kurudisha mtaji. Na itachukua miaka mingine 8 kupata faida ya 430m. Jumla miaka 16 ku double. Assuming faida ni ile ile y a 13% kwa mwaka, gharama za uendeshaji ziko pale pale na hakuna matengenezo makubwa yamefanyika.
RE: Jamaa yangu [My Mentor], kawekeza M430 kwenye RealEstate [hoteli], kumbuka Real Estate [Mf, Hoteli] huwezi kuipigia hesabu ya Compound Interest.

Nikatoa mfano Laiti kama angeamua kusema hizi pesa ngoja niziweke UTT, ndipo nikapiga hiyo hesabu, itamchukua miaka 5.5 kupata Mara2 yake yaani 430M x2 = 860M .

Rudia kusoma post #91
 
Mkataba wa malipo unaendana na muda mliokubaliana, kama ulijaza mkataba wa miezi 6 subili baada ya miezi 6 utapata ulichosign na asilimia zake.

Au tuonyeshe hapa form uliyosign agreement.
 
Mzee umepewa ubalozi kuitangaza hyo utt ama, maana kila siku ni habari hzohzo
 
wakuu mimi niko Liquid fund .Haya ndo niliyoyaona nimeweka 3M nina wiki na imeongezeka 360 ndo nn yaan mbona haiendani na % nazo calculate

NB: Nyie wa kulike kila comment tafadhari sana Mnisamehe.Nahitaji notification za hoja siyo like! Natafuta maisha jamani tusameheane
Nashindwa kuelewa tatizo ni nini kwako!Mbona Mimi nimeweka sh.600000,kwa wiki wananiingizia sh.1300 kwa wiki?
 
wakuu mimi niko Liquid fund .Haya ndo niliyoyaona nimeweka 3M nina wiki na imeongezeka 360 ndo nn yaan mbona haiendani na % nazo calculate

NB: Nyie wa kulike kila comment tafadhari sana Mnisamehe.Nahitaji notification za hoja siyo like! Natafuta maisha jamani tusameheane
Kaka una haraka sana. Anyway kwanza nikutoe wasiwasi UTT sio private company ni serikali hiyo ina zaid ya miaka 20. Wana mtaji zaid ya trilion kwa mifuko yao combined .. sema Wameanza kujitangaza kwa nguvu kwenye miaka ya karibuni.

Pili wanafanya mahesabu ya faida kwa kila siku kasoro weekeend. Ndio maana ukiangalia kuanzia ijumaa
Jioni had jumatatu asubuhi utaona hakuna kinachobadilika..

Kwa pesa ulioweka nikuhakikishie utapata 10% au hata zaidi bila shida kwa mwaka.. na kwa mwez utaona imeongezeka walau 1% ya ulioweka maana yake kwa mwez utacheza kwenye elfu 25+.

Ukinunua Vipande hesabu 48 hrs ndio
Uone vimereflect kwenye account yako na ukiuza pia ni 48 Hrs ndio pesa iingie kwenye account yako

Kuwa na subira, we chukulia
Kama Sehemu ya kujifunza Descipline ya kutunza fedha, kwa maana ya kuwa kama utakuwa na kishida cha kawaida badala ya kukimbilia kutoa fedha bank kwa UTT utabidi usubir 48hrs maana yake hiyo itakupa akili ya kutafuta plan B. Pesa yako Imesalimika
 
Ni fisadi pekee ndiye atakuwa radhi kuwekeza huko.
Fisadi haoni hasara, hata akiweka 100ml baada ya mwaka akapewa 90ml yeye ataona poa tu
Uwekezaji wa 100ml utakupatika kati ya 8ml na 13ml kwa mwaka siyo 90ml.

Huu uwekezaji si wa kila mtu. Ni wa watu ambao hawawezi kufanya vitu vingine kama biashara ambazo zinahitaji uwepo wao.

Tuchukue mfano; ndugu yako amefariki akaacha madogo wa darasa la 6 na 4. Mirathi zao zikawa 200mil. Sasa hawa madogo utawapa hizo hela watafanyia nini?

Ukiziweka UTT mil 100 kwa kila dogo wana uhakika wa kupata mil 2.5 hadi 3 kila baada ya miezi 3 kwa kila dogo. Hiyo ni hela ambayo inaweza kuwasomesha hadi chuo kikuu na bado wakapata mtaji wa kuanzia maisha watakapo maliza vyuo.

Usiseme ni mafisadi ndo wanawekeza huko.
 
Mjadala huu umetoa mwanga kwamba watu wengi hawana Elimu ya uwekezaji na hawajui kitu kinaitwa UTT(Mifuko ya uwekezaji wa pamoja)
Sitaki kusema mambo mengi, wewe binafsi kama mwekezaji mtarajiwa tafuta Elimu juu ya haya masuala. Kwa urahisi ingia YOUTUBE kisha search kwa neno UTT zitakuja video ambazo ukisikiliza zitajibu maswali mengi. UTT ni sehemu salama sana.
 
wakuu mimi niko Liquid fund .Haya ndo niliyoyaona nimeweka 3M nina wiki na imeongezeka 360 ndo nn yaan mbona haiendani na % nazo calculate

NB: Nyie wa kulike kila comment tafadhari sana Mnisamehe.Nahitaji notification za hoja siyo like! Natafuta maisha jamani tusameheane
Pia aliyehudhuria mkutano wa wawekezaji naomba atuambie performance za faida ZA mifuko
 
Back
Top Bottom