Nimeweka 3M UTT lakin imeongezeka 360 Nimeshtuka?? watalaam mje mnifafanulie

poa
 
mtoe uvundo huyo jamaa
 
Muwe mnapata elimu in details kuhusu UTT kabla hamjajiunga..elimu zimetapakaa huko Youtube.
unafikiri sijapata

Ningekua sijapata ningeamua vip maamuzi.
Badala ya kucomment comment hela ungetumia muda huo kutoa ufafanuzi wa kimahesabu kama wewe unajua
 
Ila huu uwekezaji unataka moyo sana au mtu mwenye pesa nyingi au kama una hela unahisi utaiharibu kwa matumizi ambayo hukupanga.

Kuweka milioni tatu nikae mwaka mzima nasubiri laki mbili na ushee inahitaji moyo sana au labda pengine mimi ndio sijaelewa.

Milioni tatu ukiwekeza eneo zuri kwenye biashara return yake ikipungua kwa mwaka ni nzuri kuliko huko.

Niko tayari kurekebishwa.
 
Uko sahihi mkuu, Kitaalamu wanashauri kama unataka kufanya huu uwekezaji ni Condition mbili tu:

1. Kuwekeza ili kupata faida, hapa inatakiwa kuweka mpunga mrefu kweli kweli, Inashauriwa ukitaka ufanye uwekezaji wa aina hii bhasi hakikisha walau una vyanzo vya kipato vya uhakika vinavyokulipa vizuri na ambavyo unavyovisimamia vizuri walau vi2,3 na zaidi ...


2. Kutumia hii mifuko kama kibubu na njia ya kustawisha nidhamu yako ya pesa, hapa hata kama bado unajitafuta badala ya kucheza michezo ya mwezi, weka huko, unajifunza kutunza fedha zako mwenyewe. Unabana matumizi yasiyo lazima mf. Soda, Keki, Biskuti, Kubeti, Beer, Unatupia huko, ukipata kafaida asilimia kidogo unatupia huko..


Baada ya miezi 6 hivi utajionea maajabu ya pesa uliyojiwekea, unaweza ukaitoa ukaanzisha mradi, uzuri hii mifuko pesa haikatwi zaidi inapanda, pia huwezi kuitoa mpaka muda uliopanga ufike..



Lakini si lazima uweke pesa huko, Ziko savings account nyingi tu za bank tofauti tofauti, Ni wewe tu uamuzi wako, unapendelea nini .
 
Mkuu asante sana, nimeelewa vyema sana
 
let say magaiwio yakawa 12%

12% x 3,000,000= 360,000

ni kama lak 3 na 60 siyo laki mbili lakini inategemea na riba yabmwaka huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…