Nimeweka shabu maji lakini bado meusi?

Nimeweka shabu maji lakini bado meusi?

Kisima kina urefu Gani na kipo umbali Gani kutoka kwenye mifumo wa maji taka?
Usije ukawa unahangaika bure kumbe ni maji taka tu
futi kumi tu hamna mifumo ya maji taka,,, maji ya mvua labda huwa yanaingia ikinyesha kubwa
 
wataaalam wa teknologia ya maji

KAMA TUJUAVYO shabu inasafisha na kung’arisha maji.Nimenunua nimeweka kisimani lakin maji bado yana rangi ya juice cola!!

Mbinu gan nyingine

wataaalam wa teknologia ya maji

KAMA TUJUAVYO shabu inasafisha na kung’arisha maji.Nimenunua nimeweka kisimani lakin maji bado yana rangi ya juice cola!!

Mbinu gan nyingine ya kitaalam nimesahau
Hauweki tu mkuu!Lazima ufanye JAR TEST kujua optimum dosage utakayoitumia kusafisha maji yako.Na je unatibuje wakati ujui Turbidity(NTU) ya raw water yako.
 
futi kumi tu hamna mifumo ya maji taka,,, maji ya mvua labda huwa yanaingia ikinyesha kubwa
Kina futi 10, umbali wa kutoka kwenye nyumba ni kiasi gani? Maji taka hayahusu mifereji na mabomba tu kama wengi wanavyodhani, maji taka yako ardhini pia kutoka kwenye vyoo, mfano kisima futi kumi choo cha karibu kiko futi thelathini upande wa muinuko huku kisima kikiwa upande wa bonde, ni wazi kisima kitapata majitaka kutoka chooni, lakini kisima kikiwa upande wa muinuko na choo upande wa bonde ni wazi majitaka hsyawezi kupanda kwenda kwenye kisima, sasa wewe kisima chako kiko upande upi?
Jambo la mwisho, usitie shabu ndani ya kisima, shabu inawekwa ndani ya maji yaliyomo kwenye chombo, mfano tangi au pipa ambamo utajua ujazo wa maji na kiasi gani shabu inawekwa kwa lita moja.
 
kiko upande wa mwinuko choo kipo mbali bondeni
 
hii chloline inapatikana dukan ??
Zipo za vidonge na za maji zote ni maalumu kwa matumizi ya nyumbani tofauti na tunazotumia kuondoa madoa kwenye nguo hivyo zina maelekezo, nenda kwenye maduka makubwa ya dawa, uliza dawa ya kutibu maji.
 
Back
Top Bottom