“Nimeweka vocha ya 10,000 lakini salio limekuwa 10,000 tu… kampuni wanapata faida wapi?

“Nimeweka vocha ya 10,000 lakini salio limekuwa 10,000 tu… kampuni wanapata faida wapi?

Bila shaka wewe umeishia darasa la 3c ndiomaana umeshindwa kugundua utofauti wa hela na vocha pia umeshindwa kugundua jua vocha ni bidhaa ambayo inaweza kupanda thaman nakushuka
Sijawahi kuona vocha zimeshuka thamani.

Nimeishia form 5 mkuu.
 
Vocha yabuku hua haijumuliwi na mfanya biashara kwa buku (bei za jumla kwa vocha ya 1000 hua kati ya 950-970tsh kwaiyo
 
Kwa kifupi kabisa: wewe ukinunua vocha ya 10,000 na kupata 10,000, bado kampuni ya simu inapata faida — na faida yao haipo kwenye vocha yenyewe, ipo kwenye matumizi yako baada ya kuweka vocha.


1. Vocha siyo faida — matumizi yako ndiyo faida
Unaponunua vocha ya 10,000, kampuni haipati faida hapo. Hiyo ni kama kuweka pesa kwenye akaunti yako ya simu.

Faida yao inakuja pale unapoitumia hiyo pesa kwenye:
  • Kununua bando
  • Kupiga simu
  • Kutuma SMS
  • Kutumia M-Pesa/TigoPesa/Airtel Money (kuna makato)
  • Kununua huduma nyingine (kama Skiza, Caller tune, n.k.)

Mfano:
  • Ukiweka 10,000
  • Halafu unununua bando ya 10,000
  • Ile bando yenyewe tayari ina faida ndani yake (haupati GB halisi kulingana na thamani ya pesa yako)


2. Bando zina “margin” ya faida
Mfano wa haraka:
- Ukipewa 3GB kwa 10,000
Hiyo 3GB haijawagharimu 10,000 kutoa. Gharama yao halisi ya data ni ndogo sana kuliko bei wanayokuuza.

Hapo ndipo wanapopata faida kubwa.


3. Kwenye kupiga simu kuna bei ya dakika
Dakika moja ya simu inaweza kukugharimu:
  • 50/=
  • 80/=
  • 120/=
Lakini gharama yao halisi ya kuendesha mtandao kwa dakika moja ni ndogo sana.

Hapo pia wanapata faida.

4. Kwenye miamala ya pesa (mobile money) kuna makato
Hapa ndipo wanapata faida nyingine kubwa:
  • Kutuma pesa
  • Kutoa pesa
  • Kulipa bili
  • Lipa namba
Kila hatua ina makato.


5. Kuna huduma za ziada (value added services)
Mfano:
  • Caller tunes
  • SMS za matangazo
  • Huduma za kifedha (mikopo midogo midogo)
  • Internet ya muda mfupi (daily packs)


Kwa nini unaona kama hawapati faida?
Kwa sababu vocha ni kama “deposit” tu, sio bidhaa yenye faida.
Faida yao iko kwenye kile unachofanya baada ya kuweka vocha.

Kwa lugha ya mfano wa kawaida
Ni kama vile:
  • Unampelekea fundi 10,000 akununulie rangi
  • Lakini faida yake haiko kwenye ile 10,000
  • Faida yake iko kwenye kazi ya kupaka rangi atakayokufanyia

Vocha = pesa uliyopeleka
Huduma = sehemu wanayopata faida

Kutoka liwale-lindi
Japo umetoa maelezo marefu sana na sijaelewa kitu ila wewe umewazidi members wote waliochangia humu
 
Mfano umeweka vocha ya buku ukiangalia salio si unakuta buku ile ile tu, au?
Vocha ni bidhaa kama bidhaa nyingine, mfano ukinunua maji ya 600 utapewa 600. Ukinunua vocha ya buku kampuni za mawasiliano wameshapiga hesabu ya gharama ya wastani wa kiasi cha data, muda wa maongezi au meseji ambacho utatumia bila kupitiliza buku na hivyo wao watabaki na faida.
 
Vocha ni bidhaa kama bidhaa nyingine, mfano ukinunua maji ya 600 utapewa 600. Ukinunua vocha ya buku kampuni za mawasiliano wameshapiga hesabu ya gharama ya wastani wa kiasi cha data, muda wa maongezi au meseji ambacho utatumia bila kupitiliza buku na hivyo wao watabaki na faida.
Umejuaje mkuu, au na wewe una hisa huko Vodacom na ndo maana unajua mnavyopata faida?
 
IMG_7772.jpeg
 
Hapana Mkuu, vocha hiyo huwezi tena kununulia hata pipi. Waliochukua hela ndio wamefanya biashara hapo. Hela yako wanayo, na wewe una vocha yao.
Lakini unaweza kununulia dakika au sms mkuu
 
Umejuaje mkuu, au na wewe una hisa huko Vodacom na ndo maana unajua mnavyopata faida?
Ni rahisi kupanga bei ya kitu inayokupa faida mkuu, hesabu za biashara za pricing na break even point zinafundishwa darasani.
 
Nimekuwa nikijiuliza sana.

Nikiweka vocha ya 10,000 napata 10,000 exactly.

Sasa hawa makampuni ya simu wanapataje faida kama wanarudisha hela ile ile?
Au kuna kitu sielewi hapa?

Naomba nieleweshe kwa lugha rahisi maana kichwa changu kimegoma kabisa 😅
Walaji wa mwisho wengi ni maamuma!, ukimchanganulia ataona unamuibia,

kuna bidhaa ni tax included ili kuondoa sintofahamu kwa mteja...

Ndio maana ukiweka vocha ya mia5 wanakupa break down ya hiyo mia 5 yako...unakuwa umenunua muda wa maongezi wa 350 ,umelipa kodi, unapewa muda wa maongezi uliothaminishwa kwa hiyo shilingi mia 5 yako ili kuondoa hiyo sintofahamu

Wakikuambia huo muda wa maongezi wa mia5 ulionunua una thamani ya 350 utaona umeibiwa! Kitu ambacho si kweli.
 
Nafikiri vocha kwa mara ya kwanza kabisa ilikuwa mfano ukitoa 700 unapewa kikaratasi chako cha 500 baadaye kampuni za simu wakaona wafiche tu faida yao waikate ndani kwa ndani, kama vile siku hizi unavyoambiwa free delivery
 
Back
Top Bottom