Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Msaada wa kusemangwa?huo ni msaada!??unapewa huku unasimangwa?!!!acha zakooo...mbona kamshukuru aunt yake pamoja nakua alikua analala nje...
 
Pole sana ila Mungu yupo na anatuona kwa kweli...
 
Mimi nakushauri pambana na maisha yako na hayo ya nduguzo,hao waliokutendea ubaya achana nao,Wala usiwaulize kwa Nini walikutendea hivyo.
Mungu kakusaidia kufika hapoulipo wewe songa mbele tuuu,na jitahidi usiwe na kinyongo au kisasi moyoni
 
Watoto yatima wakimpata mtu wa kuwalea na kuwatunza kwa upendo huwa na furaha Sana,wanakuwa na ile kudekadeka ,hahahahahah
 
Pole saan ndugu yangu, maisha ni safari ndefu, funzo kubwa hapa hakuna kukata tamaa na wala hakuna shida za kudumu, matatizo yanakuja na yanapita.

Wakati mwingine yako unayaona mazito ila ukichungulia kwa jirani unaona bora wewe, ndio maana mtume alituusia tuwaangalie wa chini yetu wala sio waliotuzidi, hapo ndipo tutaona neema za mungu kwetu.
 
Pole mkuu na hongera sana stories inataka kufanana na yangu tofauti mimi sikuwaachia waendelee kutesa na Mali za wazazi wetu wakati kuna wadogo zetu walihitaji kusoma n.k Nilipo maliza kidato cha 4 Nilihakikisha nawafikisha mahakamani na nilirudisha Mali zote zisizo Hamishika, kasoro magari na mashine za kusaga ambazo zilikufa au kuuzwa.
 
Dunia hii inamambo mengi sana shukrani za dhati ziwaendee baba zangu wadogo wamenikuza hadi hapa, baba kapoteza 1997 na mother 2003 pindi nipo dalasa 3

Unakaa kwa mtu unaambiwa maneno makali sana, hakuna mtu anaejali walala nini ila katika wengi kuna wachache wanajali. nahishia hapa sitaka hata kukumbuka
 
Pole Sana.

Uyatima kumamaeeee
 
Pole sana Mkuu yote kwa yote Mungu ni mwema yamkini alipokupitisha ndiko kumekufanya uwe kama ulivyo sasa,
Yatima hadeki
N.B
Nje ya topic kama ikikupendeza basi siku moja tusimulie ni kitu gani kilipelekea mpaka uanze kampeni ya"KUTOOA"
 
hadi kufika hapo, ni Mungu amekusaidia, shangazi yako alitumika kama chombo tu. Mshukuru Mungu. wewe pia sio mtakatifu, unahitaji kuwasamehe hao ndugu zako wote unconditionally, ili Mungu naye akusamehe. hilo ni agizo la Mungu kusamehe watu ili na yeye atusamehe. usilipe baya kwa baya. pia, maadamu bado unaishi, hujafika bado, unaweza kushangaa kuna siku hao hao ndugu zako unaofikiri sio wa maana wakaja kukuokota huna hata uwezo kusogeza kiti ukae hata kama kazi au pesa unazo, pengine wameshajifikiria sana na kutubu kwa Mungu na Mungu amewasamehe lakini wewe bado unaendelea kuhangaika kuwahesabia uovu, wao walishamalizana na Mungu na wameshabadilika pengine ila tu ni ile aibu kwamba wanaogopa wataanzia wapo kukusogelea pengine sio ili wapate msaada toka kwako bali ili kurudisha relationship. fahamu hitu hiki, ndugu zako wa damu hata kama walishawahi kukukosa ni wa muhimu kwenye maisha yako walau kuliko kutokuwa nao kabisa. uwepo wao ni substantial walau kuliko kutokuwepo kwao kabisa. pia, mwanadamu huwa anabadilika, mtu mwovu huwa anaweza kuwa mzuri kuliko hata wewe uliyetendewa uovu naye. usiteseke kwaajili yao, kama kuteseka ungewaacha wao wateseke kwaajili yako, kama watakuwa hawajabadilika.

usijione umefika sasa ni wakati wako kushindana na wanadamu ili uwanyooshe kulipiza waliyokufanyia, kumbuka Mungu amekutoa mbali sana aisee, na hakukutoa mbali ili ufanye hivyo, yeye alitegemea wema wako ndio unaweza kuwabadilisha hao watu. ukifanya kosa la kuwa na kiburi hicho cha mafanikio, Mungu huwa anashusha mtu chini. jua kua Mungu huwa ana uwezo kumwinua mtu na kumshusha pia, na kama Mungu ni pendo, unafikiri anafurahia hayo unayoyawaza?

kitu kikubwa nilichojifunza maishani, mwanadamu akifanikiwa huwa anaamini amefanikiwa kwa nguvu zake/efforts zake, kumbe Mungu ndio amemfanikisha, usingefika hapo wala usingeandika na ungekuwa unatafuta ndugu zako hao sasaivi hata kama walikutupa, Mungu ni pendo kama anavyotupenda watu wote anataka hata sisi tupendane na kusameheana kama anavyotusamehe sisi pia.

sisi wengi tumeishi maisha magumu sana, mimi kuna ndugu mmoja alikuwa tajiri sana, alinitamkia waziwazi tena mbele za watu kwamba hawezi kunisaidia elimu yangu kwasababu hadi mimi nije nimsaidie yeye itakuwa lini? miaka 5 iliyopita alikufa baada ya kupooza kwa miaka 4 hatoki ndani. alikuwa na wake wawili, ameacha watoto wengi, hawajasoma, na mimi nahisi ninahitaji kuwasaidia watoto wake pia kama Mungu akinipa nafasi. yeye alikuwa mtoto ka baba yangu mdogo kabisa aliyekulia mjini, mimi nimekulia bush huko nimepita kwake wenzake wakamwambia anipe hata nauli tu inisaidie kwenda shule ndo akaongea hayo, lakini siwezi kulipa baya kwa baya kwasababu hata mimi Mungu amenisamehe mengi ambayo pengine nimewaumiza watu wengine. Mungu angehesabu maovu yetu nani angekuwa hai leo? au wewe ni mtakatifu mzee?

kwa wasomaji wote, Tupambane tutafute maisha, tuwe na maisha mazuri, lakini ukibarikiwa kimaisha, hakika usisahau vitu hivi:-

1. Ukiona yatima anahitaji msaada, fanya juu chini msaidie tena kwa moyo wote bila kuhitaji chochote toka kwake.

2. ukiona mnyonge au masikini, fanya hivyo pia.

3. samehe watu waliokukosea ili uwe huru, upate marafiki na ndugu wapya na ili Mungu akusamehe pia.

huu ndio ukweli mchungu ambao ndilo agizo la Mungu pia, na yeyote atakayefuata haya atabarikiwa.
 
Ulipigwa na chuma kizito
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...Nlishawahi kuambiwa Jangili mkubwa we nenda kaishi hata Zambia huko hakuna mtu atakae kutafuta..
 
Pole sana Mkuu yote kwa yote Mungu ni mwema yamkini alipokupitisha ndiko kumekufanya uwe kama ulivyo sasa,
Yatima hadeki
N.B
Nje ya topic kama ikikupendeza basi siku moja tusimulie ni kitu gani kilipelekea mpaka uanze kampeni ya"KUTOOA"
Achana na kuoa ila USISAHAU KUTAFUTA HELA.

#YNWA
 
Pole sana Mr. Liverpool![emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Umeniliza mama[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hasira za mama zako wadogo ndo unashushia watoto wa watu, nilitegemea ulivyoumizwa wewe usingekuwa unaumiza wengine,, kuanza PhD si mafanikio sana maisha yanaweza kukuchapa vizuri na PhD yako, ishi vizuri na watu punguza kiburi na majivuno,
Kwani nani kakuambia haishi vizuri na watu na ana majivuno? Yeye kajisemea wazi hataki kuoa. Si kosa kisheria wala kidini, ni uamuzi wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…