Pole sana mkuu nimeyasoma maelezo yako kwa makini, lakini pia nimeyasoma maelezo ya wachangiaji wengine. ushauri uliopewa na wachangiaji mwingine nauafiki mwingine naona kama ni mzaha.
Nimesene nina utalaamu wa kutosha kujibu swali lako. Hakuna uwezakano wowote na naomba nisisitize tena hakuna uwezokano wowote kwa mtalaamu yeyote kufahamu kama mama mjamzito alikuwa anashiriki matendo hayo au la, iwe wakati wa kujifungua au wakati mwingine wowote. Na tena makunga si kazi yao kuchunguza vitu hivyo na hawana ujuzi na utaalamu au vipimo vya kuchunguza hayo.
Na tena wakati wa kujifungua hakuna uhusiano wowote unaohusisha kutoka mtoto na njia ya haja kubwa japo ni viungo ambavyo vipo karibukaribu. Na tena hakuna hali imbayo hupata mama wakati wa kujifungua ambayo huwalazimu manesi wajaze pamba sehemu hiyo kama ulivyosema!
Nakushauri kama una ushahidi wa kutosha lalamika kwa mkuu wa hiyo hospitali kwa maandishi na dai fidia. otherwise wafungulie mashitaka kwa kosa la kukudhalilisha wewe na mkeo, kwa kitu ambacho hawawezi kukitolea ushahidi.