Nimeweka Engine Oil 20w-50 X-trail NT30 (2003) nipo sawa?

clasi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
379
Reaction score
716
Wakuu salama? Nimeweka Engine Oil 20W-50 kwenye X-trail niliyonujua majuzi nipo sawa? Ama nimeingia cha kike?
mileage: 41,000kms

IMG20201230115752.jpg
 
image-2021-01-02-20:59:20-301.jpg

Hata mm nimenunua Hiyo oil kwa ajili ya Rav 4 2006 AKA Miss TZ je nipo sawa
image-2021-01-02-21:00:01-480.jpg

Pia nimenunua Hizi dawa kwa ajili ya kusafisha mfumo wa oil na Kusafisha mfumo wa petroli je nipo sawa au kuna changamoto??
 
Si ungeenda oil station wakakuekea castrol oil tu boss...xtrail haipend kuzingua kwenye oil

Hata alivyonunua hiyo kapata ushauri. So anajaribu kupata maelezo mengine, maana hizi oil zipo nyingi sana na mbaya zaidi zile zikizoandikwa kwenye Vitabu vya gari hazipo huku kwetu ndio maana mada za oil haziishi.

Mfano mm gari yangu inatakiwa oil 0W20 lakini Nchi nzima hii hakuna unahangaika na mafundi wakutajie Equivalent yake Mara uambiwe ni 5W30 mara 20W50 mambo ni mengi
 
Wakuu salama? Nimeweka Engine Oil 20W-50 kwenye X-trail niliyonujua majuzi nipo sawa? Ama nimeingia cha kike?
mileage: 41,000kms
Bora choo cha kike bosi unaweza ukaona hata pichu ya mrembo...

Gari yenye mileage ya km 41k bado ni bikira kabisaa....
SAE VISCOSITY ya hiyo gari ni 5w30 au 10w30....

Hiyo 20w50 ni oil nzito sana mkuu..utachosha engine soon...hiyo ni special for high mileage engines na malori..
 
Si ungeenda oil station wakakuekea castrol oil tu boss...xtrail haipend kuzingua kwenye oil
Castrol,Toal, Oryx na nyinginezo zoooote, usipofuata specifications za gari lako utapigwa tu...

Wakati wa kuchagua oil, unaangalia viscosity inayopendekezwa kwa gari lako, kisha brand ya oil inafuata baadae..

Lakini kibongo bongo mtu akiona tu dumu limeandikwa Castrol, anaweka tu kwenye injini bila kujua kuwa Castrol zina namba tofauti kulingana na specifications za engine
 
Mkuu nimeona mambo ya 20w50 kwenye xtrail hapo...
Inaonekana watu si wapekuzi wa nyuzi za nyuma...suala la oil limejadiliwa sana huku...
Japo ninatamani niandike uzi special wa matumizi ya oil..
Daah aisee mkuu kesho hapa watakuja kulalamika oooh nissan hua zinazingua sijui nini,ile thread yako khs Nissan inajibu mengi sana khs mambo mengi sana + threads nyingine za wadau sema kama kawaida yetu hatupendi kujisomea somea.

Ukipata muda andika tu mkuu khs matumizi ya oil unaweza kusaidia watu wengi sana,tofauti na sasa ambapo watu wanapeleka gari kwa mafundi huku wakitegema fundi ndio awape ushauri na fundi mwenyewe ni wa chini ya mti hajui tech. ya kisasa ya magari inaendaje.
 
View attachment 1665912

Hata mm nimenunua Hiyo oil kwa ajili ya Rav 4 2006 AKA Miss TZ je nipo sawa
View attachment 1665913

Pia nimenunua Hizi dawa kwa ajili ya kusafisha mfumo wa oil na Kusafisha mfumo wa petroli je nipo sawa au kuna changamoto??
Wewe na huyo wa Xtrail wote mpo nia moja....Gari zetu nyingi haswa za petrol za miaka ya 2000 kuja juu, nyingi SAE VISCOSITY ni 5w30 au 10w30.

Kuhusu hizo dawa, hiyo ya kusafisha injectors wanashauri uweke kichupa kimuja kwa kila lita 50 za petrol....niliwahi kuifuatilia revies zake mitandao ya nje, wengi walisema wameona matokeo mazuri..

Hiyo injini oil flush sina info zaidi..

Ushauri kwa Hii Rav 4 na Xtrail ya mleta...
Mwageni hizo oil muweke oil recommended
 
Oil recomended ni 0w20 hii tutapata wapi?
unasema oil ni 5w30 na 10w30 na hizo nyingine 20w50 na 10w60 ni za magari gani
 
Hata alivyonunua hiyo kapata ushauri. So anajaribu kupata maelezo mengine, maana hizi oil zipo nyingi sana na mbaya zaidi zile zikizoandikwa kwenye Vitabu vya gari hazipo huku kwetu ndio maana mada za oil haziishi.

Mfano mm gari yangu inatakiwa oil 0W20 lakini Nchi nzima hii hakuna unahangaika na mafundi wakutajie Equivalent yake Mara uambiwe ni 5W30 mara 20W50 mambo ni mengi
Sawa sawa lakini kwa hali yetu ya hewa na barabara mbovu, mara nyingi tunazipa engine kazi ya ziada hiyo 0w20 haifai kwa TZ...hiyo labda kule Canada kwenye barafu...kwa bongo kwa hiyo gari yake suluhisho ni 5w30
 
Daah aisee mkuu kesho hapa watakuja kulalamika oooh nissan hua zinazingua sijui nini,ile thread yako khs Nissan inajibu mengi sana khs mambo mengi sana + threads nyingine za wadau sema kama kawaida yetu hatupendi kujisomea somea.

Ukipata muda andika tu mkuu khs matumizi ya oil unaweza kusaidia watu wengi sana,tofauti na sasa ambapo watu wanapeleka gari kwa mafundi huku wakitegema fundi ndio awape ushauri na fundi mwenyewe ni wa chini ya mti hajui tech. ya kisasa ya magari inaendaje.
Na matumizi mabovu ya oil yamepelekea injini nyingi sana kufa,

Nitaandika tu hapa ili kila mtu ajisomee huenda tukaokoa kitu fulani
 
Mdau mimi ninamiliki ma nissan mwaka wa 10; kwenye oil achana na majaribio na mapicha picha tupia castrol hiyo 20w 50 (for old cars) zamani ilikua equivalent to Bp standard, ama Atlantic synthetic wachana na majaribio nissan inataka adabu, hizo oil zingine wacha watu wa Brand za wereva waweke
 
Back
Top Bottom