Nimeziba jino zaidi ya mwezi nyuma, sasa hivi nikitafuna kama lina ganzi, nikibonyeza juu ya shavu kuna maumivu kwa mbali nayasikia, nini tatizo?

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Nimeziba jino mmoja ya hospitali hapa mjini sio vizuri kuitaja jina kwa sababu nitaharibu biashara ya watu wakaikimbia Dar.

Jino langu nimeziba zaidi ya mwezi wakuu siku ya kuziba nilichomwa sindano ya ufizi ganzi ikaingia uzuri nikafanyiwa harakati nikamaliza, nikarudia kama awamu mbili kisha wakaziba kabisa.

Sasa hivi hili jino ambalo nimeziba naona kama nikila kitu kama linafanya ile ganzi ya kuuma pale ninapotafuna ama ikitokea jino nimeligonga basi nahisi maumivu kama ya ganzi hivi nisipolifanya kitu haliumi.

Sasa nikibonyeza upande wa juu kule ambako nilichomwa sindano naona kama naskia maumivu hivi,tena ile sehemu ya maumivu iko sawa sawa na jino ukishuka kwa chini.

Je nini tatizo mpaka maumovu haya wana ndugu?
 
Mimi nisaidieni tu dawa ya jino, mke wangu anasumbuka sana
Dawa ya jino bovu ni kungoa,mengine yote ni mbwembwe tu mkuu,eti kuziba,Mara kulipiga shoti ya umeme,yote hii ni bure nenda kaongoe
 
Dawa ya jino bovu ni kungoa,mengine yote ni mbwembwe tu mkuu,eti kuziba,Mara kulipiga shoti ya umeme,yote hii ni bure nenda kaongoe
Hii kauli ya wakati wa zama za mawe haifanyi kazi tena sasa hivi.

Sasa mtu anazibwa jino anakaa nalo miaka 10 inaisha risasi anaenda kuziba tena miaka 10 hivyo hivyo mpaka anakufa na jino lake.

Wewe ng'oa jino ukaulizwe kwa nini umeng'oa wakati iliwezekana kuziba 😃😃😃😃
 
Nimeziba jino mmoja ya hospitali hapa mjini sio vizuri kuitaja jina kwa sababu nitaharibu biashara ya watu wakaikimbia Dar...
Pole Sana
Hilo walifanya RCT
MATIBABU YA mzizi wa jino
Na Hali kuwa obturated
Imepelekea kupata infections kupitia canal wazi
Tiba dawa waliyoziba itolewwe Na ufanye RCT UPYA
###0774891006

Sent from my MRD-LX1F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nisaidieni tu dawa ya jino, mke wangu anasumbuka sana
Zipo dawa za meno mzuri kwa ajili ya kutumia na meno hayaumi, kuna siku jino liliuma Kuna dawa nilipewa imeandikwa kama kihindi au kiarabu (sikuizingatia niliizadhau) ni nyekundu kuanzia tube yake mpaka dawa yenyewe na ina harufu ya karafuu ukitumia ipo vizuri sana.
 
Hiyo inaitwa dabur red.

Dawa yenyewe kama ina rangi nyekundu flani dawa kama pilipili, ndo dawa yangi saivi baada ya kuachana na sensodyne.
 
Pole Sana
Hilo walifanya RCT
MATIBABU YA mzizi wa jino
Na Hali kuwa obturated
Imepelekea kupata infections kupitia canal wazi
Tiba dawa waliyoziba itolewwe Na ufanye RCT UPYA
###0774891006

Sent from my MRD-LX1F using JamiiForums mobile app
Alaaa kumbe.
Sasa wakifanya tena hiyo RCT si utarudia tena au?
 
Pole Sana
Hilo walifanya RCT
MATIBABU YA mzizi wa jino
Na Hali kuwa obturated
Imepelekea kupata infections kupitia canal wazi
Tiba dawa waliyoziba itolewwe Na ufanye RCT UPYA
###0774891006

Sent from my MRD-LX1F using JamiiForums mobile app
Maumivu juu ya maumivu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hakuna kitu kinauma kama kurudiwa kutibiwa tena JINO aiseee

Na kama root canal treatment imefaul na kuna infection si kuna posibility kubwa ya kuvimbia usaha wa ndani (abscessed tooth) ?
 
Jino hata ukiziba kama limelika ,utakuja kung'oa tu hakuna namna mkuu bora unge ng'oa
Jino langu bado zima kijana.

Kuna jino ambalo limelika hasa hasa linafahamika,lakini pia daktari hakunishauri ning'oe kwa sababu halikufikia hatua ambayo wewe unaihukumu mkuu😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…