Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Yatima hadeki...mkuu

Tupo wengi na tumekutana na mengi.

Tunayaishi kimya kimya tu...


Pole ndio ulimwengu ...muhimu kujielewa tu wewe ni Nani na uishi vipi..

Afadhali ya wewe hata shangazi alikuwepo...
 
Mungu azidi kukutunzia huo moyo ulionao..hata ikitokea umeoa (kama bado)basi mwanamke asijekuubadilisha.

Bravo 👊🏿👊🏿

Hata ikijakuwa kuwa ni Chakorii ....sitabadilika

Nimepitia maisha ya kuondokewa na mzazi mmoja nikiwa kwenye early teen age, kwa hiyo kwangu mimi ni wajibu kama sadaka kwa kutoa kidogo nilichojaaliwa ili ule ugumu niliowahi upata, wao wasiupate
 
Ningekuliwaza na kukupooza machungu, huwa napenda sana wadada wanaolia dawa yao ninayo😋
😀😀😀muone

Aise Nina huruma sana Kwa watoto ningekuwa hili swala ninauwezo nalo..hakika nisingeruhusu mtoto apitie changamoto kabisa.

Wiki kama mbili nilikutana na mtoto wa kiume(rika la kijana wangu kabisa)usiku Ana fanya biashara ya kuuuza nini Sijui huko aise nilimwaga machozi sana ujasiri sikuwa nao tena Kwa Yule mtoto.

Nikamwambia funga unachokifanya nifuate.nikampeleka sehemu ya kula ale akitakacho..aise mtoto alikuwa na njaa yule 🥺🥺🥺..nilikahoji kanandoto ni katoto ambako kapo kwenye plans zangu.haijalishi ndoto zangu zitawahi ama kuchelewa lakini lazima nikawe mbegu njema moyoni mwake.

Itoshe kusema ninahisia za karibu mno
 
Aisee hawa watoto wanatia huruma sana
 
Hata ikijakuwa kuwa ni Chakorii ....sitabadilika

Nimepitia maisha ya kuondokewa na mzazi mmoja nikiwa kwenye early teen age, kwa hiyo kwangu mimi ni sadaka na kusaidia kwa kidogo nilichojaaliwa ili ule ugumu niliowahi upata, wao wasiupate
Nimecheka tu..

Ikitokea basi kutakuwa na kusudi maalumu la Mungu
Alama nzuri tutakayoiacha duniani basi itakuwa ni ya kizazi hadi kizazi
 
Hasira za mama zako wadogo ndo unashushia watoto wa watu, nilitegemea ulivyoumizwa wewe usingekuwa unaumiza wengine,, kuanza PhD si mafanikio sana maisha yanaweza kukuchapa vizuri na PhD yako, ishi vizuri na watu punguza kiburi na majivuno,

Punguza makasiriko madam.....

Sina Hasira zozoteee.
Haya ndio maisha niliyo amua.

Mwezi wa 9 napanda ndege na 01/10/2022 nitakua darasani nikiianza safari yangu ya kuitafuta PhD.

Nimeamua kuchukua njia ya kutafuta hela na kusoma.
Hayo ya kuoa YANAWAFAA WENGINE.

Muda ni mdogo HATUWEZI FANYA YOTEE.

Mtu kuamua kuchagua njia ambayo huikubali haimaniishi yeye ana matatizo na wewe upo sawa.

Binafsi SINYWI POMBE KABISA, ila nadhani wewe unatumia ARE YOU JISIKIA NA MAJIVUNO PROBLEM WITH POMBE?

#YNWA
 
Sijasoma maelezo zaidi ya kichwa cha habari ila hii inatoa majibu kwanini hauamini katika ndoa.
Penda sanaa kusoma.

Kwanini hauamini katika muunganiko.

Kwanini hauamini katika watu kua pamoja, familia n.k.
Nina familia.
Nina binti Nampenda sanaa.
Mama ake aliolewa nikamuomba aniachie, akakubali.

Na nikienda kusoma PhD huko duniani NAONDOKA NAE.

Naamini sanaa kwenye familia ila FAMILIA HAINA UHUSIANO WOWOTE NA KUOA.
Now am not saying kila aliyepitia uyatima ana maoni yako but it obviously means ulipitia rough childhood.
Yap ilikua ni kipindi cha jasho na damu ila NILITOBOA.
Hope you will heal.
Yap, Majanga kwenye maisha ni mengi huja hili then hili.

Yale ya UYATIMA nishasahau.

#YNWA
 
Pole sana. Zamani nilikua najua mashangazi ni watu wa hovyo hawana msaada tofaut na ndugu wa mama. Hakika umeni-prove wrong.
Wapo mashangazi shetani Tena hasaa na wapo MALAIKA WEMA.
Wa kwangu alikua MALAIKA MWEMA.

#YNWA
 
Yani yatima kila kitu wanaona wanaonewa kumbe wanapigwa msasa wa maisha

Kuna story tulizozishuhudia tukianza kuhadithia hapa JAMII FORUM inabidi wajipange kwa server za ziada

POLE
Hongera sanaa mtoto wa kishua.

Ila usiombe ya kukute ma nigga
Usiombe ya kukute baharia.

Niliyopitia siwezi kumuombea mwengine yoyote yamkute.

#YNWA
 
Ni vizuri kuwa na hisia kama zako, lakini pia jifunze kuzi control kwa kujiambia huwezi saidia kila mwenye shida (huu ndio ukweli)...

Saidia unapoweza, pale usipoweza Mungu atainua mwingine...
Kuna wakati nashindwa kabisa.

Yes ni kweli kabisa Siwezi kusaidia kila mtu na hilo ninalifahamu sana tu na ndo mana nikasema ingekuwa niuwezo wangu..Kwa maana hiyo uwezo huo sina Watu8

Wengine nawaombea bila hata wao kujua(ingawa najua mimi ni mdhambi)lakini imani yangu kubwa maombi yangu yatawavusha sehemu fulani katika maisha yao
 
Mkuu pole sana aisee,ila uyatima unaumiza asikwambie mtu. Kuna muda nilikua nasoma story yako huku machozi yakinilenga.

Binafsi nimepitia hali hiyo katika maisha yangu yote mpaka sasa na bado napitia huko. Nahisi kama sijawahi kuipata furaha au faraja ya kweli hapa duniani.

Msoto ulikua ni mkali sana,ndugu wanageuka mashabiki wa shida zako na haters wa mafanikio yako. Na ndipo nilipoamua kuishi bila mawasiliano yoyote na ndugu yoyote mpaka sasa.

"Mama na ndugu zangu ni wale watu ambao kwa namna yoyote walininitia japo moyo pale nilipokua mtaani nikiishi kama chokoraa", period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…