Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Kuna kale kamsemo kanasemaga adui yako ni mtu wa karibu... Au ule msemo mtegemea cha nduguye hufa masikini, ndugu wana maajabu yao na wanaweza kukuacha mdomo wazi
 
jamaa hajui kama hao ndugu zake, yawezekana wameshatubu kwa Mungu, wanaendelea na Mungu maishani, yeye amebaki na kinyongo na mzigo moyoni, na zigo hilo linamuumiza yeye zaidi ya hao ndugu zake, na akifa leo hii na zigo hilo anaenda moja kwa moja motoni. Mungu anasema ukitaka akusamehe dhambi, na wewe samehe wenzako, usipowamehe wengine hata Mungu hatakusamehe. kwahiyo kama yeye ni msafi kabisa hajawahi kumtenda Mungu dhambi basi asiwasamehe hao ndugu zake, ila kama na yeye ni mwanadamu kama tulivyo sisi wenzake, ni lazima asamehe na ajue kuwa mwanadamu mbaya wa jana anaweza kuwa mzuri wa kesho na akakusaidia kesho hata kama jana hakukusaidia. kukusaidia sio lazima pesa, kiburi cha uzima alichonacho sasaivi ndicho kinamdanganya ajione hawahitaji ndugu zake, Mungu akikipiga hicho kiburi utahitaji hata ndugu yako mmoja tu akutembelee hata kukutembelea tu. kuna siku atakuja kujua hili.
 
Aisee pole sana kaka, imenibidi nichimbue nijue nini kilijiri kwako. Mimi ni yatima pia 80% uliyoyasema nimepotia....uyatima unaumiza sana. Mno mno
 
Aisee pole sana kaka, imenibidi nichimbue nijue nini kilijiri kwako. Mimi ni yatima pia 80% uliyoyasema nimepotia....uyatima unaumiza sana. Mno mno
Mungu Mkubwa kwa maana TUMEFIKA japo sio juu ila ANGALAU TUMEFIKA.

#YNWA
 

Sijakwambia Nina NINA KINYONGO ila nimekwambia NAHITAJI TU KUWAULIZA.

ila pia NILISHAWA DELETE na hasa NDUGU WA MAMA Hawa ndio nadhani ni woteee NISHAWA DELETE.

Na Wala sina kisasi nao, ila waliamua kunitupa basi tuendeleze ile life style ya KUTUPANA.

#YNWA
 
Kuna Mambo mengi omba kuyasikia tu. kwa sehemu kuna baadhi ya mambo nimepitia kama wewe ikiwa ni pamoja na kutengwa na upande wa mzazi wetu aliefariki na upande wa ndugu waliyebaki hai walikuwa wanakuja kujibebea vitu kwa siri. ila mwisho wa siku nilikuja kujua ilikua ni umaskini tu. ILA UMASKINI NI MBAYA SANA mshua wenu alistahili kuwainua wengine kiuchumi maudhi ya dizaini hiyo yangepungua ila inaonekana ni kama yeye ndo alikuwa anategemewa na wengine wote hapo tatizo ndo lilipoanzia sasa.
 
Uyatima hauna mazoea..pole na hongera kwa kufika hapo ulipo.
Umeniliza aisee..wazazi wapumzike kwa amani
 
Mateso sio ishu saana, yatima kinachowaumizaga ni kunyanyaswa kukosa kupewa upendo, huwezi kumsaidia usimtamkie maneno mabaya, yupo mtu hapo anaumia akikumbuka ameishi maisha ya mtaani ili Hali yupo mkoa wa chimbuko lake kwenye ndugu zake. Jamaa alilala kwenye korido na kwenye Baraza ila rohoo kwatu sababu shangazi alimpenda. Huyo mke wa ba mdogo alipungukiwa nini mpaka a mwambie maneno Yale, yule alosema huoni ndugu wengine, siyo maneno ya kumuambia mtu. Ndo hayo hayafutiki kwenye kumbukumbu, watu hawalaumu ila wanaona kwa nini hawakuchukuliwa kama watu. Muonyeshe muhitaji upendo hatosahau na utabarikiwa. Ahimidiwe MUNGU baba wa yatima.
 
Kamwe hawezi kusahau, na siyo kusahau tu, ubaya ule unaweza ukamfanya aje kuwa mtu mbaya katika maisha yake, Hakuna aliyefilisika kwa kumsaidia muhitaji.
 
Pole sana yatima mwenzangu , ifike mahali basi sisi yatima tuungane tuwe na umoja wa kuwakomboa ndugu zetu , huko mtaani na pia kuwatetea mahali popote pale wanapoguswa maana ukipita kwenye familia nyingi , hakika yatima wanazalilishwa sana .[emoji24][emoji24][emoji24], watoto wa mtaani wengi ni yatima, hao panya roads wengi ni ndugu zetu , itoshe kusema kuna haja ya kuungana kukifariji kizazi cha watoto wanaoachwa na wazazi wao., financially , psychologically na responsible towards their future life.[emoji120][emoji120]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma hii nmejikuta tu nalia sijui hata nalia nini maana sijapitia hayo maisha nina wazazi wote wawili mpaka sasa ila maisha yalikua magumu tu wakati wa kusoma.
 
QURAN 4: 6

6. "Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni werevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri na ajizuilie(asiguse kabisa mali ya yatima), na aliye fukara basi na ale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao wekeni mashahidi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu."


 
QURAN 4: 9-10

9. "
Na wachelee (wasile mali ya yatima) wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli wahofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa"


10. Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni"
 
Nimesoma hadi nikajisikia uchungu pole sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…